UCL: Deportivo la Coruna, timu iliyowahi kufanya maajabu

jelenga

Member
Joined
Apr 18, 2013
Posts
66
Reaction score
37
Heshima nyingi sana kwenu wadau na wanazi wa soka hususani ulaya.
Tukiwa tunasubiri kuangalia mtanange wa UEFA Leo,naomba niwakumbushe timu hii iliyopotea katika michuano hii na katika La liga pia, lakini iliwahi kutisha na kutikisa kigogo wa soka la ulaya wakati huo

Katika msimu wa 2003/2004 wa Uefa champions league hatua ya robo fainali, deportivo ilipigwa goli 4-1 katika mechi ya kwanza na timu iliyokuwa Moto wakati huo, Ac Milan ya Anceloti pale katika dimba la San Siro Italia. Katika mechi ya marudiano dimba la Riazor, Spain, Anceloti na Jeshi lake waliamini kwamba wana kazi ndogo sana ya kumalizia, kwani kwa hakika hakuna timu hata moja ambayo iliwahi kupindua matokeo ya aina ile katika michuano ya Uefa. Ilichukua dakika 5 tu baada ya kipenga, Walter Pandiani akampga chenga ya kumgeuza mtu mzima, Paolo Maldini, na kumimina mkwaju mkali ambao golikipa Dida hakuuona. Deportivo walizidi kupapasa soka balaa, ambapo kwa kifupi tu, hadi mapumziko walikuwa wakiongoza 3 bila, kipindi cha pili wakapga la 4, na kuitoa Milan kwa 5-4. Hadi mechi inaisha Anceloti hakuamini kilichokuwa kikitokea mbele ya macho yake, akaamini huenda anaota. Pamoja na kuwa na washambuaji walafi wa magoli kama Filipo Inzagi na Rui Costa, akajikuta akitupwa nje ya michuano hii.

Vikosi vilikuwa hivi.
Deportivo la Coruna.
Jose Francisco Molina (GK), Manuel Pablo, Enrique Romero, Nourredine Naybet, Mauro Silva (C),Walter Pandiani,Sergio Gonzalez, Jorge Andrade, Sanchez Victor, Albert Luque na Juan Carlos Valeron.

Ac Milan.
Dida (GK),Cafu, Paolo Maldini (C),Andry Chevchenko,Genaro Gattuso, Alessandro Nesta, Joh Dahl Tomasson, Clarence Seedorf, Andrea Pirlo, Ricardo Kaka na Giussepe Pancaro.
 
sasa mdau hapo unataka kutueleza nini sisi wanazi wa man utd? je tutarajie miujiza kama hiyo?

btw nadhani hapa afrika simba ndo iliweka rekodi ya pekee dhidi ya mufulira wonderous
 
Heshima nyingi sana kwenu wadau na wanazi wa soka hususani ulaya.
Tukiwa tunasubiri kuangalia mtanange wa UEFA Leo,naomba niwakumbushe timu hii iliyopotea katika michuano hii na katika La liga pia, lakini iliwahi kutisha na kutikisa kigogo wa soka la ulaya wakati huo

Katika msimu wa 2003/2004 wa Uefa champions league hatua ya robo fainali, deportivo ilipigwa goli 4-1 katika mechi ya kwanza na timu iliyokuwa Moto wakati huo, Ac Milan ya Anceloti pale katika dimba la San Siro Italia. Katika mechi ya marudiano dimba la Riazor, Spain, Anceloti na Jeshi lake waliamini kwamba wana kazi ndogo sana ya kumalizia, kwani kwa hakika hakuna timu hata moja ambayo iliwahi kupindua matokeo ya aina ile katika michuano ya Uefa. Ilichukua dakika 5 tu baada ya kipenga, Walter Pandiani akampga chenga ya kumgeuza mtu mzima, Paolo Maldini, na kumimina mkwaju mkali ambao golikipa Dida hakuuona. Deportivo walizidi kupapasa soka balaa, ambapo kwa kifupi tu, hadi mapumziko walikuwa wakiongoza 3 bila, kipindi cha pili wakapga la 4, na kuitoa Milan kwa 5-4. Hadi mechi inaisha Anceloti hakuamini kilichokuwa kikitokea mbele ya macho yake, akaamini huenda anaota. Pamoja na kuwa na washambuaji walafi wa magoli kama Filipo Inzagi na Rui Costa, akajikuta akitupwa nje ya michuano hii.

Vikosi vilikuwa hivi.
Deportivo la Coruna.
Jose Francisco Molina (GK), Manuel Pablo, Enrique Romero, Nourredine Naybet, Mauro Silva (C),Walter Pandiani,Sergio Gonzalez, Jorge Andrade, Sanchez Victor, Albert Luque na Juan Carlos Valeron.

