Uchumi wa Buluu kwa Tanzania tuna Maanisha ni uchumi utokanao na Anga utalii ,na vyanzo vya maji (Bahari, Mito, maziwa, chemchem).
Mada yangu itajikita kwenye vyanzo vya maji na hasa uchumi wa uvuvi utokanao na Bahari na kwenye maziwa makuu ,hapa nchini.
Sisi wa Tanzania kupitia serikali inatupasa tupeane uwezo wa Sisi Kwa sisi kuendesha uchumi wa Buluu na kuumiliki ili kuweza kuleta utajiri wa moja Kwa moja Kwa ngazi ya familia au kaya .
Kwa kuwezeshwa wananchi kumiliki shughuli za uvuvi moja Kwa moja, itaongeza mnyororo wa fedha Kwa wananchi na kukuza kipato Chao.
Yafuatayo ni miongozo ambayo haina buni kuitekeleza Kwa vitendo.
1. Serikali
A). Kuboresha Sera na Sheria pindi inapohitajika.
Serikali inahitaji kuboresha na kutekeleza sera madhubuti mara Tu inapohitajika kufanya hivyo Kwa Sababu kuna mabadiliko makubwa ya kiteknologia , mabadiliko ya Hali ya hewa, zinazohusiana na uchumi wa buluu. Kwa hivyo serikali haipaswi kukaa Muda mrefu bila kufanya marekebisho ya Sheria na Sera Zake.
Uchumi Wa Buluu : Serikali Iwawezeshe Wananchi Kumiliki Shughuli Za Uvuvi.
B). Serikali kuanzisha programu za biashara uvuvi.
Serikali ikishirikiana na wadau wa maendeleo isadie kutoa mafunzo Kwa wavuvi wa kitanzania . (Start up accelerator for bluu economy )
Mafunzo hayo yatausiana na kufundisha Sheria za uvuvi, matumizi ya teknologia ya kisasa ya uvuvi na elimu ya uchumi wa Buluu Kwa ujumla wake.
C). Serikali iwape mikopo ya vifaa vya kisasa kwa wavuvi.
Serikali iwape mikopo ya vifaa vyenye teknologia ya uvuvi wa kisasa kwa wavuvi wa kitanzania. Hii mbinu itawawezesha wavuvi kuwa na uzoefu wa kutumia vifaa vya kisasa , ambapo vita Waongezea kipato chao.
D). Serikali iwape ruzuku wavuvi.
Serikali kupitia wabia mbalimbali wa maendeleo, itakuwa ni Baraka kama ikiamua kuwapa ruzuku wavuvi, baada ya kapewa mafunzo ya kisasa ya husuyo uvuvi, ubaharia, na matumizi ya teknologia ya kisasa.
Wavuvi wakipewa ruzuku itasadia Sana kuinuka kiuchumi, Kwa Sababu Mali samaki ipo ya kutosha, Nchi ina Amani na utulivu wa kisiasa na kiuchumi, Hali ya hewa imetuliia, kujumlisha na mafunzo ya kisasa ya uvuvi waliyo pewa, ni dhahiri ruzuku watakayo pewa itawanufaisha pakubwa Sana kufanya mageuzi chanya kwenye Shughuli za uvuvi.
2. Wavuvi.
A). Ubunifu na Teknolojia
Vijana wetu wasomi na wabunifu wa teknologia wanapaswa kuwezeshwa ili kuleta ubunifu na teknolojia mpya katika sekta za uchumi wa buluu. Teknolojia mpya zinaweza kuongeza ufanisi na tija katika uvuvi, usafiri wa baharini, na uchimbaji wa madini baharini.
Teknologia za vijana wetu wasomi zitakuwa ni nafuu Kwa wavuvi wa kitanzania kuzinunuua. Pia kuongeze ujira Kwa wabunifu wetu na Pia zitakuwa salama Kwa Sababu zitakuwa zimedhibitishwa na mamlaka husika za kitanzania na kimataifa.
3. Masoko , Mitaji na Biashara.
A). Kuunda Vyama vya Ushirika na kuanzisha kampuni za uvuvi
Wavuvi Wana paswa kuunda vyama vya ushirika, wakiwa kwenye vyama vya ushirika ,wanaweza kupata nguvu ya kujadiliana bei bora za samaki na kupata mikopo nafuu kwa ajili ya kuendeleza shughuli zao. Ushirika pia unaweza kusaidia katika kupata mafunzo na rasilimali muhimu.
