Uchumi wa Tanzania unapaa. Je, hali za wananchi zikoje?

Uchumi wa Tanzania unapaa. Je, hali za wananchi zikoje?

S.N.Jilala

JF-Expert Member
Joined
Jan 26, 2012
Posts
540
Reaction score
507
Uchumi wa Tanzania Unapaa.

Je, hali za Wananchi zikoje?

Sekta zipi zimesababisha uchumi kupaa?

Uchumi wa Tanzania umekuwa kwa asilimia 7.9 katika robo ya pili ya mwaka 2016, ukuaji huo umechangiwa na sekta za madini, uzalishaji na nishati. Takwimu hizi zimetolewa na Bodi ya Takwimu nchini. Katika robo ya kwanza uchumi ulikuwa kwa asilimia 5.5.

Tanzania ni nchi nzuri sana katika rasilimali asili, tuna milima, mabonde, ardhi yenye rutuba, madini ya kila aina kama Tanzanite, dhahabu, almasi, na mengine mengi tu. Tuna gesi asilia nyingi na za kutosha kabisa. Tuna mifugo wengi, na Tanzania ni nchi ya tatu kwa kuwa na mifugo wengi Afrika. Watanzania zaidi ya asimilia 70 bado wanategemea kilimo lakini bado umasikini unawaandama sana.

Kwa hiyo basi, viongozi wetu wanapotuambia uchumi wa Taifa letu unakuwa ni kweli kabisa wakiwa na maana ya kuongezeka kwa pato la Taifa. Pato la Taifa ni thamani ya shughuli zote za uchumi-biashara, uzalishaji, huduma, na nyinginezo- katika kipindi cha miezi kumi na miwili. Je, kwa vipimo hivi, thamani ya shughuli za uchumi kwenye nchi imekuwa?? Je, inaongezeka kwa kasi ya kuridhisha mwaka kuanzia mwaka jana? Haya maswala ni ya wachumi zaidi.

Changamoto kubwa ninayoiona Mimi katika ukuaji wa uchumi Tanzania kwamba ni shughuli-biashara, uzalishaji, huduma, na vinginevyo vipi vinakuwa na kusema pato la Taifa limekuwa?. Je ni sekta ya kilimo, uvuvi na ufugaji ambazo watanzania wengi wanazitegemea? Au ni kampuni za watu binafsi ambazo asilimia ndogo mno ya watanzania wanafaidika nazo?. Kama sekta za uvuvi, kilimo na ufugaji zitaongezeka ni lazima zitapunguza umasikini kwa hali ya juu kabisa.

Kama wabobezi wa mambo ya Uchumi wanatuambia uchumi wa Tanzania umekuwa kwa asilimia 7.9 na ukuaji huo umechangiwa na sekta za madini, uzalishaji na nishati. Je, sekta hizi zimeajili wazawa kwa kiwango gani? Na Je, wananchi wa Tanzania wanafaidikaje na sekta hizi? Na zinapunguza kwa kiasi gani hali duni walizonazo?.

Kama sekta za uvuvi, kilimo na ufugaji zitaongezeka ni lazima zitapunguza umasikini kwa hali ya juu kabisa maana Watazania wengi ndiko waliko. Tuwaachie wajuzi wa maswala ya Uchumi kujadili takwimu, lakini lazima tuhoji UHUSIANO WA TAKWIMU NA HALI ZA WATANZANIA KIMAISHA japo kiuchumi inawezekana isiwe sawa, lakini kuhoji ni jambo zuri kuliko kujifanya tunajua au kushangilia takwimu na kusema NDIYO UCHUMI UNAKUWA.

Simon Ngusa Jilala
1/10/2016
 
Back
Top Bottom