SoC02 Uchumi na Maendeleo

SoC02 Uchumi na Maendeleo

Stories of Change - 2022 Competition

Ali Nassor Px

JF-Expert Member
Joined
May 6, 2022
Posts
2,384
Reaction score
3,926
UTANGULIZI

Uchumi ni nini?
Uchumi ni hali ya ukuaji au udororaji wa kiwango cha hali za kimaisha kwa jamii husika , au tunaweza kusema kuwa uchumi ni msingi mkuu wa maendeleo kwa taifa unaorabitiwa kutokana na rasilimali zilizopo ndani ya taifa husika.

Vipo viashiria mbalimbali vinavyonesha kuwepo kwa hali nzuri au hali mbaya ya kiuchumi katika taifa husika. hali hizo zinatokana na sababu mbalimbali zilizopo katika taifa husika.

Hali nzuri ya uchumi ushajihishwa na mambo mbalimbali , miongoni mwa mambo hayo ni kama ifuatavyo ;

Elimu ; Hii ni moja ya nyenzo muhimu sana katika ukuaji wa uchumi. awali uchumi uibua maarifa mengi juu ya namna gani uchumi hususishwa na vile vile kusaidia kutoa muongozo au muelekeo wa uchumi husika kutokana na takwimu mbalimbali zinazofanywa kupitia watafiti wa uchumi.

Nguvu kazi ; Bila kuwa na nguvu kazi ya kutosha ( Vijana wenye uwezo wa kufanya kazi ). Uchumi hauwezi kustawi kwa sababu vijana ndio nguzo imara katika ukuaji wa uchumi kwa taifa lolote.

Teknolojia na Rasilimali ; Kama tunavyojua kuwa maendeleo ya ukuaji katika taifa lolote lile uchochewa na uwepo wa teknolojia na rasilimali za kutosha ili shughuli za kiuchumi ziweze kupata msukumo. Mfano mzuri wa tenknolojia zinazoweza kusaidia uchumi kukuwa katika taifa ni viwanda vya kisasa vya uzalishaji wa gesi asilia dhidi ya matumizi ya kuni au mkaa.

Uzalendo ; Bila ya uzalendo katika taifa hapawezi kuwepo kwa ukuaji wa uchumi. kwani kila taifa lililoendelea kiuchumi basi uzalendo ulitangulia kabla.

Mfano mzuri ni kama nchi ya China ambapo ilipata maendeleo makubwa baada ya kuwepo kwa uzalendo wa wananchi juu ya nchi yao.

Pamoja , na hayo yote tuliyoyaelezea ambayo uashiria uwepo wa hali nzuri ya kiuchumi katika taifa pia zipo changamoto zinazopelekea zinazopelekea udororaji na hali mbaya ya uchumi katika taifa na miongoni mwa changamoto hizo ni kama zifuatazo ;


CHANGAMOTO

Miundombinu duni ; ili taifa lolote lipate maendeleo ni lazima pawe na miundimbinu imara . Hivyo basi miundombinu duni ni kikwazo kikuu cha ukuaji wa uchumi ndani ya taifa lolote , kwani bila ya uwepo wa Barabara nzuri , Madaraja , viwanja vya ndege , Bandari . maendeleo ni vigumu kupatikana.

Ukosefu wa takwimu na mipango ; Bila ya takwimu hapawezi kuwepo ukuaji mzuri wa uchumi kwa sababu tafiti ndio uonesha, Dira na muelekeo wa maendeleo kwa taifa lolote . Mfano mzuri Uwepo wa utaratibu wa Sensa ya watu na makaazi wenye lengo la kutathimini hali ya taifa kwa sasa na baadae.

Vilevile Urasimu ; huweeza kuwa ni changamoto moja wapo ya udororaji wa uchumi katika taifa kwani husababisha wale wenye uwezo kuratibu na kusimamia masuala ya maendeleo kutopewa kipaumbele kutokana na uwepo wa urasimu katika taifa.

