Uchumi wa nchi

Nguza junior

Member
Joined
May 12, 2013
Posts
28
Reaction score
2
Mbona serikali inatangaza kila mwaka kupanda kwa uchumi wa tz wakati ndo maisha ya wananchi yanavyozidi kuzorota....
 
wanamaanisha economic growth ,kuna tofauti kat ya economic growth na development,ka vp google.
 
So u mean uchumi unakua sana ila wananchi wanazidi kudidimia havihusiani.... Wht about per capita income ya nchi
 
Ukitaka kujua kama uchumi haukui, angalia deni la Taifa mafisadi walilikuta liko kiasi gani na sasa likoje! Kisha linganisha na walizoficha Uswis. Kadri deni la Taifa linavyo kuwa na account zao uswis zinavyo nona!
 
Yaaani hilo ndo tatizo kubwa hela inayokuwa allocated sekta tofauti kwaajili ya maendeleo unakuta zinaishia kwenye matumbo ya wachache tu sasa lini nchi itakua....
 
Kukuza uchumi,uhalisia najua lazima tuuze sana nje ili tupate pesa za kigeni. sio kuuza ndani na kutozana kodi
 
Uchumi kukua sio lazima impact ionekane kwenye maisha ya watu, inategemea sana the way unavoupanga uchumi wako. Ukuwaji unaweza ukawa pro-poor kwa maana ya kuwanufaisha masikini au usiwe. Kwa case ya Tanzania, kwa miaka kumi iliopita uchumi wetu umekuwa kwa kasi sana (relative to other countries and global growth) but poverty rate imebaki constant!!
>ukitaka kujua sababu angalia ni sekta zipi zinazochangia ukuaji wa uchumi wetu zaidi (eg. utalii, madini etc), zinamilikiwa na nani?, wazawa au wageni?, je, ndio zinazoongoza kuajiri watanzania wengi? (note: kilimo kinaajiri zaidi ya 80% ya watanzania lakini hiyo sekta inakuwa kwa kasi ndogo sana)
>Je, vipi kuhusu gap kati ya walionacho na wasionacho? Kama linazidi kuongezeka tegemea ukuaji unaopaa na umasikini usiopungua!!!!!!
 
Uchumi umepanda kwenye makaratasi sio kiuhalisia.

kukuwa kwa uchumi haima(economic growth)haimaanishi kuimarika kwa maisha ya wananchi(standard of living) kama ilivo kwa kuengezeka kwa kipato cha mtu mmoja mmoja (Income per Capital) haimainishi kwamba standard of living itaimarika, unaweza kujiuliza kwa nini? kabla sijatoa jawabu, kwanza tuangalie vp pato la taifa linatafutwa (Calculated of National Income)
kama utatumia Expenditure method,
NI= C + I + Nx (Export -Import) + G: C = Public Consumption; I= Investement portion hii ni muhimu sana, na ikitokezea kubadilika kidogo basi itaathiri kwa kiwango kikubwa pato la Taifa, na I imejumuisha "Inventory" " Residential Building" pamoja na " private Investement nyengine" katika hili la Investement, utagundua kuwa ndani yake inapatikana Residential Building, thamani yake ( Residential Building) ina jumlishwa katika kutafuta pato la taifa, tujuilize hapa, nani anepinga kwamba thamani ya soko za nyumba za Tanzania kuwa hazikuwi, kila uchao new private resident building zinajengwa zenye thamani kubwa, hivyo kupelekea ku unuwa pata la taifa ; G = Government spending

Mimi na kubaliana kuwa uchumi unakuwa actual lakini kwa nini maisha hayaimariki,? jibu la suala hili linatokana na tatizo la Ugawanyaji wa keki ya Taifa " Distribution of National Cake" ina maanisha hakuna usawa, kwa io kuwengezeka kwa uchumi kutawafaidisha pamoja na kuona kwamba uchumi unakuwa wale ambao watajuhusisha moja kwa moja na zile shughuli zilizopelekea kukuwa kwa uchumi, mfano kama uchumi umekuwa katika secta ya utalii basi wale walio partcipate more ndo watakao hisi na kuona kwamba secta hii, inakuwa ukilinganisha na wale wasio partcipate kwa kiwango kikubwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…