Uchunguzi wa vinasaba (DNA) umebainisha wasichana Sharon Mathius na Melon Lutenyo ni pacha ambao mama yao halisi ni Rosemary Khaveleli Onyango

Uchunguzi wa vinasaba (DNA) umebainisha wasichana Sharon Mathius na Melon Lutenyo ni pacha ambao mama yao halisi ni Rosemary Khaveleli Onyango

Makanyaga

JF-Expert Member
Joined
Sep 28, 2007
Posts
11,129
Reaction score
7,321
pic+dna.jpg

Advertisement
Nairobi, Kenya. Uchunguzi wa vinasaba (DNA) umebainisha wasichana Sharon Mathius na Melon Lutenyo ni pacha ambao mama yao halisi ni Rosemary Khaveleli Onyango.

Kwa mujibu wa uchunguzi huo, mapacha hao na mama yao Rosemary wana chembechembe za kufanana kwa asilimia 99.999.

Mapacha hao ambao wamekuwa gumzo mitandaoni katika siku za karibuni katika nchi za Afrika Mashariki baada ya picha zao kuonekana hadharani wakionyesha kutoka katika familia mbili tofauti licha ya kufanana.

Lakini jana kitendawili cha wasichana hao wanaotoka kaunti ya Kakamega kiliteguliwa ambako imebainika kwamba msichana wa tatu, Melvis Mbaya, ambaye amekuwa nao mara kwa mara si ndugu yao halisi katika kuzaliwa.
Uamuzi huo ulifikiwa Aprili mwaka huu baada ya familia hizo kuomba msaada wa vipimo vya DNA ambako taasisi ya Lancet Kenya ikajitolea kufanya kazi hiyo kwa gharama nafuu.

Kwa mujibu wa matokeo hayo, sehemu 12 kati ya sehemu 23 zinazotumika katika tathmini hiyo ya Melvis Mbaya zilikosa kufanana.

“Sehemu tatu tu zikikosa kuonyesha mfanano katika uchunguzi wa aina hii, inafafanuliwa kwamba matokeo ni hasi,” ilisema sehemu ya matokeo hayo ya uchunguzi wa DNA.

Hata hivyo, matokeo hayo yalionyesha Melvis Mbaya ana chembechembe sawa kabisa na za Angeline Omina na Wilson Lutah Maruti ikimaanisha kwamba huyo ni mtoto wa familia nyingine ya ndugu hao.

Wasichana hao ambao kwa sasa ni watahiniwa wa kidato cha nne, wamekuwa wakielezea kuwa tangu wakutane wamejenga urafiki wa karibu ambao ulionekana kuzidi hata undugu.

Chanzo: Mwananchi
 
Yaani hii nimeifuatilia nikasema,God is alive. Wamekutana thanks to the facebook. Pia najiuliza au labda yule mama wa Nairobi alimbadili mwanae akachukua Sharoon,alihisi labda mwanae halisi asingeishi labda hali yake ilikuwa mbaya sana. Any way it is just complicated. Asante Mungu wamekutana after 19 yrs of separation.
 
Kwa aliyefuatilia Story za Pacha hawa wa Kakamega Kenya atakubaliana nami
Ni tukio lililojaa msisimko mkubwa!
Pacha hawa waliozaliwa pamoja na Mama yao miaka 19 iliyopita na mmoja wao kutenganishwa na mzazi wakiwa Labour,mama mzazi akikabidhiwa watoto pacha wawili bila kufahamu kuwa mmoja Kati ya watoto hao si wake!
Tokea August 1999 mpaka 2018 ndio hawa watoto Ambao sasa ni mabinti wa kidato cha nne ndio wanakuja kukutana kwa msaada wa marafiki na Facebook app na kila mmoja kumshangaa mwenza wake kwa ufanani uliopitiliza!
Ni Story very interesting kwa ambaye hajaifuatilia aende YouTube aifuatilie
Ni wiki iliyopita tu ndiyo kwa msaada wa taasisi moja hatimae matokeo ya DNA yamedhihirisha kuwa wasichana hawa mapacha ni ndugu wa Baba na Mama mmoja licha ya mmoja wao kuishi na familiya ingine kwa zaidi ya miaka 20!
Story hii ina mengi ya kujifunza na inatukumbusha upande mwingine kua mungu ni mkubwa!
Wasichana hawa wanafikiria huko baadae kuja kutoa Movie itakayoitwa The Lost Twins.
57485778_305012636841580_7375356684375425024_n.jpeg
 
Kwa aliyefuatilia Story za Pacha hawa wa Kakamega Kenya atakubaliana nami
Ni tukio lililojaa msisimko mkubwa!
Pacha hawa waliozaliwa pamoja na Mama yao miaka 19 iliyopita na mmoja wao kutenganishwa na mzazi wakiwa Labour,mama mzazi akikabidhiwa watoto pacha wawili bila kufahamu kuwa mmoja Kati ya watoto hao si wake!
Tokea August 1999 mpaka 2018 ndio hawa watoto Ambao sasa ni mabinti wa kidato cha nne ndio wanakuja kukutana kwa msaada wa marafiki na Facebook app na kila mmoja kumshangaa mwenza wake kwa ufanani uliopitiliza!
Ni Story very interesting kwa ambaye hajaifuatilia aende YouTube aifuatilie
Ni wiki iliyopita tu ndiyo kwa msaada wa taasisi moja hatimae matokeo ya DNA yamedhihirisha kuwa wasichana hawa mapacha ni ndugu wa Baba na Mama mmoja licha ya mmoja wao kuishi na familiya ingine kwa zaidi ya miaka 20!
Story hii ina mengi ya kujifunza na inatukumbusha upande mwingine kua mungu ni mkubwa!
Wasichana hawa wanafikiria huko baadae kuja kutoa Movie itakayoitwa The Lost Twins. View attachment 1130651
Watanzania kwa uwongo ,hata pasipo na sababu wataingiza tu ada yao ya uongo na uzushi au kutia chumvi !
Futa uongo wako lete facts za ukweli
 
Hiyo habari inadhihirisha wazi jinsi mapungufu ya hospital yanavyo kuwa --- Kuna watoto wengi sana hulelewa na wazazi ambao sio wao
 
Mkuu kwahiyo ile kauli ya mama zetu, dada zetu wake zetu, ilie kauli yao pendwa wanayosemaga "MTOTO NI WA MAMA" imeexpire?

Kuna kitu nimegundua hapa, ukimshtukia mtoto mkaenda kupima DNA lazima mpimwe wote watatu, namaanisha wewe Baba, Mama na Mtoto.
Kwani unaweza ukapima wewe Baba na Mtoto tu ukakakuta siyo mwanao kumbe hata mama yake siyo mwanae, ila ukipima baba na mtoto ukakuta ni mwanao basi hata mama ni mwanae kweli.

Ile kauli yao pendwa ya mtoto ni mama ilikua ya watu wa zamani waliokua wanazalia majumbani tu, sasa hivi hiyo kauli imepitwa na wakati.
 
Back
Top Bottom