Kutokana na hali hizo tulizojionea , tumeweza kufahamu mambo mbalimbali yanayohusiana na maana halisi ya uchumi na Sababu zinazopelekea ukuaji wa uchumi na mambo yanayosababisha udororaji wa uchumi katika taifa ( changamoto).

Hivyo basi , yapo mambo mbalimbali yanayotakiwa kwa taifa lolote kiujumla kuyafanyia kazi au kuyasimamia ili yaweze kuleta tija kwa kuinua uchumi kwa lengo la kuinua uchumi na kuleta maendeleo.

Miongoni mwa hayo ni kama yafuatayo.

i. Utoaji wa elimu inayomsaidia mwananchi.

• Elimu uwepo na uboreshwaji wa elimu ambayo itamsaidia muhitimu baada ya masomo yake. mfano mitahala ya elimu isigemee zaidi kwenye nadharia zaidi iegemee pia upande wa vitendo ili isaidie kuzalisha wataalamu wengi zaidi . au ikiwezekana itakuwa vizuri zaidi kwenye elimu ya awali pawepo na Somo la Ujasiliamali Mali .

ii. Serikali iwe na nidhamu katika sera za mapato na matumizi

• Serikali iwe inapanga na inatumia pesa katika vipaumbele vya sera zake na kuwa na usimamizi mzuri. katika matumizi ya kila siku. Usimamizi mzuri unasisitiza kuwa na tija katika matumizi ya serikali.
Gharama za kununua Bidhaa/ Huduma ziwe chini huku ikizingatia ubora wa bidhaa na huduma husika.


iii. Serikali ipanue zaidi wigo wa kodi ili itegemee pesa zinazozalishwa na nchi zaidi kuliko wahisani

• Ingawa sasa hivi tunaweza kukopa zaidi kutokana na uchumi tuliokuwa nao ila. kukopa bila mipango na kwa riba kubwa, tunaweza kujikuta tupo kwenye kundi la nchi fukara (Low income economy) na atuendi mbele.

hivyo serikali ijitahidi kupanua wigo wa kodi kutoka kwenye vyanzo vyake vya mapato zaidi kuliko kutegemea sana misaada ya wahisani.

iv. Serikali iwe na vipaumbele vichache vitakavyoleta manufaa mengi kwa wananchi / nchi ambalo ambavyo vipo ndani ya uwezo wetu

• Pesa zinazowekwa kwenye vipaumbele ziwe na matokeo mazuri. serikali iweke vipaumbele vichache venye maslahi mapana. Mfano :Kama serikali itajikita kwenye kilimo basi pawepo na hamasa kwa wananchi na pembejeo yenye ubora na zinazoendana na mabadiliko ya tabia ya nchi ziwepo , lakini pia yote hayo yaambanate na soko la uhakika.

v. Serikali itengeneze mazingira rafiki kwa wananchi kulipa kodi

• Utoaji wa elimu ya ulipaji wa kodi pia pawepo na uboreshwaji wa huduma za kiserikali. Serikali iweke tozo zake ndogo kwenye huduma ndogo makato ya serikali yasiwe juu sana kwani upelekea wananchi kuachana na utumiaji wa huduma hizo.

vi. Kufufua na kuboresha miradi na miundombinu yote yenye maslahi na nchi*

• Kuboresha miradi na miundombinu inaenda moja kwa moja kukuza pato la taifa na kuinua uchumi. utengenezaji wa Barabara , Madaraja , Viwanja vya ndege urahisha upatikanaji wa huduma/ bidhaa kwa wakati, pia inachochea uwekezaji ndani ya nchi na kuzalisha ajira kwa wingi.

USHAURI

kwa mujibu wa Bank ya Dunia wastani wa pato la mtu mmoja mmoja (Per capita income) ni chini ya dola 1 lakini tulipokuwa katika awamu ya tano ya Hayati. Dr. John Pombe Magufuli tulifikia uchumi wa kati uchumi uliodhoofu. unaanzia $1,036 hadi $4,045. Sisi wastani wa pato letu ni $1,080.

