Tukuza hospitality
JF-Expert Member
- Jul 30, 2022
- 321
- 691
Gesi Asilia ni nini?
Kwa mujibu wa tovuti ya “renovablesverdes”, Gesi asilia ni mafuta ambayo, kama makaa ya mawe au mafuta ya petroli, huundwa na hidrokaboni, mchanganyiko wa molekuli zinazoundwa na atomi za kaboni na hidrojeni. Utafiti wa kisasa wa kijiolojia umewezesha kugundua na kutumia amana za gesi zilizozalishwa chini ya ardhi kwa mamia ya maelfu ya miaka na shughuli za bakteria. Kwa kifupi, ni nishati rafiki kwa mazingira kuliko nyingine kama makaa ya mawe na petrol.
Matumizi ya Gesi Asilia
Kwa mujibu wa chapisho la Taasisi ya Mafuta ya Marekani [“American Petroleum Institute – API”], (2021), mwanzoni mwa karne ya 19 na 20, gesi asilia ilitumika zaidi kuwasha taa katika majengo na mitaani; leo, teknologia ya kisasa inaruhusu kupanua matumizi, hadi kuzalisha umeme, kuendesha mitambo na vyombo ya usafiri, na kuzalisha bidhaa mbalimbali kama plastiki, mbolea, vipodozi na madawa.
Historia Fupi ya Gesi Asilia Tanzania
Watu wengi tunadhani gesi asilia imegunduliwa nchini hivi karibuni, yaani miaka ya 2010 na kuendelea! Lakini, utafiti wa gesi asilia umefanyika tangu mwaka 1952, chini ya utawala wa Uingereza; hii ni kwa mujibu wa chapisho la Laxology (Mei 22, 2019).
Kwa mujibu wa tovuti ya Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati (“EWURA”), ugunduzi wa kwanza wa gesi asilia nchini ulifanyika mwaka 1974 katika Kisiwa cha SongoSongo kilichopo Mkoani Lindi na kufuatiwa na ugunduzi wa pili katika eneo la Mnazi Bay mkoani Mtwara mwaka 1982.
Mtambo wa kuzalisha Gesi Asilia. Chanzo: www.ucsusa.org
Hazina ya Gesi Asilia
Kwa mujibu wa tovuti ya “EWURA”, kufikia Machi 2016, Wizara ya Nishati ilithibitisha kuwa, hifadhi ya gesi asilia iliyogunduliwa Tanzania hadi sasa, inafikia futi za ujazo trilioni 57.25.
Kwa mujibu wa tovuti ya “Wardometers”, nchi ya India ina hazina ya Gesi Asilia ya futi za ujazo trilioni 43. Utaona, Gesi Asilia ya Tanzania inazidi ile ya India kwa futi za ujazo trilioni 14.25. Idadi ya watu Tanzania (inayokadiriwa kuwa milioni 60), inaingia karibu mara 25 kwa nchi ya India yenye watu takriban bilioni 1.5 sasa. Hivyo, tuna hazina kubwa sana ya Gesi itakayoweza kuleta mapinduzi makubwa ya kiuchumi nchini, endapo itatumika vizuri.
Kiwango cha Matumizi ya Gesi Asilia Tanzania
Kwa mujibu wa gazeti la Mwananchi (Agosti 03, 2022), idadi ya magari yaliyofungiwa mifumo ya gesi mpaka sasa (Agosti 2022), ni takriban 1000. Kiasi kikubwa cha gesi kwa sasa kinatumika na “Tanesco” kuzalishia umeme. Kwa upande mwingine, nchi ya India, ambayo Tanzania imeizidi hazina ya gesi kwa futi za ujazo trilioni 14.25, mbali na kuitumia kuzalishia umeme, kuendesha viwanda nk; ina magari takriban milioni tatu yanayotumia gesi asilia (kwa mujibu wa tovuti ya “Statista” (2022). Kwa ulinganifu huu, bado Tanzania tupo nyuma katika matumizi ya rasilimali hii adimu.
Gari iliyofungwa mfumo wa Gesi Asilia. Chanzo: www.songeadc.go.tz
Uwekezaji Mkubwa kwenye Gesi Asilia
Kwa mujibu wa Chapisho la DiraMakini (Juni, 2022), mnamo Juni 11, 2022, Rais wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ameshuhudia makubaliano ya awali ya uwekezaji wa dola za Kimarekani Bilioni 30 kati ya Serikali na kampuni kubwa tano za kimataifa ambazo ni Equinor, Shell, ExxonMobil, Medco Energy na Pavilion, Ikulu, jijini Dodoma. Kwa mujibu wa chapisho hili, uwekezaji huu ni nusu ya uchumi wa Tanzania kwa sasa ($64bn).
