SoC01 Uchumi shirikishi kwa kila Mtanzania

SoC01 Uchumi shirikishi kwa kila Mtanzania

Stories of Change - 2021 Competition

Mgaya123

New Member
Joined
Mar 4, 2019
Posts
1
Reaction score
0
UCHUMI SHIRIKISHI KWA KILA MTANZANIA

Kila binadamu kwenye jamii yoyote anapenda kuisha maisha yenye mafanikio na maendeleo, hata hivo maisha hayo hutegemea utashi wa mtu binasfi kuchangamkia fursa na fursa zinazopatikana mazingira aliyopo. Lakini pia sisi wananchi tunategemea serikali kututengenezea na kuturahisishia mazingira ya mihangaiko yetu ya kila siku. Ni ukweli usiopingika kwamba kila taifa linapenda liwe na uchumi imara kwa maendeleo ya nchi na raia wake, lakini swali linakuja ni namna gani kila mwananchi atakuhusika kujenga uchumi wa nchi na kujipatia kipato chake.

Sote tunajua swala la nguvu kazi katika nchi yeti sio tatizo, tatizo kazi ni chache na za kugombaniwa, ukianzia hata wale wanaofanya vibarua vya kulipwa kwa siku upatikanaji wake bado ni shida, kupitia hili unaweza ukaona taifa linapoteza nguvu kazi kiasi gani.

Hebu fikiria ikiwa kila mtanzania mwenye uwezo wa kufanya kazi akiwa busy kwenye shughuli yake ya uzalishaji, bila shaka italeta mabadiliko makubwa kiuchumi na kibishara. Tunahitaji kila mwanachi ajikite kwenye shughuli za uzalishaji kulingana na taaluma yake, kipaji, ujuzi wake n.k. Kila sekta ikiwa na msawaziko wa nguvu kazi, ni rahisi kuwa na uchumi changamfu. Kwa mfano ukiangalia upande wa bodaboda, hakuna usawaziko kati ya uhitaji na bodaboda wenyewe maana kuna wakati mwingine mtu anakaa mda mrefu bila kupata abiria, hii inaonyesha ni matumizi mabaya ya nguvu kazi. Lakini inawalazimu watu wafanye kazi hata kama hawaitaki ili kujiingizia kipato. Kama kungekuwa na kazi nyingine hii nguvu kazi ingehamia huko.

Swali muhimu tunalotakiwa kujiuliza ni kwanini mtu anamua kuacha pesa benki bila kufanyia chochote kwa mda mrefu, wakati hiyo pesa ingeingizwa kwenye mzunguko ingeweza kuajiri watu, yeye mwenyewe kujipatia kipato na serikali pia kupata kodi.

Game changers katika nchi yeti ni wachache sana, hapa nazungumzia watu kama Bahresa, Mo Dewji na wengineo. Kwahiyo tunahitaji wenye mitaji ya chini na ya kati wawekeze kwenye sekta mbalimbali, kati ya milioni 100 mpaka billion 2 za kitanzania. Kwenye kundi hili tuna uwezo wa kupata wafanya biashara wengi sana. Kila atakayekuwa na uwezo awekeze hata kiwanda kidogo cha watu watano. Tuchulie watu watakaoitikia wito wa kuwekeza na kufungua biashara mpya kwa kiwango cha chini wawe 20000 Tanzania nzima na kila biashara iajiri watu angalau watano, hili linawezekana ila je hawa walengwa wanaona fursa ambazo wanaona wakiwekeza pesa zao watafanya biashara? Tunahitaji taasisi ambazo zitwaonyesha masoko na njia za kuwafikia. Tukifanya hivo kiuchumi italeta afya sana.

Kama nchi tunahitaji kuwaonyesha na kuwashawishi wawekezaji wadogo na wa kati fursa zilizopo ndani na nje ya nchi. Taasisi za serikali kama TCCIA, TANTRADE, TIC, NDC, Tanzania business council, Balozi zetu nje ya nchi n.k, ndio zinazowajibika kufanya haya ili watu wawe na taarifa mbalimbali. Ikiwezekana hizi taasisi zitanue wigo zaidi wa kuwafikia watu wenye mitaji midogo na ya kati kwa kuwapa taarifa za fursa mbalimbali. Mfano ubalozi wetu uliopo China wanajitahidi kufanya vizuri kwa kutoa taarifa mbalimbali za fursa zinazopatikana china, wamefikia hatua mpaka wameanzisha podcast kwa ajili ya kutoa taarifa tofauti tofauti, rejea hapa (Tanzania Embassy Beijing Podcast). Tunahitaji kila mwenye mtaji wa kufanya kitu awekeze sekta inayomfaa ili kuongeza mzunguko wa pesa iwe ni bishara, au sekta ya kilimo, viwanda vidogo vya uzalishaji n.k.

