Udasa kuchambua muswada Katiba Mpya Jumamosi

mzambia

JF-Expert Member
Joined
Dec 31, 2010
Posts
885
Reaction score
60
JUMUIYA ya Wanataaluma wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Udasa), imeandaa kongamano la pili la Katiba ambalo pamoja na mambo mengine, litajadili muswada maalumu wa sheria unaopendekeza mabadiliko ya katiba ya Tanzania. Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Makamu Mwenyekiti wa Udasa na Mratibu wa Kongamano hilo, Dk Kitila Mkumbo, alisema muswada huo una upungufu mwingi ambao lazima uangaliwe kwa umakini.

“Kwanza ni kwanini suala la tume apewe Rais, kwanini shughuli hii isifanywe na Bunge? Katika nchi za wenzetu kama Kenya, Ghana na Afrika kusini Bunge ndio limefanya hiyo shughuli,” alisema Dk Kitila na kuongeza: “Muswada unapendekeza tume iwe na watu 30, Kenya walikuwa na watu tisa tu, wakati mwingine mambo mazuri lazima tuyachukue kutoka kwa wenzetu, halafu haina ukomo wa kukusanya maoni na haiainishi moja kwa moja sifa za watu wanaotakiwa kuteuliwa kwenye tume.”

Kutokana na hali hiyo, alisema upungufu huo na mwingine, utachambuliwa siku hiyo kuwapa wananchi uelewa kilichopo kwenye muswada huo. Kwenye kongamano hilo, wananchi na watoa mada watajikita zaidi kueleza maudhui ambayo yanatakiwa kubebwa kwenye katiba na kuainisha mambo yanatakiwa kuchukuliwa kutoka katiba ya sasa.

Naye Mwenyekiti wa Udasa, Dk Mshumbuzi Kibogoya, alisema watoa mada wakuu kwenye kongamano hilo litakalofanyika Jumamosi hii, ni Jaji Mkuu mstaafu Barnabas Samata na Mkurugenzi Mtendaji Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu, Francis Kiwanga.

Pia, vyama vya siasa vyenye wawakilishi Bungeni vimelikwa na vimethibitisha ushiriki wake, CCM kitawakilishwa na Makamu mwenyekiti wake, Pius Msekwa na Chadema kitawakilishwa na Mwanasheria wake, Mabele Marando. “Kila chama kitapewa dakika kumi kutoa maoni yake na wananchi wengine watakaoshiriki wataruhusiwa kutoa maoni yao,” alisema Dk Kibogoya.
 
asante kwa taarifa,mkuu!!
muda na TV station gani itarusha LIVE????
 
Mswada usipitishwe! shughuli nzima ya kutafuta na kujadili juu ya katiba mpya upelekwe bungeni! That is enough!
 
Mswada unasema MAREKEBISHO ya katiba, wananchi tunataka katiba MPYA. Hii imekaaje jamani?
 
This make no sense; Sioni sababu ya Chuo Kikuu kuandaa mjadala wa kutolea maoni muswada wa sheria kupitia Katiba. Ni kupoteza muda.
 
This make no sense; Sioni sababu ya Chuo Kikuu kuandaa mjadala wa kutolea maoni muswada wa sheria kupitia Katiba. Ni kupoteza muda.
Hapana babu....bunge ni la CCM,kwa hiyo,without challenging this bill before it hit the floor is a recipe for disaster!
 
Hapana babu....bunge ni la CCM,kwa hiyo,without challenging this bill before it hit the floor is a recipe for disaster!

Kama Bunge ni la CCM, Rais wao, ni kitu gani kitazuia sheria isipitishwe hata ikiwa challenged? Mswada huo utapita kama ulivyo. It is an exercise in futility.
 
jE UNAAMINI KUWA BUNGE LINAWAKILISHA WATU(WATANZANIA)?
 
Kama Bunge ni la CCM, Rais wao, ni kitu gani kitazuia sheria isipitishwe hata ikiwa challenged? Mswada huo utapita kama ulivyo. It is an exercise in futility.
Let me give you an example,suala la DOWANS kutokulipwa,was brought about by the mass,the mass pressured CCM MPs and they challenged it!,CCM-CC,President and Attorney General were for it,those two pillars needs to be extremely challenged.NGOs,Technocrats,Religious organisations..etc needs to start discussing this bill,the legislature will follow the mass,trust me!...not because thats what they believe,but because thats how they gonna keep that 90mil coming!!!
 
I do believe that sothing tangible can very well still be done to knock sense into certain minds around, after all Uwezo Tunao kama wananchi wa taifa hili na wala tusione unyonge kama vile ni sifa zuri mbele ya mafisadi.

Mimi, wewe na yule, kila mmoja wetu tucheze katika nafasi zetu kwa udhati mkubwa kabisa tena bila kuchoka wala kuruhusu kugawanyika wakati sote adui wetu ni yule yule FISADI.

Kama Bunge ni la CCM, Rais wao, ni kitu gani kitazuia sheria isipitishwe hata ikiwa challenged? Mswada huo utapita kama ulivyo. It is an exercise in futility.
 


nakubaliana na wewe kwa asilimi mia moja,hii ndio hali halisi na hili ndio suluhisho mimi nimeshasema na vijana ishirini na wengi wamekubaliana na jambo hili tunahitaji muongozo na mahali pakuanzia ni kesho kwenye kongamano la katiba pale udsm
 
Ninashukuru kwa taarifa. Je, ni lini, wapi na saa ngapi kongamano hilo litafanyika?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…