Udhaifu wa Bunge na kitisho kwa Rais Samia Suluhu Hassan

Udhaifu wa Bunge na kitisho kwa Rais Samia Suluhu Hassan

Kaparare

Member
Joined
Apr 19, 2021
Posts
93
Reaction score
234
Kuna msemo unasema kiendacho kinazunguka hurudi kinazunguka.

Wabunge takribani Asilimia 95 walipatikana kwa kauli na Maamuzi ya Hayati Dkt. Magufuli wakati akiwa mwenyekiti na katibu wake Dkt. Bashiru (Rejea mchakato baada ya Kura za maoni) Kawaiyo jamaa hao wataendelea kulihusudu jina la mwendazake siku zote za ubunge wao. Mwanaume mmoja alisimama na ku control Kila kitu aliogopwa na kushauriwa vile apendavyo.

Kazi ya BUNGE ikawa ni kumsifu Serikali. Wachache wenye nia ya nzuri au kukosoa ili kuleta tija wakaamua kukaa kimya kulinda nafasi. BUNGE hili liliandaliwa kumtumikia mzeya bila kukunjua makucha yake.

Sio kwamba BUNGE halikujua hasara za ATCL hapana ila nani angesimama kusema. Mpaka akina Halima Mdee wapo pale kwasababu Serikali iliamua wawepo.

Sasa aina hii Bunge letu na jinsi wanavyomuhusudu John hasa wale Sukuma Gang wanaweza kuwa kitisho kwa rais Samia. Kiongozi tulienae Sasa ameonesha angalau kusimamia misingi ya utawala bora lakin hivi karibuni ni kama alitoa Warning kwa Bunge kwamba Kuna ngoma Zina pigwa sehemu na wachezaji wakuu ni Bunge Swali ni je nani anapigiwa hizo ngoma na mwenye Shughuli?

Ni rais Samia au Hayati Magufuli mwendazake?

Ni ukweli usiopingika kwamba alama alizoziacha mwendazake zipo katika Sifa zote nzuri na mbaya na katika nyanja zote kiuchumi kiutawala na kisiasa.

Na jinsi mambo yalivyo kumuhujumu rais Samia ni kitu rahisi Mno kuliko tunavyofikiria. Na Maamuzi yake kumpeleka Dr Bashiru Bungeni it's another mistake japo najua tarehe 30 April atapata Fresh Air kwenye ofisi yake nyingine.

Kulivunja Bunge sio Sahihi kwasababu ya gharama za Uchaguzi japokuwa kwa wasihuzunike Sana kwasababu walilazimishwa kuwapigia Kura watu wasiowataka.

Time will tell

Neno langu sio halali
 
Rais Tanzania anazo nguvu za kifalme, hakuna wa kumfunga breki. Asipozitumia kwa faida ya taifa na yake itakuwa ni kwa hasara yake na yetu.
 
Back
Top Bottom