Vyama vya ushirika na kampuni za uvuvi zisajiliwe kwenye Soko la hisa (DSE).
Ita pendeza kama vyama vya ushirika na kampuni za Wavuvi zikasajiliwa Soko la hisa la (DSE). Kusajili Vyama vya Ushirika na kampuni za uvuvi kwenye soko la hisa zitapatikana faida nyingi , kama ifutaatavyo :
i). Urahisi wa upatikanaji wa mitaji: makampuni na Vyama vya ushirika wakisajiliwa kwenye soko la hisa, kutatoa fursa ya kupata mitaji kutoka kwa wawekezaji wengi, kutoka nje ya nchi kuja kuwekeza kwenye uvuvi nchini.
ii). Uaminifu na Uwazi: Kusajiliwa Kwa biashara kwenye soko la hisa kunaonyesha uwazi na uwajibikaji, ambapo inaweza kuongeza uaminifu wa washirika na wadau wengine. Kuja kufanya biashara ya uvuvi nchini Tanzania .
iii). Thamani ya Soko kupanda: Vyama vya ushirika vinaweza kuongeza thamani yao kupitia kuongeza ushiriki wa wanahisa na soko la hisa linaweza kusaidia kuonyesha thamani halisi ya ushirika, kampuni za Wavuvi.
iv). Ukuaji wa Haraka kwa mitaji: Kupitia mtaji wa soko la hisa, ushirika na kampuni vinaweza kukua kwa kasi zaidi, kuanzisha miradi mipya, na kufanikisha mipango mikubwa ya uwekezaji nchini.
4). Utunzaji wa mazingira na maliasili za Bahari,maziwa, Mito, chemchem.
Ieleweke kuwa viumbe na maliasili vya kwenye Bahari maziwa, Mito, chemchem tumevikuta vikiwa salama,na ndio maana Sisi binadamu tunavitumia, ivyo inatupasa tuvitunze ili viendelee kutumika kizazi na kizazi.
A) . Kuzuia Uvuvi wa kupindukia.
Tanzania inatakiwa isizikubalie makampuni ya Asia ya mbali kuja kuvuna samaki Bahari ya hindi.
Wao tayari yameshamaliza samaki huko kwenye Bahari za nchi zao na kufanya uharibifu mkubwa wa viumbe na maliasili ya Bahari, Sasa wameamua kuja kwenye Bahari zetu za Africa ikiwa pamoja na Tanzania.
Hizi kampuni za uvuvi kutoka Asia ya mbali (china, South Korea, Japan)Hata wavune samaki kiasi gani, haziwezi kukidhi mahitaji ya Soko lao.
Suluhisho
i) serikali ni lazima izisimamie rasilimali zake mwenyewe ,
hapa namaanisha Kampuni za Wavuvi nchini Tanzania ndizo zinazo paswa , kuvua , kuchakata na kuuza samaki.
Kwani Tanzania tunaharaka gani , mpaka tuwaachie waje na Meli zao zivue samaki, Huku wananchi wetu wakivua samaki kwa kutumia majahazi na mitumbwi, wasituharakishe bhana, kwao tayari samaki wameisha jumlisha na sumu za viwandani zinazoingia kwenye Bahari zao Zina hatarisha afya za samaki na walaji.
Kwa hiyo Bahari za Africa na ikiwemo ya Tanzania wanazimezea mate. Serikali lazima hilo walitambue, wajibu Wao wa kulinda maliasili za Bahari.
ii). Serikali ilinde mipaka yake ya Bahari kikamilifu.
Serikali ya Tanzania inawajibu wa kulinda mipaka yake ya Bahari kikamilifu ikishirikiana na taasisi za kimataifa zinazo simamia usalama wa Bahari.
Mfano wa taasisi hizo ni UNEP ,oceana. Ikishirikiana na nchi zinazo tumia ushoroba wa Bahari ya hindi.
B). Kuzuia Utalii wa kupindukia.
Utalii una faida kwenye uchumi , Lakin kama Shughuli za utalii zitasababisha athari za maliasili ya Bahari, kiasi cha kuingia gharama,za kuyatunza Tena hayo mazingira, kuna kuwa hakuna maana ya utalii Tena.
Hitimisho.
Wavuvi wa kitanzania wawezeshwe ili kuongeze mnyororo wa fedha kwenye jamii!!.

Upvote
3