Maoni yangu kwa Serikali ijao:
1)Maendeleo ya viwanda nchini:
Tukirudi nyuma mwaka 1961 Tanzania ilikuwa nyuma sana kwenye suala zima la viwanda ukilinganishwa na nchi zingine za Afrika mashariki.Sekta ya viwanda ilikuwa ikichangia asilimia 3.5% kwenye pato la Taifa wakati ni asilimia 9% tu ya watu ilikuwa imeajiliwa kwenye sekta hii.Mwaka 1964 Serikali iliingia kwenye mkakati mkubwa kabisa wa kuendeleza viwanda vya ndani wakati nguvu kubwa ikielekezwa kwenye kilimo kama uti wa mgongo wa Taifa.
Mwaka 1967 tulipitisha Azimio la Arusha na moja ya maazimio yaliyopitiwa ilikuwa ni kuweka mikakati mipya ya mapinduzi ya viwanda na kuifanya Tanzania kuwa nchi ya Ujamaa na kujitegemea.Moja ya mikakati iliyowekwa ilikuwa kutoruhusu mkono wa nje kujihusisha na viwanda.Kweli maendeleo hayakuwa mazuri kama ilivyopangwa.Ukipitia Azimio la Arusha kuna neno kujitegemeaikiwa na maana kujitegemea kiuchumi zaidi.
Kuanzia miaka 1970 viwanda vilivyokuwepo viliathirika sana kutona na vita vya Uganda na Tanzania.Moja ya mambo makubwa ni kusambaratika kwa mfumo wa fedha wakati huo huo kukatokea tatizo la kuporomoroka kwa uchumi duniani (The global Economy cricis) bei ya mafuta duniani ilipanda kwa asilimia 25 mpaka 30 kutoka hapo uhcumi wetu umeyumba sana mpaka kufikia leo njia nyingi na mbadala zilichukuliwa ili kunusuru nchi yetu.
Mashiika mengi yalianzishwa na kila shirika lilifanya shughuli zake mahususi Moja ya mashirika yaliyoanzishwa ndani ya Azimio la Arusha ni Shirika la maendeleo la Taifa(NDC) mwaka 1965 ili kuwa mlinzi na kuendeleza maliasili za Taifa.
NDC ni shirika nyeti sana na hasa kwenye kuibadilisha Tanzania kutoka mahali tulipo.Kwa kile kilichodaiwa kuwa Tanzania na watanzania hawana mitaji ya kuendeleza maliasili za Taifa leo hili shirika limefanikiwa kuingia kwenye mikataba mingi sana na makamuni ya nje hasa katika sekta ya madini na Nishati.Wakati huo huo Tanzania kupitia shirika nyeti kama hili linamiliki hisa asilimia chache kupitia hiyo miradi kwa kigezo kuwa hatuna miradi ya kutosha
Wakati huo huo watanzania hawaelewi nini kinaendelea ndani ya shirika hili,hakuna anayejua mikataba imefikia wapi na maendeleo ya miradi ni yapi,hakuna anayejua hatma ya maliasili yetu na jinsi shirika linavyoendeshwa.Hakuna anayejua Shirika lina lipa kodi na kama linalipa ni kiasi gain shirika limelipa,Hakuna anayejua mapato halisi ya shirika
Mpaka wakati huu watanzania wanafaidika kidogo sana kutokana na mali asili ya Taifa.
MAKOSA:
Shirika linaendesha shughuli zake kisiasa zaidi kuliko kimaendeleo hatujui ni vigezo vipi viongozi wa shirika walichaguliwa.
MAONI:
Serikali inayokuja lazima iliangalie sana hili suala.moja ya vitu vifuatavyo inaweza kupitia
1)Zipitiwe upya sheria zinazoliongoza hili shirika.Livunje mfumo wake mzima na ligawanyiswe sehemu tatu
1.1 Shirika liingizwe kwenye IPO (PUPLIC INITIAL OFFERING) na hisa zake ziuzwe DSE ili kila mtanzanie apate kuwa mwanahisa kwenye maliasili ya Taifa.Kwa miradi kama ya umeme na kuendeleza mikodi Watanzania wenyewe wanaweza.Serikali yetu imekuwa ikiamini kuwa hakuna watanzania wenye mitaji mikubwa,ni kweli hakuna ila hakuna makampuni makubwa ya nje yenye mitaji hiyo yote ya kuwekeza Tanzania.Wao na makampuni yao yanatafuta pesa kupitia kwenye masoko ya hisa ya Duniani.Kama wao wanafanya hivyo kwa nini NDC isifanye hivyo na kama ni shida basi tuliingize kwenye LSE,au NSE au Frankfurt stock exchange tatizo liko wapi?