Ac Milan.
Dida (GK),Cafu, Paolo Maldini (C),Andry Chevchenko,Genaro Gattuso, Alessandro Nesta, Joh Dahl Tomasson, Clarence Seedorf, Andrea Pirlo, Ricardo Kaka na Giussepe Pancaro.

punguani wewe...
Hakuna mchezaji aliewahi kumpiga chenga paolo maldini. Hata de lima mwenyewe alimshinda kwa mbio tu ila hakumpiga chenga.

Pia milan hawakuwahi kuwa na mshambuliaji mwenye uchu alieitwa rui costa.

Kwa kifupi
umekurupuka bila kuchamba
 
Duh haya majanga
 
Siku zote kuharisha kwa kutumia mdomo hudhoofisha utu wa mtu. Huna haja ya kunishambulia mimi, shambulia hoja mkuu. Kukuonesha kwamba sijakurupuka, tembelea UEFA.COM, tafuta mechi ya robo fainali Kati ya timu hzo msimu huska. Then, usijione we ni bingwa wa matusi kwa wenzio, kama huna cha kuchangia unakaa kimya
 
Mkuu shifta Said, nahisi punguani ni mama yako aliyekuzaa, kwa vile hajakulea katika mazingira ya utu kwa watu.
 
Heshima nyingi sana kwenu wadau na wanazi wa soka hususani ulaya.
Tukiwa tunasubiri kuangalia mtanange wa UEFA Leo,naomba niwakumbushe timu hii iliyopotea katika michuano hii na katika La liga pia, lakini iliwahi kutisha na kutikisa kigogo wa soka la ulaya wakati huo

Katika msimu wa 2003/2004 wa Uefa champions league hatua ya robo fainali, deportivo ilipigwa goli 4-1 katika mechi ya kwanza na timu iliyokuwa Moto wakati huo, Ac Milan ya Anceloti pale katika dimba la San Siro Italia. Katika mechi ya marudiano dimba la Riazor, Spain, Anceloti na Jeshi lake waliamini kwamba wana kazi ndogo sana ya kumalizia, kwani kwa hakika hakuna timu hata moja ambayo iliwahi kupindua matokeo ya aina ile katika michuano ya Uefa. Ilichukua dakika 5 tu baada ya kipenga, Walter Pandiani akampga chenga ya kumgeuza mtu mzima, Paolo Maldini, na kumimina mkwaju mkali ambao golikipa Dida hakuuona. Deportivo walizidi kupapasa soka balaa, ambapo kwa kifupi tu, hadi mapumziko walikuwa wakiongoza 3 bila, kipindi cha pili wakapga la 4, na kuitoa Milan kwa 5-4. Hadi mechi inaisha Anceloti hakuamini kilichokuwa kikitokea mbele ya macho yake, akaamini huenda anaota. Pamoja na kuwa na washambuaji walafi wa magoli kama Filipo Inzagi na Rui Costa, akajikuta akitupwa nje ya michuano hii.

Vikosi vilikuwa hivi.
Deportivo la Coruna.
Jose Francisco Molina (GK), Manuel Pablo, Enrique Romero, Nourredine Naybet, Mauro Silva (C),Walter Pandiani,Sergio Gonzalez, Jorge Andrade, Sanchez Victor, Albert Luque na Juan Carlos Valeron.

Ac Milan.
Dida (GK),Cafu, Paolo Maldini (C),Andry Chevchenko,Genaro Gattuso, Alessandro Nesta, Joh Dahl Tomasson, Clarence Seedorf, Andrea Pirlo, Ricardo Kaka na Giussepe Pancaro.
Kaka nakuita kaka nikiamini ni mwanaume, umenikumbusha mbali sana, nakumbuka mechi ya Nusu fainali walitolewa na Porto ya Morinho nakumbuka mashabiki wa Deportivo walilia sana, refa Collina aliwapa Porto penati ya kimagumashi sana.
 
punguani wewe...
Hakuna mchezaji aliewahi kumpiga chenga paolo maldini. Hata de lima mwenyewe alimshinda kwa mbio tu ila hakumpiga chenga.

Pia milan hawakuwahi kuwa na mshambuliaji mwenye uchu alieitwa rui costa.

Kwa kifupi
umekurupuka bila kuchamba

Kama hujui mpira si ukae kimya. JELENGA kaongea ukweli sana wewe huna hata data unabisha tu. Hamnazo wewe!
 
RICARDO KAKA, nakushukuru sana kaka, kuna watu humu jf wapo kwa ajili ya kutukana watu na siyo kuchangia hoja. Kaka hii michuano ya UEFA ya mwishoni mwa tisini kuja mwaka 2000 hadi katikati ya 2000 Kuna timu zilikuwa zinafanya maajabu sana, ikumbuke Man U ilivyotwaa taji mbele ya Bayern.
 
Mkuu umenikumbusha Mmorocco Naybet bonge la beki,Pandiani baadae alihamia EPL hakutamba sana...
 
Dipotivo lilikua chama langu,pia iliwai fanya hivyo kwa TIMU ufaransa,umenikumbusha Diego Tristan,Roy Makaay(mholanzi),alafu kulikua kiungo anaitwa Ruben Baraja,sina Uhakika kama alikua Dipotivo
 
Baraja alikuwa Valencia..kama sijakosea.
 