Chanzo "www.worldbank.org"
lakini hivi karibuni tumetoka kwenye wa uchumi wa kati na tumeshuka zaidi. kutokana na majanga kama UVIKO 19 (Covid -19) na Vita ya Ukraine na Urusi.

Kuna hatari inaonesha kuwa malengo yetu ya Mwaka 2010 ya Dira ya maendeleo ya taifa (Tanzania Development Vision 2025) na tuliweka lengo la kufika Uchumi wa kati wa wastani wa Pato la mtu mmoja mmoja kuwa $3,000 ifikapo mwaka 2025. chanzo " www.tanzania.go.tz "(tovuti kuu ya serikali).

Kuna hatari tusifikie malengo tuliyoyaweka kwa wakati.

Hivyo, basi tunaishauri serikali ni vizuri kuwashirikisha wananchi wote kuamua ni maendeleo yapi wanataka na vipaumbele vipi wanahitaji . ushirikishwaji na uhimizwaji watanzania wote hata wa huko nje ya nchi kujihusisha na maendeleo ya nchi yetu.

picha kutoka mtandaoni.
View attachment 2323410
 
Upvote 8
nawakalihisha wote kwa ajiri ya majadiliano juu la andiko langu pia nilikuwa naomba mulipigie kura andiko hili.

ASANTENI SANA.
 
Nimeshapiga Kura mkuu....andiko zuri na umegusia mambo mengi ambayo ni kikwazo Kwa ukuaji wa uchumi na vile vile umetoa jawabu ya nini kifanyike ili uchumi uweze kukua...

Kuna Jambo moja limenivutia zaidi kuhusiana na serikali kuweka tozo ndogo ktk huduma mbali mbali ili WANANCHI wapate kuendelea kutumia huduma hiyo....mfano mzur ni hivi karibuni kulipokuwa na ongezeko la Makato ya huduma za kutuma na kutoa hela ktk Simu....ilileta kelele nyingi na hata kufikia baadhi ya watu kusitisha kutumia huduma hiyo....hasara yake ni kwamba wananchi wanakosa huduma na serikali nayo pia inapoteza mapato
 
Nimeshapiga Kura mkuu....andiko zuri na umegusia mambo mengi ambayo ni kikwazo Kwa ukuaji wa uchumi na vile vile umetoa jawabu ya nini kifanyike ili uchumi uweze kukua...

Kuna Jambo moja limenivutia zaidi kuhusiana na serikali kuweka tozo ndogo ktk huduma mbali mbali ili WANANCHI wapate kuendelea kutumia huduma hiyo....mfano mzur ni hivi karibuni kulipokuwa na ongezeko la Makato ya huduma za kutuma na kutoa hela ktk Simu....ilileta kelele nyingi na hata kufikia baadhi ya watu kusitisha kutumia huduma hiyo....hasara yake ni kwamba wananchi wanakosa huduma na serikali nayo pia inapoteza mapato
asante sana ndugu kwanza kwa kulielewa andiko langu pia kwa kunipigua kula asante sana ndugu
 
Hongera muandishi kwanza umetumia lugha safi kabisa ya kiswahili fasaha Cha pili andiko linafutia kulisoma . Cha tatu umeandika njia za kutatua tatizo kiufupi hongera sana
 
Hongera muandishi kwanza umetumia lugha safi kabisa ya kiswahili fasaha Cha pili andiko linafutia kulisoma . Cha tatu umeandika njia za kutatua tatizo kiufupi hongera sana
asante sana ndug
 
Habari yako ndugu Ally Nassoro Px

Hongera kwa nakala nzuri yenye mawaidha na tija kwa jamii.

Kura yangu umepata!!

Nikiamini katika uchakataji wako wa mambo na uwezo wako wa fikra na ubunifu, naomba ukipendezwa, nipate mawazo yako au mapendekezo juu ya nakala ihusuyo


Ahsante!!
shukran mkuu acha nisome ss andiko lako
 
Back
Top Bottom