kizazi kipya
JF-Expert Member
- Jul 21, 2010
- 327
- 62
Mara tu baada ya mlipuko wa bomu katika mkutano wa chadema arusha zilitoka kauli nyingi kutoka kwa wahusika.Sijui kama zilikuwa kweli au ulikuwa unafiki.Iliundwa tume ya kipolisi ikiongozwa na chagonja ambaye alianza na mikwara mingi sana arusha.Tabu ilianza baada ya mbowe kutangaza kwamba polisi inahusika.Nadhani kazi yote ya upelelezi iliishia hapo na kilichofuata ni kumwandama mbowe alete ushahidi.Chagonja aliibuka na mikwara mingi sana.
Baadae kidogo tukaambiwa FBI wapo arusha suala lililokanushwa na ubalozi wa marekani.Swali :kwa nini tulidanganywa kwamba FBI wapo arusha?kulikuwa na lengo gani?Baadae mkuu wa mkoa wa arusha aligeuka msemaji wa polisi kwa kutangaza kwamba uchunguzi unaonesha mipango ya ulipuaji bomu ilipangwa arusha.Na kwamba wachina wanachunguza bomu hilo kujua liliingiaje nchini.
Cha kushangaza toka hapo kumekuwa kimya.Polisi wanamfwatilia mbowe awape ushahidi wa wao kuhusika.Lakini hawatuambii uchunguzi wao umefikia wapi?na kama sio wao nani anahusika?Je ni kweli intelijensia ya polisi imeshindwa kubaini waliolipua bomu?
Mbona wauaji wa kamada barlow walipatikana.Kwa nini anaandamwa mbowe na hatupati maendeleo ya tume ya mgonja?Kwa nini hawataki kuunda tume ya kijaji kwa suala nyeti kama hili?kwa nini mwigulu haambiwi kupeleka ushahidi wa kuwa chadema ilihusika?Na je ni lini tutapata majibu ya tume ya chagonja?
Tutafakari....