Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,872
- 34,363
Matumizi ya kila siku ya dawa za kupunguza maumivu kwa jina Paracetamol huongeza hatari ya ugonjwa wa moyo ,kiharusi na kusababisha mtu kuaga dunia mapema ,utafiti umeonya.
Utafiti huo umebaini kwamba wagonjwa wanaopewa dawa hizo za kupunguza maumivu
mwilini kwa mda mrefu wana hatari kubwa ya asilimia 63 kuaga dunia haraka.
Hatari ya kupatikana na ugonjwa wa moyo iko juu kwa asilimia 68 huku pia kukiwa na
hatari kubwa ya asilimia 50 ya kupatikana na vidonda vya tumbo ama hata kuvuja damu.
Paracetamol kama zinavyojulikana hupendelewa sana na madaktari wengi wakidai ni
salama kushinda Aspirin, ambayo imehusishwa na kuvuja damu tumboni na Ibuprofen
ambayo imehusishwa na magonjwa ya moyo na kiharusi.
Lakini watafiti wa Uingereza waliofanya uchunguzi huo uliowahusisha wagonjwa 666,000
wanasema kuwa hatari hiyo huenda ilipuuzwa na sasa wameagiza uchunguzi ufanywe
kuhusu usalama wa dawa hiyo.
Wanasayansi hao wanatoka katika taasisi ya matibabu ya Rheumatic and Musculoskeletal
iliopo mjini Leeds.