SoC02 Uchumi wa kimkakati wa kikanda na Elimu kwa wakazi wake

SoC02 Uchumi wa kimkakati wa kikanda na Elimu kwa wakazi wake

Stories of Change - 2022 Competition

BA KUDO

New Member
Joined
Jul 27, 2022
Posts
2
Reaction score
0
UCHUMI WA KIMKAKATI WA KIKANDA NA ELIMU KWA WAKAZI WAKE

Kwa nionavyo mimi, ili kukuza UCHUMI unahitajika mpango mkakati wa kuzipeleka fursa maeneo jumuishi.

Upande wa Mbuga za Wanyama; Ningependekeza viwanja vya ndege vya Kilimanjaro International Airport, Mwanza Airport na Musoma Airport Vitumike kupokea watalii ili kuongeza kipato kwa Wananchi wa Mikoa yenye vivutio hivyo pia kupandisha mapato ya mikoa husika.

Upande wa Kilimo cha Tumbaku Ningependekeza kiwanda cha kusindika Tumbaku kijengwe Tabora ili kuongeza ajira wa wakazi wa eneo husika vivyo hivyo kwa upande wa Kilimo cha Alizeti ningependekeza kiwanda cha Mafuta ya Alizeti kijengwe Singida na Dodoma.

Upande wa zao la Pamba kiwanda cha nyuzi pia nguo ningependekeza kijengwe Simiyu na kwa upande wa Matunda Ningependekeza kiwanda cha usindikizaji kijengwe Tanga na kwa zao la Zabibu kiwanda cha usindikaji ningependeza kijengwe Dodoma.

Upande wa Michikichi ningeamasisha kiwanda cha usindikaji na mafuta ya maweze kijengwe Kigoma na Kyela, pia ningeshauri Wananchi wapatiwe mbegu za kisasa ili wengi wapate fursa ya kulimama kisasa.

Upande wa Kilimo cha Mpunga ningependekeza uanzishwaji wa Mabwawa na visima virefu kwenye mabonde na maeneo ambayo zao hilo linalimwa kwa wingi nchini Tanzania ili Wananchi walime kwa uhakika wa kupata mavuno pasipo kutegeme mvua na ningependekeza maafisa kilimo wapelekwe huko na wakulima wapatiwe mbegu za kisasa.

Upande wa Korosho ningependekeza kiwanda kinachohusiana na zao hilo kijengwe Mtwara na kwa zao la ufuta kiwanda kijengwe Lindi.

Upande wa Bahari ningependekeza viwanda vya kuchakata Samaki vijenge kwenye mwambao wa Bahari yetu kuanzia Tanga hadi Mtwara kadri wataalamu watakavyopendekeza pia kwenye Visiwa vya Zanzibar na Mafia.

Upande wa Madini ningependekeza Wananchi ambao maeneo yao yapo yalipo Madini (yaani eneo la uchimbani) kwa majibu wa watafiti ningependekeza waisiishie tu kulipwa fidia bali wapewe sehemu ya umiliki wa asilimia 5+ na wale wengine ambao watakuwepo eneo la Mgodi kwa pamoja wajengewe nyumba eneo moja na huko wapelekewe huduma zote za kijamii na Mgodi uwajengee vyuo vya ufundi na uchangie ghalama za malipo kwa asilimia 50 na utoe ufadhili kwa wanafunzi wenye sifa za kujiunga na vyuo vya Elimu ya Kati pia Elimu ya Juu.

Pia ningeshauri bandari ya nchi kavu kwa upande wa Mbeya ijengwe Tunduma ili kuboresha huduma.

Kwa Upande wa Moshi, ningeshauri kuuutangaza mji huo kupitia mwezi wa 12 ili kushawishi wangeni wengi kwenda kutembelea huko ili wajionee utamaduni wa wenyeji wa eneo hilo wanaporudi mwezi wa 12 kwao kwa ajili ya kusherekea sikukuu za krismsi na mwaka mpya na hii ingeongeza kipato kwa wenyeji.

Mikutano mwingine ya KIKANDA ningeshauri ipelekwe Sumbawanga pia Tabora kwa lengo la kuitangaza nchi yetu kwa wangeni na kuchochea kipato pia Elimu kwa wakazi wa maeneo husika.

Kwa upande wa Mikoa ya Iringa, Songea, Songwe na Njombe ningepeleka wataalamu wa Kilimo ili kukuza na kuinua kilimo biashara kwenye mazao ya maparachichi, mahindi, viazi mviringo, Ufuta na Maharage.

Mikoa ya Manyara, Iringa, Singida na Tabora kwenye maeneo wanayolima vitunguu, ningeshauri yaboreshwe kwa kuchimba Mabwawa na visima virefu, kupeleka mbegu za kisasa na wataalamu ili kuwaongezea tija na uwezo wakulima wa zao hilo.

NB: YOTE HAYO NILIYOYAANDIKA HAPO JUU NINGESHAURI YAFANYIKE KWA LENGO LA KUONGEZA TIJA ILI KUINUA UCHUMI WA WANANCHI, KUWAPA ELIMU WANANCHI ILI WASIPOTEZE HAKI ZAO HASA KWENYE MAENEO YAO YANAYOCHUKULIWA NA WAWEKEZAJI PIA KWENYE KILIMO BIASHARA.

Ruksa kusahihisha kwa LENGO la kupanga vizuri na atakayefanya hivyo nitamgawia asilimia 30 za malipo.
 
Upvote 2
Back
Top Bottom