Marehemu Ruge aliona mbali sana kwa kuanzisha semina za fursa na kuzunguka Tanzania nzima(heshima zimwendee popote alipo), ila wengi waliokuwa wanahudhuria semina hizo ni vijana ambao bado hawana mitaji. Ulikuwa ni mpango mzuri sana kama walengwa wangekuwa wanahudhuria, kuna wakati fulani pia marehemu raisi John Pombe Magufuli aliitisha kikao na wafanyabiashara watano kila kila wilaya kuwapa imani na serikali yao. Hii ni namna mojawapo ya kuweza kuwakusanya watu na kutoa fursa zinazopatikana kila eneo ndani ya nchi na je ya nchi yetu.

Kuna changamoto tatu ambazo naziona, ya kwanza ni wafanyabishara kutokuwa na imani na mfumo wa serikali kibiashara, hapa namaanisha kodi, vikwazo na urasimu tofauti tofauti. Hili limekuwa ni lalamiko la wafanyabiashara wengi ndio maana wakati mwingine mtu anaona ni bora atunze pesa zake kwa kuwekeza sehemu ambayo mzunguko wa pesa unakuwa dhaifu, kwa mfano majengo.

Changamoto ya pili ni kukosa taarifa mbalimbali za fursa za kibiashara, kama nilivosema hapo mwanzo serikali ina uwezo wa kukusanya taarifa za wafanyabiashara wenye mitaji ya kuweza kufanya uwekezaji wa chini na wa kati(maana hapa tunategemea tutapata watu wengi zaidi) na kufanya upembuzi yakinifu wa fursa tofauti tofauti na kuwapa wafanyabiashara wafanyie kazi hizo taarifa. Kupitia hili unaweza kuanzaishwa mfumo wa kutoa taarifa na dondoo mbalimbali kwa wafanyabiashara kila mwezi au wiki kwa gharama ndogo ili mfumo uwe endelevu.

Na changamoto ya tatu ambayo ni muhimu sana ni kukosa watafiti wa fursa za ndani ya nchi na nje ya nchi yetu ambao watatupa taarifa mbalimbali za masoko yanayopatikana ili watu waweze kuzikimbilia hizo nafasi. Kabla hatujaenda mbali ulaya na America, tukaanza na nchi jirani kama Rwanda, Congo, Zimbabwe, Zambia, Burundi, Angola, South Africa, Botswana na nyinginezo ambao watakuwa wanatuletea taarifa halafu tunawafikishia wafanyabiashara.

Nafikiri hili ni wajibu wa TIRDO(Tanzania Industrial Research and Development Organization), kitengo chao cha utafiti wa wamasoko wanaweza wakakiongezea nguvu kwa kuhakikisha taarifa za kibiashara zinawafikia walengwa na pia kuongeza idadi ya watu wataokuwa wanfanya utafiti wa masoko nje za nchi. Hapa gharama inaweza ikawa kikwazo ila ukitengenezwa mfumo wa uanachama ambao utakuwa unatoa hizo taarifa unaweza kuziba hilo pengo ili kazi iende vizuri. Tuchukulie mfano wafanyabiashara 50000 wamejisajili kwenye huo mfumo na ada ya kupata hizo taarifa kwa mwezi ni shilling elfu hamsini, inamaana jumla ya mwezi inakuwa ni shilling 2,500,000,000.

Bila shaka hiyo inakuwa pesa ya kutosha kuweza kuendesha huo mchakato, kwa maana kwamba itumike kulipa mishahara wa watafuta masoko na pia kuendesha mfumo. Jambo la msingi litakalotakiwa hapa ni kuhakikisha taarifa zinazotolewa na wahusika ziwe zimefanyiwa upembuzi yakinifu na zenye tija ili wadau watakaojiunga na huo mfumo waone thamani ya kujiunga. Sote tunajua takwimu na taarifa za kibishara ni dhahabu, wahusika wakiweza wakulifanyia kazi hili jambo wakilifanya kwa usahihi litaleta tija sana kwa maendeleo ya uchumi wa nchi yetu.

Kwa ujumla mdau wa kwanza kwenye hili ni taasisi za serikali zilizoanzishwa na serikali kwa lengo la kumuunganisha mwanachi na masoko mbalimbali yanayopatikana ndani na nje ya nchi. Hizi taasisi zijiangalie vizuri malengo mahsusi ya kuanzishwa na je yanatekelezwa? Kama hayatekelezwi nini kikwazo?

Penye vitu vizuri hakuna asiyetaka kusogelea, wakijipanga wakatengeneza mazingira mazuri kila mwenye uwezo atataka kujua anaweza kupata kitu gani. Mabadiliko yanawezekana ni sisi tu kubadilisha fikra zetu!
 
Upvote 2
Back
Top Bottom