AMRAT KOMBO
New Member
- Oct 19, 2024
- 1
- 0
Bahati Issa Suleimani, mwenye umri wa miaka 51 , mwenye watoto 6 alithubutu kuwania nafasi mbalimbali za uongozi, ikiwemo ya katibu wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) katika mwaka 1995, na Mwenyekiti wa Umoja Wanawake Tanzania mnamo mwaka 2017.
“Katika mwaka 2020 niligombea nafasi ya udiwani, lakini kwa bahati mbaya sikufanikiwa, sikukata tama. hivyo niligombea tena nafasi ya Mwenyekiti Wanawake Tanzania (UWT) wa jimbo mwaka 2023 ila sikufanikiwa’’,alielezea.
Kukosa huko hakukumkatisha tama Bahati kwa kuamini iposiku atafanikiwa. Amesema ilimsikitisha kuwa sasabu ya kutofanikiwa ni kuona kilichothaminiwa katika hizo chaguzi ni pesa na sio utu na uwezo wa mtu.
‘’ Umaskini wangu ndio uliopelekea nikose nafasi kwani baadhi yawananchi waliona siwezi kuleta maendeleo kwakuwa sina pesa ,hivyo wakaona bora wasinipigie kura.”ameongezea
Alichobaini ni kuwa jamii iliyomzunguka ina mtazamo hasi juu ya wanawake kushiriki katika siasa na jambo la kushangaza ni kuona wanawake wenzake waliokuwa mstari wa mbele kumkandamiza.
“Ukiangalia nafasi ya udiwani wagombea tulikuwa 6 wanaume watano na mwanamke nilikuwa peke yangu na kwa nafasi ya ubunge wagombea wote watatu walikuwa wanaume. .”Amesema
Bahati ameniambia anaona ni vyema vyama vya siasa vikachukua juhudi za kuwainua wanawake kiuchumi ili hatimaye wawe na nguvu ya kugombea uongozi.
Safari haikuishia kwa Bahati tu niliendelea kusonga mbele hadi Kombeni na kukutana na Aisha Haji Mzee aliethubutu kuwania nafasi ya uwakilishi katika jimbo hilo.
" Katika mwaka 2020 nilithubutu kugombea uwakilishi katika jimbo la kombeni lakini sikufanikiwa kupata aliongea kwa masikitiko huku akitikisa kichwa."
Alisema kukosa fedha ndio kikwazo kilichopelekea kushindwa kwake, kwani hakua na uwezo wa kupiga kampeni ,kuandaa mikutano na kuwafikia watu kwa wakati. ingawa chama kilimsaidia lakini kilishiwa njiani kutokana na hali duni ya chama hicho. amesema
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa chamacha Adatadea Ali Makame Issa, amesema ukosefu wa Ruzuku kwa baadhi ya vyama vya siasa ni sababu kubwa ya kushindwa kusaidia wanawake kushika nafasi za uongozi.
“Ili chama kiweze kumsaidia wanawake kuingia kwenye nafasi ya uongozi kinatakiwa kiwe na Ruzuku ambayo itakayoweza kutatua changamoto wanayokabiliana nayo.”Amesema
Katibu Mkuu wa Chama cha Makini, Ameir Hassan Ameir, amesema bado chama chao ni kichanga na hakina vyanzo vya mapato ambavyo vingeweza kupunguza tatizo hilo, alipendekeza serikali itowe ruzuku maalum kwa wagombea wanawake ili kuwasaidia kutimiza malengo.
Ushauri huo umenifanya nitembelee ofisi ya msemaji wa serikali Hamza Hassan Juma ambae ni waziri wa nchi ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar na kueleza kuwa serikali inatoa ruzuku kwa kufuata sheria.
" Kifungu cha 16 cha sheria ya vyama vya siasa hairuhusu kila chama kupewa ruzuku isipokuwa chama ambacho kina uwakilishi ndani ya Baraza la Wawakilishi, au chama ambacho kimepatakura nyingi." Amesema
Hata hivyo, amesema ruzuku sio sababu ya kuwazuia vyama vya siasa kusaidia wanawake kuingia katika uongozi kwa sababu vyama vya siasa vinatakiwa kutoa michango katika matawi yao ili kusaidia shughuli za kisiasa.
“Serikali haitoi ruzuku kwa vyama visivyotimiza vigezo vya kupewa Ruzuku kama vile kuwa na wanachama wachache wa kuweza kuwaweka viongozi wao katika chombo cha kutunga sheria ”Amesema
Hata hivyo, zipo taasisi zinazohamsisha wanawake kujikomboa kiuchumi kwa lengo la kuwasaidia katika harakati za kisiasa .Katika Idara ya Maendelao ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto niliongeana na mkurugezi wa idara hiyo, Siti Abasi Ali, Amesema
Wamehamasisha vikundi mbalimbali vya wajasiriamali wanawake kuchukuwa mikopo isiyo na riba ya viko 19 ambayo itawasaidia kuimarika kiuchumi na kuwajengea uwezo katika shughuli zao za kisiasa.
“Tumepata vikundi vya wajasiriamali wanawake 1,971 vikiwa na wanawake 59,753 lengo ni kuhamasisha wanawake waweze kufanya biashara ili kuhakikisha wanapata fedha ambayo itawainua kiuchumi katika kugombea nafasi za uongozi.
Amewashauri wanawake kuchangamkia fursa za mikopo iliyopo ili kuwasaidia katika shughuli zao za kimaendeleo na kisiasa.
Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tamwa – Zanzibar kinatoa mafunzo ya uongozi kwa wanawake na kutatua changamoto zinazowakabili.
Mkurugenzi wa Chama hicho Dkt.Mzuri Issa alikiri kwa masikitiko kwamba wanawake wengi wamekumbana na changamto walipotaka kugombea uongozi.
“Tumetoa mafunzo ya uongozi kwa wanawake kwa kushirikiana na Jumuiya ya wanasheria wanawake Zafela na zidi ya wanawake 100 tumewapatia mafunzo hayo Unguja na Pemba. Tulichogungundua ni asilimia 50 ya wanawake wamekutana na changamoto ya uchumi.”Amesema
Ukiangalia wawakilishi wa majimbo 50 Zanzibar wanawake 8 sawa na asilimia 16,wabunge wa jamuhuri ya muungano kutoka Zanzibar kwenye majimbo 50 wanawake wanne ,sawa na asilimia 8 mawaziri 6 sawa na asilimia 33,makatibu wakuu 7 sawa na asilimia 39.
Kwa upande wa wakuu wa mikoa mwanamke mmoja sawa na asilimia 20,wakuu wa wilaya wanne sawa na asilimia 36 na masheha wanawake 79 sawa na asilimia 20, wanaume 309 sawa na asilimia 80 kwa masheha wote wa Unguja na Pemba ambao ni 388.