SoC02 Uchumi Tanzania

SoC02 Uchumi Tanzania

Stories of Change - 2022 Competition

Nyaganilwa N

New Member
Joined
Aug 12, 2022
Posts
1
Reaction score
0
Nianze kwa kutoa pongezi na shukrani za dhati kwa serikali ya awamu ya sita (6) ikiongozwa na Mh.Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kupambana na hali ya uchumi wa nchi yetu kila siku.


Ningependa kujikita katika sekta ya uchumi maana ndiyo inayopambaniwa sana kwa sasa ,Kama mwananchi mwenye nia njema na nchi hii kiuchumi ,nimeona sekta ya michezo nchini inakua kwa kasi mno ,ambapo serikali hainabudi kuwekeza zaidi katika michezo ili kujiingizia mapato zaidi.

FB_IMG_16599873676175919.jpg


Ni wazi kuwa asilimia kubwa ya watanzania wanapendelea michezo sana kama ukifuatilia katika mitandao ya kijamii ,hivyo basi ,serikali ijaribu kuwekeza katika michezo kuliko kuendelea kutegemea kodi na makato mbalimbali yanayoumiza wengi.


Viwanja vya michezo ni moja ya changamoto kubwa ,serikali haina budi kuliangalia hilo ,pia usimamizi wa sekta hii ni mdogo mno ukilinganisha na sekta zingine ,na mengine mengi ,ningependa kuishauri serikali ijikite katika masuala hayo kimichezo.


Lakini pia maamuzi ya serikali ya shirikisho la mpira nchini ,yamekuwa yakichelewa mno kanakwamba hamna katiba inayotuongoza kimichezo ,hapa naongolea kwenye ukiukwaji wa sheria za mpira nchini ,jambo linalopelekea kucheleweshwa kwa mapato serikalini na ukomavu kwa vilabu vyetu nchini na kimataifa.

Kama ni mfuatiliaji mzuri wa sekta ya michezo nchini ,utagundua kuwa uwakilishi wa vilabu vyetu kimataifa umekuwa ni mkubwa na wa uhakika tofauti na miaka kadhaa iliyopita , utakuja kugundua kuwa ,mbali na kuingiza kipato kupitia mafanikio ya vilabu hivyo kimataifa ,bado nchi inafaidika kwa kutangaza sekta zingine kimataifa ikiwemo utalii.

Hatuna budi pia kuwashukuru wawekezaji ,mashabiki na wadau wa mpira kwa ujumla ,kwa kutokata tamaa mbali na changamoto mbalimbali wanazopitia katika kuendesha shughuli kubwa za mpira wa miguu nchini ,shukrani za dhati ziwafikie popote walipo ulimwenguni.

Yote haya yatawezekana kwa ukubwa zaidi endapo tu ,serikali itaamua kuweka nguvu kubwa katika sekta ya michezo kimataifa na kusaidia vilabu vingine ambavyo havishiriki kimataifa miaka ijayo navyo viweze kushiriki na kuongeza pato la taifa zaidi.

Lakini ukiachana na mpira wa miguu pia kuna masumbwi ,moja ya mchezo unaokua na kuongeza wafuatiliaji kila siku nchini ,hivyo basi serikali ione namna ya kuboresha mchezo huu ili iweze kujiingizia mapato zaidi kwa kuwekeza katika sekta hii pia.

Ni jambo zuri mno endapo serikali itajaribu kutatua changamoto mbalimbali zinazoikumba sekta ya michezo nchini.

Tunatazamia kuwa moja ya waandaaji wa michuano ya kimataifa Afrika katika mpira wa miguu ,jambo ambalo ni zuri na linaweza likaishia kuwa kama ndoto endapo serikali haitaona umuhimu na ukubwa wa sekta ya michezo nchini , hivyo basi , angalau tungekuwa na viwanja vya mpira wa miguu visivyopungua vitano (5) vyenye hadhi ya kimataifa ,nasisi tungesema tunauwezekano mkubwa wa kuwa wenyeji wa mashindano hayo.

