UDEREVA KENGE UTAUACHA LINI?

Xubzero

JF-Expert Member
Joined
Jul 21, 2018
Posts
243
Reaction score
413
"Tuma meseji hii kwa watu 20 kuna kitu
kizuri kitakutokea ndani ya siku 3
wengine walipuuza wakafukuzwa kazi na
kupata ajali mbaya
"

Sms za hivi huwa zinanikera


yaan Tumekuwa watu wa
kuishi kwa mazingaombwe sasa,
tumegeuza maandiko na kuyaweka katika mbwembwe za kimitandao ili
kuhalalisha kuwa ibada na baraka zote
zitapatikana kupitia simu ya mkononi na
mitandao ya kijamii. Mungu si
mchezesha kamari eti kama
tunavyotumiana hivyo vimeseji, kanuni za Mungu kuhusu baraka zinaeleweka
vizuri ktk maandiko. Huko ni
kujidanganya tu badala utende matendo
yampendezayo Mungu ubaki kuona
kufowad meseji ni utume kweli kweli
wakati matendo ya utume hata huyatendi. Sasa imekuwa fashion kwa
siku unazipata mpaka tano na mtu
anafowad na kulala kifua kimejaa eti
ametenda kazi ya Mungu wakati mlango
wa kanisa haujui, hana toba, si mtoaji na
hata maana ya fungu la kumi hajui ila anangoja baraka za Bwana kwa kutuma
meseji. Je ww ni sms gani zinakukera?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…