Rais Samia akishuhudia utiaji sahihi Mkataba wa awali wa Uchakati wa Gesi Asilia (Juni 11, 2022). Chanzo: www.diramakini.co.tz
Huu ni uwekezaji mkubwa kuwahi kutokea, ambapo kama mikataba ya utekelezaji ni mizuri, basi kila mwananchi atakula mema ya nchi.
Mapendekezo
Serikali iwezeshe kuongezeka kwa vituo vya kufunga mifumo ya gesi asilia kwenye vyombo vya usafiri (magari, pikipiki, bajaji nk.) maeneo mengi nchini, na kutoa ruzuku kuvutia wamiliki wengi kupata huduma hiyo. Kwa sasa, ni kituo kimoja pekee kinachotoa huduma hii, kilichopo Taasisi ya Teknologia ya Dar es Salaam (“Dar es Salaam Institute of Technology – DIT”), ambapo gari ya kawaida, inapata huduma hii kwa gharama ya shilingi 1,800,000.00.
Serikali itoe ruzuku kwa huduma hii, kwa vyombo vyote vya usafiri, isipokuwa vile vinavyomilikiwa na taasisi binafsi (kama Mashirika yasiyokuwa ya Kiserikali, makampuni makubwa ya kibiashara, nk), taasisi za serikali, mabasi ya kusafirisha abiria mikoani na malori ya mizigo. Huu utakuwa ni uwekezaji mkubwa wa serikali, ambao utailetea mapato makubwa kutokana na matumizi makubwa ya gesi asilia – ambayo kwa sasa hayapatikani.
Mfano: Gharama ya kufunga mfumo wa gesi katika gari la kawaida ni shilingi milioni 1.8; serikali ikitoa ruzuku ya shilingi 1,500,000.00, mwenye gari atalipia huduma hii shilingi 300,000.00. Kama serikali itaweka kodi ya shilingi 100 kwa kila kilo ya gesi, na kwa siku gari ikatumia kilo 10 za gesi, itakusanya jumla ya shilingi 1,000.00 kwa siku; na kama gari itafanya kazi kwa siku 300 kwa mwaka, itakusanya shilingi laki tatu. Kwa kipindi cha miaka 5, serikali itakuwa imekusanya jumla ya shilingi 1,500,000.00 kwa gari moja. Mbali na kurejesha kiasi cha ruzuku kilichotolewa, serikali itakuwa imepata mapato mengi kutoka kwa magari ambayo hayapo kwenye mpango wa ruzuku.
Kwa kushirikiana na wadau wengine, serikali isambaze kwa kasi huduma ya gesi asilia majumbani na viwandani, ili kupunguza kasi ya ukataji miti nchini, wakati huohuo ikiongeza mapato yake.
Serikali ihimize wanaogiza vyombo vya usafiri, kuagiza vile vilivyofungwa mifumo ya kutumia gesi asilia.
Serikali itafute wawekezaji makini wa kuwekeza katika uzalishaji na usambazaji wa gesi asilia na kuhakikisha kunakuwa na mikataba yenye tija (kunufaisha kila upande – “Win Win state”).
Hitimisho
Tuwekeze kwenye uchumi wa gesi asilia kumtoa kila mwananchi kwenye lindi la umaskini.
Marejeo
Api (2021), “Natural Gas Solution”
Diramakini (Juni, 2022), Rais Samia na Uchumi wa Gesi, tupo Njia Sahihi
EWURA (2022), Gesi Asilia
Lexology (Mei 22, 2019), “Oil & Gas in Tanzania”
Mwananchi (August 03 2022), Kilio chatawala uhaba vituo vya kujazia gesi za magari
Renovablesverdes (Julai 21, 2022), “What is the Natural Gas?”
Statista (2022), “Number of compressed natural gas vehicles across India as of December 2017, by state”
Tanzaniaweb (Aprili 14, 2022), Mikakati ya Tanzania kuongeza kasi matumizi ya magari ya gesi asilia”
“The Hindu BusinessLine (Februari 22, 2022), India’s natural gas consumption to grow at 8 per cent y-o-y in 2022”

Upvote
7