Muda unaokaa chuoni unaendana vipi na ubora wa elimu utakayopata?
kama ndio hivyo basi BBA, HR, BCOM degree watabadili na kuwa mwaka 1, wakati wenzetu wanaongeza miaka ya kusoma MD sisi tunapunguza
Serikali kupitia wizara ya afya inaanzisha degree ya udaktari wa binadamu ya miaka mitatu. Hatua waliyofikia hadi sasa ni kuandaa mtaala(curiculum) na watu walikuwa morogoro wiki yote hii kwa ajili hiyo. Jamani wanajamii si wanataka kutumaliza? Iweje mtu asome miaka mitatu apewe dhamana ya miili na afya za wananchi wanyonge ilhali kwa kipindi hicho haimtoshi hata kuifahamu anatomia ya mwili?
Au ni kwa kuwa wao hawatatibiwa na hawa Mavoda fasta maana hata juzi tu tulishuhudia mtu kapata upele kakimbizwa india fasta!!
come on, ...are you serious? unadhani muda sio issue kabisa katika suala la elimu? ubora wa elimu unategemea vitu vingi ikiwemo vitendea kazi (vitabu vya kaida na ziada, reagents za maabara kwa pure science,nk), ubora wa walimu, ubora wa mazingira ya shule, muda ili kuweza ku-cover yale yote yanayotakiwa kufunzwa. Kama muda sio issue basi hata elimu ya sekondari (O'level) tuifanye kwa mwaka mmoja basi badala ya miaka minne ya sasa!
Acheni uzandiki pale watu wanapotaka kuboresha nyie mnalialia, mbona RMA alipokuwa anaenda ku upgrade kuwa MA alikuwa anasoma miaka miwili badala ya mitatu kwa fresh from school? Hivi CO aliyemaliza mafunzo na kufanya kazi kwa miaka kadhaa bado anahitaji miaka 5 kama fresh from school?
Angalieni pale Muhimbili college jinsi waliotoka kazini wanavyotesa kwa kufanya vizuri kimatokeo na si kudharau kila kitu mradi kinatoka ktk serikali ya Magamba
@Suggestion, hii si habari ya kupikwa kama ulivyozoea nyinginezo. Leo nimeonana na wataalam walotoka kutengeneza mitaala hiyo na ukweli unabaki ulivyo. Subiri kuuwawa kama huamini!