UCL Final: Tutegemee kuona nini katika fainali ya Madrid Vs Liverpool

Mchochezi

JF-Expert Member
Joined
Feb 29, 2012
Posts
10,962
Reaction score
7,830
Kwa upande wa Liverpool yajayo yanaogopesha, kivipi? Safu yao ya ukuta imekuwa ikivuja sana. Wanaruhusu magoli sana hali ambayo sidhani kama itawaacha salama. Namuona CR7 akienda kupiga hat trick kama ukuta wa kamanda Van Dijk na Lovren utaendelea kuwa vile.

Ila kwa upande wa pili wa shilingi naiona safu ya ushambulizi ya Liverpool ikiwanyanyasa na kuwatesa akina Ramos hasa pale Marcelo atakapokuwa anapanda huku nyuma akiacha nafasi kwa Salah kufanya yake.

Kwa upande wangu kama Chamberlain angekuwepo mchezo wa fainali taji ningewapa Liver ila kwakuwa ni majeruhi namuona nahodha wa Madrid akinyanyua kwapa mara baada ya kipenda cha mwisho pale jijini Kiev.

Wewe kwa upande wako unategemea fainal ya aina gani?
 
Mambo niii...
 
Nahisi mtoa mada n wale majamaa walioisakama Liverpool toka round 16 kuwa haifik popote lakin mwisho wa siku timu IPO final na bado haitoshi mkaona mje na matokeo yenu ya mfukoni haya ngoja tuone
 
Madrid nafasi wanayo, sema shida itaanzia pale tu wakijisahau coz wapinzani ni wepesi sana
 
Kama kawaida tutarajie ile timu kupewa penati au kadi nyekundu kwa Liver...na mpira umekwishaaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…