KERO Udanganyifu Mahospitalini

KERO Udanganyifu Mahospitalini

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

X men

Member
Joined
Dec 26, 2021
Posts
18
Reaction score
35
Habari wadau!!

Nimeona leo tujadili hili suala ambalo kadri siku zinavyozidi linazidi kuota mizizi, kumekua na udanganyifu mkubwa sana katika hizi Hospitali binafsi hasa zile zinajinasibu kutoa huduma za kibingwa, ukienda hizo hospitali mfano Nkinga referral hospital ya Igunga, Malolo Hospital ya Tabora n.k

Milango yote ya madaktari imeandikwa Daktari bingwa wa hiki na hiki, lakini ndani humo wanaotoa huduma sio Madaktari bingwa, unakuta mgonjwa anatoka zake Hospitali ya ya Wilaya ambako kuna Madaktari wa kawaida amepewa rufaa ya kwenda huko kupata huduma za Kibingwa lakini akienda anaishia kupigwa pesa na kuhudumiwa na Daktari wa kawaida kwa matibabu yale yale aliyoyapata huko alikotoka. Kwanini wanadanganya wagonjwa?

Serikali haitambui huu utapeli?

Na hii imekua ikifanyika kwa hizi Polyclinic na referral hospital nyingi nchini.

Huu ni utapeli dhidi ya afya za Watu.
 
Habari wadau!! Nimeona leo tujadili hili suala ambalo kadri siku zinavyozidi linazidi kuota mizizi, kumekua na udanganyifu mkubwa sana katika hizi Hospitali binafsi hasa zile zinajinasibu kutoa huduma za kibingwa, ukienda hizo hospitali mfano Nkinga referral hospital ya Igunga, Malolo Hospital ya Tabora n.k milango yote ya madaktari imeandikwa Daktari bingwa wa hiki na hiki, lakini ndani humo wanaotoa huduma sio Madaktari bingwa, unakuta mgonjwa anatoka zake Hospitali ya ya Wilaya ambako kuna Madaktari wa kawaida amepewa rufaa ya kwenda huko kupata huduma za Kibingwa lakini akienda anaishia kupigwa pesa na kuhudumiwa na Daktari wa kawaida kwa matibabu yale yale aliyoyapata huko alikotoka. Kwanini wanadanganya wagonjwa?? Serikali haitambui huu utapeli?? Na hii imekua ikifanyika kwa hizi Polyclinic na referral hospital nyingi nchini. Huu ni utapeli dhidi ya afya za Watu.
Unaruhusiwa kumhoji daktari kuhusu elimu yake kabla hajakuhudumia. Kama siyo sawa na hitaji lako unaachana nae. Halafu hospitali za Rufaa siyo hizo ulizozitaja kama private, hospitali za Rufaa huwa za Serikali badala ya kwenda Nkinga ungeenda Tabora, Bugando ama Benjamini Mkapa.
Kumlipa bingwa awepo kila siku si rahisi,wengi wa private mabingwa hawawaajiri,wanakuwa wanaazima toka serikalini ndomana wanafanya kwa part time tu.
So ukihitaji huduma yake utakutana nae kwa appointment.

Sent from my SM-G970U using JamiiForums mobile app
 
Unaruhusiwa kumhoji daktari kuhusu elimu yake kabla hajakuhudumia. Kama siyo sawa na hitaji lako unaachana nae. Halafu hospitali za Rufaa siyo hizo ulizozitaja kama private, hospitali za Rufaa huwa za Serikali badala ya kwenda Nkinga ungeenda Tabora, Bugando ama Benjamini Mkapa.
Kumlipa bingwa awepo kila siku si rahisi,wengi wa private mabingwa hawawaajiri,wanakuwa wanaazima toka serikalini ndomana wanafanya kwa part time tu.
So ukihitaji huduma yake utakutana nae kwa appointment.

Sent from my SM-G970U using JamiiForums mobile app
Nkinga ni referral hospital though ni ya Kanisa kama ilivyo Bugando
 
Watu wanaaamini kuwa ghali ndio quality. Sometime wanapigiwa mno. Kulipa ada kubwa hakumfanyi mtt awe na uwezo wa kuelewa Mambo na akawa na uwezo mkubwa.
Hospital za serikali ni nzuri hawafanyi biashara kivile Kama private.
Yaani mtu akitumia pesa yake kubwa kwa huduma Ile Ile basi Ego yake inakuwa inflated anajiona yeye ni Bora na anavimba mno.

Yaani ukiwa mfanyabiashara wateja ni watoto wako unawajua Wanachowaza na wanachokitaka.
Kuna muda huo mkono wako uko ndani ndani haupimwi. Yaani wanaenda na wewe ulivyoenda
 
Back
Top Bottom