Greatest Of All Time
JF-Expert Member
- Jan 1, 2017
- 23,620
- 52,790
Leo jumapili ya 23/08/2020 baada ya watu kumaliza shughuli zao, kazi itakuwa ni moja tu, huko Estadio da Luz, nchini Ureno ambapo kutapigwa Fainali ya aina yake kati ya PSG Vs Bayern Munich.
Ni fainali inayowakutanisha PSG ambao wameingia fainali yao ya kwanza dhidi ya mabingwa mara 5 wa kombe hilo Bayern Munich.
Ni Fainali inayozikutanisha timu zinazocheza mpira wa kushambulia tangu dakika ya kwanza mpaka ya mwisho, hasa Bayern Munich yenye vijana wenye kasi sana!
PSG itaingia uwanjani ikiwategemea zaidi Neymar na Mbappe huku Bayern Munich maarufu kama "The Bavarians" wakiwategemea zaidi Mshambuliaji hatari zaidi kwasasa ulinwenguni Robert Lewandowski na Thomas Muller mzee wa nafasi.
Bayern Munich anapewa nafasi kubwa ya kutwaa ndoo kutokana na soka lao linalotengeneza zaidi nafasi nyingi za magoli.
Mechi itapigwa saa 4:00 Usiku kwa saa za Afrika Mashariki!
Utabiri wangu ni baada ya mechi kuisha namuona Captain Thiago Silva wa PSG akienda kubeba ndoo! PSG atashinda 2-1
Tupia na wewe utabiri wako...