Uchunguzi: Wakopeshaji wa mitandaoni hawajasajiliwa na BoT wala BRELA na uendeshaji wao umejaa vitendo vya udhalilishaji

Uchunguzi: Wakopeshaji wa mitandaoni hawajasajiliwa na BoT wala BRELA na uendeshaji wao umejaa vitendo vya udhalilishaji

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
1,869
Reaction score
4,877
Siku 36 baada ya mwandishi wa Nipashe kuwasilisha maswali Benki Kuu ya Tanzania (BoT), kutaka kujua kwanini wakopeshaji mitandaoni wanadhalilisha wakopaji, taasisi hiyo imetengeneza mwongozo kwa watoa huduma ndogo za fedha wa daraja la pili, wanaotoa huduma za mikopo kidijitali.

Agosti 19 mwaka huu, mwandishi wa habari hii aliwasilisha maswali BoT akitaka kujua, pamoja na mambo mengine, kama taasisi/kampuni zinazotoa mikopo mtandaoni zinatambuliwa na BoT na hatua inazochukua dhidi ya wakopeshaji wanaodhalilisha wakopaji.

Septemba 2, mwaka huu, BoT ilijibu maswali hayo, ikieleza kuwa haitambui taasisi hizo na kwamba imeshatoa tangazo kwa umma la katazo la kuendesha mikopo hiyo, mpaka watakapopata kibali cha BoT.

Soma pia:

Katika majibu yake kwa mwandishi, BoT ilieleza kuwa Sheria ya Watoa Huduma Ndogo za Fedha, inaruhusu kutoa mikopo kwa njia ya mtandao, lakini mpaka wapewe kibali cha taasisi hiyo, ingawa hadi wakati huo hakuna hata mkopeshaji mmoja wa mtandaoni aliyekuwa amesajiliwa.

BoT pia ilithibitisha kumekuwa na malalamiko ya matumizi mabaya ya taarifa za waombaji mikopo ya mtandaoni.

Septemba 24, mwaka huu, ikiwa ni siku 36 tangu mwandishi wa Nipashe awasilishe maswali BoT, Naibu Gavana Dk. Yamungu Kayandabila, alitoa taarifa kwa umma kuwa wamechapisha Mwongozo wa Watoa Huduma za Fedha wa Daraja la Pili, wanaotoa huduma za mikopo kwa njia ya kidijitali.

Alisema kuwa mwongozo huo wa mwaka 2024 una lengo la kuimarisha usimamizi wa uendeshaji huduma za mikopo kidijitali.

"Mwongozo huu unalenga kuhakikisha uzingatiwaji kanuni za kumlinda mlaji wa huduma za kifedha, ikijumuisha uwazi, uwekaji bei, njia za ukusanyaji madeni, utunzaji taarifa za wateja na faragha.

"Kufuatia mwongozo huu, BoT inawaelekeza watoa huduma ndogo za fedha wa daraja la pili wanaotoa au wanaokusudia kutoa mikopo ya kidijitali, kutii matakwa ya mwongozo huu.

Soma pia:
"Endapo mtoa huduma atakiuka agizo hili, BoT itachukua hatua za kiutawala, ikiwamo faini, kusitisha shughuli za utoaji mikopo ya kidijitali na kufutiwa leseni ya kuendelea na biashara ya huduma ndogo za fedha. BoT itachapisha orodha ya watoa huduma walioidhinishwa kutoa huduma kidijitali," alisema.

Uchunguzi uliofanywa na mwandishi wa Nipashe kwa miezi minne, umebaini utoaji mikopo mtandaoni kiholela.

Ni mikopo yenye riba kubwa inayofika hadi asilimia 80, masharti ya mikopo yanafichwa, udhalilishaji wakopaji kwa kuundiwa makundi katika mitandao ya kijamii kisha picha zao kusambazwa, matumizi ya namba za simu zenye utambulisho (code) usiotambulika.

Source: Nipashe
 
Yaani BOT nao wanauzembe mwingi sana pamoja na hayo yote hakuna hatua zaidi iliyochukuliwa kwa hizi taasisi uchwara za kitapeli. Wao BOT wametoa muongozo ili hizi taasisi zijiongoze? Ilipaswa zisitishwe kwanza wakati zoezi la usajili linaendelea. Halafu imekuaje hawa matapeli wanapeleka taarifa kwenye credit reference bureau na zinafanyiwa kazi wakati hata kumbe hawajasajiliwa? Huu ni uzembe mkubwa mno
 
Back
Top Bottom