Uchumi wa tanzania unaegemea kwenye mambo yapi makuu?

KYANYINIMARAIGA

Senior Member
Joined
Oct 21, 2016
Posts
192
Reaction score
126
Kila nchi ina vigezo vyake vya kiuchumi na ina mambo ambayo yanategemewa sana ,katika kuendeleza uchumi wake.Kwa mfano mambo yanayoufanya uchumi wa Marekani kukua ni wingi wa Maliasili kama, udongo unaovuliwa, maarufu kikapu cha mkate,hali ya hewa nzuri,(temperate climate) amana kubwa ya mafuta, mkaa wa mawe, na gesi asilia.

Pia na wingi wa watu wa wa asili tofouti.hali inayofanya soko la ndani kumeza aslimia 70 ya uzalishaji wa ndani. Wakati huo karibu asilimia 50 ya uchumi wa marekani unategemea mauzo ya huduma mbali mbali kama, huduma za kifedha,huduma za afya, huduma za mali miliki kama taarifa za kiufundi(intellectaul property-technical information)

Naomba kupewa shule kidogo,(ukizingatia hapa katikati pamekuwepo maelezo ya kitaalamu kuhusu takwimu za ukuaji wa uchumi ,nina imani yalikuwa ya kitalaamu muno hata vyombo vya habari havikuweza kutoa ufafanuzi mpana) ni wapi uchumi wa Tanzania unaegemea zaidi.

Au ni mambo yapi yanaufanya uchumi wa Tanzania kukua zaidi?
 
Nafikiri ni hizi faini na kodi zisizokuwa na tija ndio tegemeo letu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…