1.2 Mkono wa pili wa shirika uwe zaidi una lenga katika kuwekeza nje.Wengi wanaweza kusema kwa nini tuwekeze nje wakati ndani pametushinda?Jibu ni moja.Ukiangalia zaidi nyuma katika historia hata wajermani na mataifa mengine yalipotutawala yalitutawala kupitia kwenye makampuni yao makubwa ya biashara mfano German East African Company au British East African Company.Kwa nini waliyatumia haya makampuni?Haya makampuni yalikuwa ya serikali zao na yalipewa nguvu kubwa za kiuchumi,kijeshi na kisiasa.Lengo lilikuwa ni kuhakikisha kukwapua mali tulizonazo ambazo wao hawana ili kujenga mataifa yao.Je walijenga miundo mbinu?Ndiyo mingi tu yote hayo ilikuwa ni kuhakikisha kazi zao zinafanywa kwa ufanisi.Nchi yetu leo tunanua bidhaa aghali sana mfano unga wa ngano,petrol,silaha si kutokana kwamba hatuwezi ila kuna mazao ambayo hayaendani na hali ya hewa yetu.Hii kampuni itakuwa na lengo moja la kuwekeza kwenye nchi zingine kwa ajili ya kujipatia malighafi kwa bei rahisi ambazo zitauzwa kwa wananchi wetu kwa bei zaidi.Kampuni hii inaweza kwenda mbali zaidi na kuwekeza kwenye visima vya mafuta mfano Nigeria.Lengo kuchukua mafuta ambayo tutayauza Tanzania kwa bei ya chini.Hili si geni katika ulimwengu wa leo.Hichi ndicho wanafanya wachina,wamerekani leo wachina wanatujengea barabara au wanatupa misaada mbona hakuna aliyehoji kwa nini watupe misaada wakati China kuna nusu ya wachina wanaishi kwenye umasikini wa kutupwa?Tumefumbwa macho.Leo hii China watoto wanaanza kufundishwa darasa la kwanza juu ya Africa ili kila mototo akuwe akijua Afrika ndiyo keki yao.Shirika pia litajiingiza zaidi katika kununua hisa kwenye makampuni ambayo tafiti itaonyesha kuna faida kubwa ,tusijibane sehemu moja tu.
1.3 Mkono mwingine wa shirika ujikite zaidi katika Private Equity(kama ingewezekana huu mkono ukabidhiwe kiasi cha dola milioni mia moja) .Lengo ni kujiingiza zaidi katika kuwainua wajasirimali wa Kitanzania ambao kampuni zao zinaonekana kukua na kutoa ajira zaidi kwa Taifa.ambapo shirika lingeweza kumiliki hisa asilimia hamsini kwa kila startup ya kitanzania.Mwisho wa siku zile kamppuni zote zingekua na kuleta mapinduzi makubwa zaidi nchini ambayo yasingeletwa na wawekezaji wanje kama tunavyofikiria
2 Shirika lijikite pia kwenye sekta zingine na hasa za kilimo.Mwaka 2007 tulipisha sera ya Kilimo Kwanza moja ya mambo muhimu ndani ya kilimo kwanza ilikuwa ni kuinua kiwango cha maisha cha mtu wa chini ambaye ni Mtanzania kufikia hatua ya kati.Mkakati mzima ulionyesha kuwa watu milioni tatu wangeweza kufaidika na sera hii ya mapinduzi ya kilimo.Jambo kama hili linaendelea kutatanisha sana kwa nini mapinduzi ya kilimo chetu yategemee fedha za wahisani.Fedha ambayo ilikubaliwa ilikuwa ni dola za kimarekani bilioni 3.3.Kama nguvu ingepewa mashirika kama haya ya Taifa ambapo watanzania wote wangeshiriki kuchangia kwenye mapinduzi ya kilimo nini kingeshindikana?Tukumbuke ya kwamba leo bajeti yetu kubwa ni kodi ambazo ni juimuisho ya makampuni mengi na ndipo ikafikia hapo ilipo.Kwa nini kwenye hili tushindwe mpaka leo?Mpaka lini tutaendelea kunyanyaswa na wahisani
3 Shirika lazima liendeshe shughuli zake kwa uwazi mkubwa ili kila Mtanzania awe na haki ya kupata taarifa wakati wowote si kama sasa 4 Uwekwe uongozi ambao unaendana na hali ya mabadiliko ya uchumi wa leo Duniani.Uongozi uliopo hauangalii mbele na hatma ya Taifa.Tuliangalie Taifa si kwa miaka mitano ya sasa.Tuliangalie Taifa kwa miaka miamoja mbele.Msingi wa miaka miamoja ya mbele unajengwa sasa.
