Udalali ndo kazi pekee inayolipa zaidi, rahisi na haina stress yoyote

Udalali ndo kazi pekee inayolipa zaidi, rahisi na haina stress yoyote

Hivi punde

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2017
Posts
2,554
Reaction score
8,587
Kuwa dalali, hauhitaji kuwa na mtaji wa fedha, hauhitaji kuwa na madegree, haihitaji kudamka asubuhi kuwahi kazini, haina cha kupoteza, kazi tamu sana udalali.

Mtu atakupigia simu mwenyewe, akikifanikishia swala la kupanga nyumba, jengo nk inabidi umlipe hell sawa na kodi ya mwezi mmoja. Fikiria anaingiza vichwa vingapi kwa majiji kama Dsm, Arusha, Mwanza, Mbeya, Dodoma nk.

Tena madalali wa viwanja, majengo ya biashara, magari wanapiga genji ndefu sana. Dalali mjini anakula tu bata. Watoto wako shule nzuri na familia maisha safi.

Haihitaji kuwa na madegree, haihitaji kukopa benki ili upate mtaji. Upo tu home simu zinaingia zenyewe. Mara laki 2, mara elfu 50, mara laki 5 maisha safi sana

Maisha ya udadli safi sana.

Udadali ndo mpango mzima.
 
Have been into that deal 2014-2016

Changamoto ni kubwa mno hasa madalali wa magari, kuna kudhulumiana ganji,kugeukana nk kubwa Kuliko pesa ya udalali haina baraka unaweza pata ganji la 500k Leo,mpaka ukifika kesho huna kitu

spend less, save more
 
Unaweza kabidhiwa uuze gari kumbe ya wizi

Unaweza uza gari kumbe inadaiwa

Unaweza kabidhiwa gari kumbe haijalipiwa ushuru tangu iingie nchini, chasis no. Kutokufanana ya gari na iliyokwenye kadi, kiufupi inachangamoto nyingi mno

spend less, save more
 
Na ukiuza vumeo usijifiche utakapotafutwa. Stress. Kuna dalali alinidhulumu elfu 50 ila tukionana namuona kabisa anatamani ayeyuke
 
udalali wa kibongo ni kuitafuta jela na laana tu, bora uendeshe bodaboda tu.
 
udalali wa vyumba miji kama dar ni kutafuta uchizi uzeeni, sijaona dalali mwenye nyumba ya tofali hapo jijini
 
Maelezo uliyotoa hapo yanakuchanganya bure.... Huyu mwenye hivyo sio dalali bali ni tapeli. Na serikali inawatafuta usiku na mchana kwa sababu tu ya ufinyu wa ufahamu ndiyo maana wanabandika matangazo na kuweka namba za simu.

Sent from my TECNO-L8 using JamiiForums mobile app
 
Naona mleta kaleta udalali jf, watu waache kazi zao wajiunge na udalali

Sent from my TECNO-J7 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom