Udanganyifu kwenye mitihani uhesabike miongoni mwa makosa ya uhujumu uchumi

Mwamuzi wa Tanzania

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2020
Posts
15,486
Reaction score
45,256
Pamoja na yote maishani mwangu kitu kinaitwa udanganyifu kwenye mitihani nakichukia sana. Udanganyifu kwenye mitihani ndio mwanzo wa mla rushwa na fisadi.

Kama mtu haogopi kufanya cheating kwenye mitihani huyo mtu katu abadani hatoogopa kula rushwa, hatoogopa kufisadi fedha na mali za umma.

Athari nyingine ya cheating kwenye mitihani ni kuzalisha wasomi vilaza ambao kazi wanajifunzia ofisini baada ya kuajiriwa.

Udanganyifu kwenye mitihani adhabu yake iwe kifo au kifungo cha maisha. Tukichekeana hatufiki mbali.
China wamefika mbali kwa Sheria kali.

Kijana yupo chuo kikuu busy na ulevi na uzinzi lakini mwishowe anafanya cheating anapata degree
 
Pamoja na yote maishani mwangu kitu kinaitwa udanganyifu kwenye mitihani nakichukia sana.

Udanganyifu kwenye mitihani ndio mwanzo wa mla rushwa na fisadi...
Nimebahatika kusoma na kugraduate degree moja na degree za juu mara mbili. Nimebahatika kuajiliwa makampuni binafsi 3 na nimefanya kazi serikalini zaidi ya miaka 10.

Kusema ukweli vyuoni kuna udanganyifu wa hali ya juu! Hasahasa degree na degree za juu ni udanganyifu mtupu! Kuangalizia (kudesa) kunakili kazi ya mtu, kupika data ni mambo ya kawaida!

Maofisa wengi serikalini wanavyeti vilivyotokana na udanganyifu! Mwisho wa siku ndo haya tunayoyaona ya kukosa wafanyakazi waadilifu. Wengi wako maofisini kwa kulogana, kupigiana majungu, wizi, ufisadi, degree za chupi, ukabila!

Mimi yalinishinda nikaamua kujiajiri na kipato changu ni kikubwa kisichokuwa na stress! Nenda maeneo ya vyuo vyetu vikuu, kuna ulevi na ukahaba wa kupindukia na mwisho wa siku wanagraduate na kuja kuwa watumishi! Watumishi wa umma hatuna! Tuna wachumia tumbo!
 
Mambo ya hovyo mno
 
Back
Top Bottom