KERO UDART wekeni utaratibu wa baadhi ya Mabasi yenu ya Mwendokasi kuanza kupakia abiria wanaoanzia safari katikati ya njia zenu

KERO UDART wekeni utaratibu wa baadhi ya Mabasi yenu ya Mwendokasi kuanza kupakia abiria wanaoanzia safari katikati ya njia zenu

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Mkono Mmoja

JF-Expert Member
Joined
Jan 26, 2019
Posts
3,359
Reaction score
6,568
Salaam

Imekuwa kero, shida, usumbufu na tabu kwa abiria wanaotegemea usafiri huu katika vituo vya kati vilivyopo katika njia kuu za mabasi ya mwendokasi.

Mfano njia ya kimara kuelekea gerezani ama kivukoni kwa abiria anayeanza safari yake katika vituo vya Korogwe, Bucha ,Baruti, Shekilango, Tiptop n.k kupata nafasi ya kupanda mabasi haya nyakati za asubuhi ama jioni ni ndoto kwa kweli kitendo kinachopelekea watu kuchelewa makazini na wanafunzi kuchelewa kufika shuleni.

Ombi langu kwa UDART kwanini wasiweke mabasi ambayo yataanzia kati kukusanya abiria waliokwama katika vituo hivi vya kati? kwasababu mara nyingi mabasi haya hujaza abiria kupita kiasi kabla hayajaanza usafiri kutoka katika vituo vikuu kama Mbezi magufuli, Kimara terminal, kivukoni, Morocco huku yakipitiliza katika vituo vya kati kutokana na kujaa kupitiliza.
 
Acha tuendelee kula commission hayo matatizo yenu pambaneni wenyewe
 
asante JF kwa kushare hii post kwenye ukurasa wenu wa WhatsApp....wahusika waione hii hakika abiria wanateseka.

Nyaakati za jioni kama unaanzia safari vituo kama Fire,Msimbazi,Magomeni, Kagera ,Manzese,Tiptop,Urafiki na shekilango unaweza kuganda zaidi ya saa nzima bila ya kupata usafiri basi zote za mwendokasi zinazopita katika hivi vituo huwa zimejaza kupitiliza hakuna hata sehemu ya kuweka mguu
 
1. Hivi watu wa Haki za binadamu ( ndani na nje ya Tanzania) hawaoni usafiri huu wa DART

2.Hii tabia ya kubaki na 50 50 zetu itaisha lini??..sisi tukija na 700/= mbona huwa mnatukatalia

3.Na hii tabia ya kutuweka kituoni zaidi ya saa 1 , ilihali magari yapo around MWISHO LINI?
 
Back
Top Bottom