5 Kwa kuwa tangu mwanzo shirika limepewa nafasi ya kulinda hazina kubwa ya Taifa na ndiyo maana likaitwa shirika la maendeo lazima liendane na jina lake.Lijiingize katika kuhakikisha tija na nafasi ya Taifa letu inakuwa mstari wambele na vipaumbele vyote lazima vitoke hapo.Mfano mdogo kuptia partnership ya sino na Tanzania Construction of $31.8b Tanzania China Logistics Centre to start soon - Construction Review Online Ukiiangalia kwa nje mradi kama huu ni mzuri sana kwa sabababu kwa nje ni kama kikombe kilichopakwa dhahabu wakati ndani hakuna kitu.Ni kweli kwa haraka haraka mradi unaotengeneza ajira 125000 si mdogo ila viongozi wetu walipaswa kupata ushauri badala ya kukurupuka.Mradi huu kwanza unalenga zaidi kuifaidisha China.Kigiografia Maisha ya Rwanda,Burundi,Congo ,Zambia,Malawi zaidi yanategemea bandari za Tanzania.Wachina wamelenga zaidi wateja zaidi ya milioni 500 kwa ajili ya bidhaa zao ambazo tayari zimekwisha tengenezwa China.Leo hakuna ambaye hafahamu kuwa bidhaa za China zinatengenezwa kwa cheap labour na ndIYO maana ni bei rahisi sana.Kitendo cha leo kuruhusu hawa waweke logistic centre ni kuruhusu bidhaa zadidi ya milioni moja kwa mwezi kuingia.Kweli ni vizuri si kila mtu atavaa viatu vya bei rahisi.Lazima tujue maisha yetu hayategemei takataka za siku mbili.Ni kitu ambacho hakionekani ila tunakwenda kuua viwanda vyote vyote.Tunakwenda kutengeneza Taifa la wachuuzi,Taifa kilema.Bidhaa zetu hazitalinganishwa na na za wachina.Kwa nini nchi za Ulya wamekimbizwa kama mbwa na miradi yao.Kwa sababu wapo zaidi kulinda ,Maslahi ya Taifa.Kuna nchi kadhaa duniani ambao waliruhusu miradi kama hii ndani ya miaka 20 viwanda vyote vya ndani vilikufa
NINI KINGEPASWA KIFANYIKE? Viongozi wetu wangepaswa kunigotiate ili mradi huu uje kivingine zaidi.Badala ya kujengwa logistic centre ilipaswa kujengwa Industria Park.Nini faida zake kama leo sino wameweza kuvishauri viwanda vyote vilete ready made products basi hao hao wangewashawauri hao wenye viwanda wawekeze viwanda vyao hapa.Kama viwanda elfu thelathini vingeingia Tanzanzania ambavyo lengo lao ni Afrika mashariki na vingewekezwa kwenye industrial park naamini kila kiwanda kingeweza kuajiri Watanzania 80 wachina 30.Tungeweza kutengeneza ajira za moja kwa moja 2400000 na ajira zisizo rasmi kama milioni tatu.Tungeweza kuifanya Tanzania kuwa industria hub of Africa
Tanzania ingeweza kuingiza mapato makubwa sana kwenye kodi vile vile asilimia 11% watanzania maisha yao yangebadilika.Na vile vile Wachina wangeweza kufaidika zaidi kwenye mauzo Miradi kama hii inapelekea Taifa kupotezamuelekeo tunahitaji bidhaa nyingi sana je ni lazima mpaka kiberiti kiagizwe kutoka China? Mfano mdogo Nigeria badala ya kuagiza metrekta kutoka China leo wameitaka kampuni ya Kichina kuja kuweka assembly plant Nigeria.Faida zake watu 5000 wamepata ajira kuachana kodi ambayo Taifa linakusanya soma Chinese, Nigerian firms to invest $40m in tractor assembly plant - Vanguard News
Nawakilisha