Endapo tutapata nafasi ya kuwa wenyeji wa mashindano hayo ,nchi itafaidika kutoka ngazi ya familia mpaka taifa kwa ujumla ,maana tutapokea wageni wengi kutoka mataifa mbalimbali ,wananchi tutafanya biashara zetu ndogondogo mfano nyumba za wageni ,vyakula n.k ,serikali itajipatia fedha za kigeni lakini zaidi sekta ya utalii itakua kwa kasi kubwa sana.


FB_IMG_16376477884411311.jpg


Ni jambo la kushangaza sana kuona kiongozi mkubwa tunayemtegemea aweze kulisongesha gurudumu la michezo nchini ,bila kujali ukubwa au udogo wa vilabu ,naye anaweka mbele ushabiki wa kilabu fulani ,viongozi tubadilike sisi wananchi ndio tuliowaweka katika nafasi hizo mlizopo ,msitumie ukubwa wa madaraka yenu kuvibeba baadhi ya vilabu ,bali nyie ndio muwe njia na milango ya vilabu vingine kupenya kimataifa.

Tunatamani sana ligi kuu nchini iwe ni moja ya ligi bora Afrika na ulimwenguni pia kwa kufuatiliwa na watu wengi kama ilivyo ligi kuu ya uingereza (England Premier League) ,serikali itajiingizia mapato ya hali ya juu ,na kusaidia kuweka sawa hali ya uchumi nchini.

Najaribu kuvuta picha sherehe za kusherehekea kuzaliwa kwa vilabu mbalimbali mfano ,Simba day ,yanga day ,jambo ambalo mpaka vilabu vingine nchini vimeanzisha baada ya kugundua kuwa kuna namna kilabu chao kinaweza kujiingizia mapato kupitia mashabiki na kuongeza uwekezaji pia ,sitoshangaa kuona serikali inajiingizia mamilioni endapo tu ,tutapata nafasi ya kuwa wenyeji wa michuano ya bara la afrika.

FB_IMG_16599756626781337.jpg


Lakini pia sitoshangaa kuona tunafunga muongo mwingine bila kuwa wenyeji wa michuano hiyo angalau mara moja ,endapo tu serikali itashindwa kuwekeza zaidi katika michezo kwa muda mfupi ,na kujiingizia mapato kwa muda mrefu zaidi.

Ni nzuri zaidi pia kama serikali itajikita katika kukuza vipaji nchini ili kuzalisha watanzania watakao itumikia na kuitangaza nchi yetu kimataifa ,sambamba na kuanza kupitisha sheria ya kutumia au kusajili wachezaji wachache zaidi wa kigeni katika vilabu mbalimbali nchini na kutumia zaidi wazawa ,ambao mbali na kukipigania kilabu fulani ,pia watakuwa na uelewa kuwa wanaipigania nchi yao kwa ujumla.

Ni wazi kuwa wengi wa vijana nchini wenye vipaji na ndoto za kufika mbali kimataifa ,wanaishia kustaafu na ndoto zao kuzima hapahapa nyumbani ,kwa sababu tofautitofauti zikiwemo ,kukosa ~sapoti kutoka serikalini na uhaba wa uwekezaji katika sekta ya michezo ,jambo ambalo kwa namna moja au nyingine lingepelekea sekta ya utalii kukua kwa kasi na kuongeza pato la taifa.

Mwisho ningeiomba serikali ijaribu kujikita zaidi katika masuala ambayo hayamgandamizi mwananchi wa chini ,ndio maana nimechangia kimichezo zaidi kwa kuwa wengi wanapenda kutoa bila kulazimishwa au kuhisi ugandamizo fulani bali ni kwa mapenzi yao tu na michezo.

Asante.
Screenshot_20220724-202137~2.png
 
Upvote 0
Back
Top Bottom