Nimebahatika kusoma na kugraduate degree moja na degree za juu mara mbili. Nimebahatika kuajiliwa makampuni binafsi 3 na nimefanya kazi serikalini zaidi ya miaka 10.
Kusema ukweli vyuoni kuna udanganyifu wa hali ya juu! Hasahasa degree na degree za juu ni udanganyifu mtupu! Kuangalizia (kudesa) kunakili kazi ya mtu, kupika data ni mambo ya kawaida!
Maofisa wengi serikalini wanavyeti vilivyotokana na udanganyifu! Mwisho wa siku ndo haya tunayoyaona ya kukosa wafanyakazi waadilifu. Wengi wako maofisini kwa kulogana, kupigiana majungu, wizi, ufisadi, degree za chupi, ukabila!
Mimi yalinishinda nikaamua kujiajiri na kipato changu ni kikubwa kisichokuwa na stress! Nenda maeneo ya vyuo vyetu vikuu, kuna ulevi na ukahaba wa kupindukia na mwisho wa siku wanagraduate na kuja kuwa watumishi! Watumishi wa umma hatuna! Tuna wachumia tumbo!