Heshima nyingi sana kwenu wadau na wanazi wa soka hususani ulaya.
Tukiwa tunasubiri kuangalia mtanange wa UEFA Leo,naomba niwakumbushe timu hii iliyopotea katika michuano hii na katika La liga pia, lakini iliwahi kutisha na kutikisa kigogo wa soka la ulaya wakati huo

Katika msimu wa 2003/2004 wa Uefa champions league hatua ya robo fainali, deportivo ilipigwa goli 4-1 katika mechi ya kwanza na timu iliyokuwa Moto wakati huo, Ac Milan ya Anceloti pale katika dimba la San Siro Italia. Katika mechi ya marudiano dimba la Riazor, Spain, Anceloti na Jeshi lake waliamini kwamba wana kazi ndogo sana ya kumalizia, kwani kwa hakika hakuna timu hata moja ambayo iliwahi kupindua matokeo ya aina ile katika michuano ya Uefa. Ilichukua dakika 5 tu baada ya kipenga, Walter Pandiani akampga chenga ya kumgeuza mtu mzima, Paolo Maldini, na kumimina mkwaju mkali ambao golikipa Dida hakuuona. Deportivo walizidi kupapasa soka balaa, ambapo kwa kifupi tu, hadi mapumziko walikuwa wakiongoza 3 bila, kipindi cha pili wakapga la 4, na kuitoa Milan kwa 5-4. Hadi mechi inaisha Anceloti hakuamini kilichokuwa kikitokea mbele ya macho yake, akaamini huenda anaota. Pamoja na kuwa na washambuaji walafi wa magoli kama Filipo Inzagi na Rui Costa, akajikuta akitupwa nje ya michuano hii.

Vikosi vilikuwa hivi.
Deportivo la Coruna.
Jose Francisco Molina (GK), Manuel Pablo, Enrique Romero, Nourredine Naybet, Mauro Silva (C),Walter Pandiani,Sergio Gonzalez, Jorge Andrade, Sanchez Victor, Albert Luque na Juan Carlos Valeron.

Ac Milan.
Dida (GK),Cafu, Paolo Maldini (C),Andry Chevchenko,Genaro Gattuso, Alessandro Nesta, Joh Dahl Tomasson, Clarence Seedorf, Andrea Pirlo, Ricardo Kaka na Giussepe Pancaro.

binafsi mi naona liver ndo walifanya maajabu kutoka tatu bila kipindi cha kwanza hadi kuchukua kombe, ila nurdin neybet alikuwa fundi jamaa ni mmoroco yule
 
Those days...it was very nice. Nimewakumbukapia Leeds United ya kocha David O'Leary na captain wao Lucas Radebe(South Africa)... kiungo Olivier Darcout, washambuliaji Allan Smith na kitasa Rio Ferdinand...to mention afew!
 
Hiyo wiki itakumbukwa sana kwani maajabu mengi yalitokea kwani monaco ya france nayo ilipita baada ya kufungwa game ya kwanza nadhani na chelsea ya ranieri.

kwenye hiyo game ya spain ambayo ac milan walishinda 4-1 kaka(mbrazili) ndiyo kwanza alikuwa na miaka 22 nafikiri alipiga hattrick kwenye hiyo mechi
 
Umenikumbusha mbali sana mkuu, hiyo timu ilikuwa maarufu kwa jina la 'Super Depo' daah nyakatiii zimepita kasi sana..leo hii wengi hawaitambui hyo
 
Those days...it was very nice. Nimewakumbukapia Leeds United ya kocha David O'Leary na captain wao Lucas Radebe(South Africa)... kiungo Olivier Darcout, washambuliaji Allan Smith na kitasa Rio Ferdinand...to mention afew!

Nyakati zimekwenda wapi, nawakumbuka sana Harry Kewell, olive Dacourt mfaransa huyu, Ian Harte, Lee Bowyer, Paul Robinson golikipa huyu, Viduka na uwanja wao maarufu kama Elland Road, walikufa nusu fainali 2001 au 2002
 
Dah,mbali sana nikiikumbuka Leeda United napata mshangao sana maana tangu walipotolewa kwenye hiyo Nusu Fainali ya UEFA ndio wakafa kimoja mpaka kesho,sijui walikumbwa na kitu gani hawa watu.
 
Mkuu vizazi vya sasa hawawezi kuijua Deportivo de la coruna maana imeshuka kiwango na enzi hizo ligi ya spain haikuwa maarufu sana kama sasa.

Mkuu umetema madini! Vizazi vya sasa wanaijua Chelsea ya Abramovich. Wengine hata Deniss Wise hawamjui na bado wanajiita mashabiki wa darajani!
Deportivo ilikuwa moto kote kuanzia La Liga hadi UCL.
Yule mmorocco alikuwa anakipiga.
 
Back
Top Bottom