Hivi Russia anapochoma gas yake ni kwa kupenda au Hana pa kuuza? Ikifikia hatua ya kichoma gas hua soko limeyumba na kama limeyumba je nchi haijapoteza mapato? Na kama imepoteza mapato je uchumi utabaki salama? Mtoa mada nisaidie kwa hili
Sijui chochote kuhusu kuchoma gesi.
Lakini majibu yangu Yako hivi,kama anachoma kwa kukosa soko maana yake anapata hasara.
Lkn anakosa soko kwa sababu wamemuwekea vikwazo asiuze kitu kwao wala asinnunue kitu kwao.
Sasa afanyeje? Ndio hivyo Tena kama Haina soko basi (anachoma).
Kwa kifupi Urusi havipendi vikwazo hivi na amewaomba mara kadhaa maraisi wa west wamuondolee vikwazo kwa sababu vinamuumiza.
Lkn vita ni vita Mura.
Kwa kua na yeye ameshajua kuwa nao wanaihitaji saaaana gesi yake naye Sasa anaitumia kama silaha ya kuwaumiza wao.
Waliamua kumwaga ugali yeye kamwaga mboga.vita maana yake piga nikupinge..
Uchumi wa Urusi hauwezi kuwa kama ambavyo ungekua kabla ya kuwekewa vikwazo aliwapenda sana ulaya alijenga Hadi Nordsteam2 kwa ajilia ya kufanya biashara na Ulaya,so hawezi kua mjinga Tena kuacha kuwauzia bila sababu za msingi.
Lkn Sasa afanyeje?
Mwenyewe umeona Sasa wanateseka wao na kuaanza kutumia Kuni badala ya gesi.najua watatafuta vianzo vingine,na yeye atatafuta masoko mengine.
Ni kweli nchi imepoteza mapato na haiwezi kua nauchumi sawa,lkn Sasa ifanyeje?
Mtu anaechochea mgogoro huu ni USA Nia ni
I)kuizunguka Urusi kijeshi,
Ii)kuidhoofisha kiuchumi,
III)kutaka itengwe kimataifa.
Lakini matokeo yamekua kinyume sana.
Ukweli Urusi ilizibembeleza sana nchi za west kuhusu Ukraine isijiunge na NATO na iache mienendo yake inayotishia amani ya Urusi,lkn wote tulikua tunaona jinsi walivyokua wanaipuuza Urusi.
USA pia alikua na wivu juu ya biashara kati ya Ulaya na Urusi