Udhaifu wa Hoja za Mohammed Said katika Makala ya Uislamu na Siasa katika Tanzania



Salaam ndugu yangu.Ndio maana sensa ya mwisho ya watu na makazi waumini wa dini ya kiislamu walipigania sana kipengele cha dini kihusishwe ili kuundoa huu utata unaosema waislamu walipungua sana baada ya 1957 kama ni kwa kufa au kubadili dini.Kwa akili nyepesi tu jamani,hivi inaingia akilini jamii yenye kushajihisha kuoa wake wengi na kupenda kuwa na watoto wengi leo hii wawe idadi yao ikipungua kwa kasi? Ngumu kumeza
 
Huyu mzee huyu na siasa dini zake
Mazaya,
Hofu ya dini ndiyo iliyofanya mchango wa Waislam katika kupambana na ukoloni ufutwe katika historia ya Tanganyika.

Ikiwa wewe unaona mimi nimefanya makosa kuiandika historia hii basi hiyo ni bahati mbaya kwako na hainihangaishi kupewa majina.
 
Ni wazi kuwa, Watu wa Ukanda wa Pwani, ndio walioanzisha Mapigano ya Majimaji na indeed eneo kubwa lililopigana na Wajerumani 1905-07 ni jamii za kiislamu. Nafahamu vyema kuwa, ni wakazi wa Ukanda wa Pwani (na si Waislamu kama wanadini) waliokuwa wa kwanza kupambana kwanza na Mjerumani (Abushir Bin Salim - Pangani 1888-89) na pia Muingereza kupitia Siasa. Hiyo yote ilisababishwa na kwamba, kabla ya Wazungu, Wakazi wa Pwani walikuwa tayari na ustaarabu wa Pwani wakiunganishwa na Lugha ya Kiswahili, pamoja na Dini ya Kiislamu. Of course, katika Karne ya 19, Pwani ya kuanzia Kusini ya Sofala (Mozambique) hadi Lamu, ilikuwa chini ya Sultan aliyehamia Makao yake Zanzibar mwaka 1832 (1840).
Kwa upande wa Bara, hakukuwepo lugha ya kuunganisha makabila mbalimbali licha ya Kiswahili kujulikana kwenye Njia Kuu tatu za Biashara ya Watumwa. Vilevile, hakukuwepo imani moja na zaidi kila Kabila lilikuwa na Utawala wake. So, ilihitaji Wajerumani kuanzisha kwanza mwaka 1886-90 Dola la DOAG (Tanganyika, Ruanda-Urundi) ili kuwaunganisha Watanganyika katika Taifa la Tanganyika.
Baada ya kushindwa kwa Vita vya Kwanza vya Kupinga Ukoloni, Watanganyika wa Interior walilazimika kukubaliana na Mfumo wa Kikoloni ili kuweza ku-survive hasa baada ya kushindwa vibaya katika Vita ya Maji Maji. Na tukumbuke kuwa, ukiacha Wahehe na Wangoni, katika Makabila yaliyopigana kwenye Maji Maji, hakuna lililopigana na Wajerumani katika Mapambano ya Awali (Early Resistances) ya 1880s - 1890s.
Ni akina nani waliwapokea Wazungu kwa vizawadi hadi kuweza kujenga Maboma ya kuweza kuishambulia Nchi nzima? Jibu ni wakazi wa Pwani.
Aidha, Wakazi wa Pwani waliweza kuorganise mapambano coz Makao Makuu ya kikoloni yalikuwa Dar es Salaam, huku mji muhimu kiuchumi ukiwa Tanga, so ustaarabu wa Pwani ulichangia watu wa Pwani kuongoza mapambano kuanzia miaka ya 1920 - 1940s. Kumbukeni kuwa, hadi katika Sensa ya 1948, miji mikuu ya Tanganyika, ilikuwa karibia yote ya kiislamu - 1) Dar es Salaam, 2) Tanga, 3) Mtwara, 4) Tabora 5) Mwanza 6) Lindi, 7) Kigoma, 8) Dodoma 9) Morogoro na 10) Moshi - ukitoa tu miji ya Mwanza na Moshi.
Hata hivyo, kufikia 1978, miji mikuu ya Tanzania, ilikuwa - 1) Dar, 2) Mwanza, 3) Tanga 4), Mbeya, 5) Tabora, 6) Morogoro, 7) Iringa, 8) Arusha, 9) Moshi na 10) Kigoma, sawa na miji mitano ya kiislamu na mitano ya kikristo. But kufikia 2012, miji mikuu ni - 1) Dar, 2) Mwanza, 3) Arusha, 4) Dodoma 5) Mbeya 6) Morogoro, 7) Tanga, 8) Tabora, 9) Kigoma 10) Sumbawanga.
Na ni wazi kuwa, Viongozi wa Kiislamu, walitaka nchi iongozwe kiislamu ndiyo maana wao walipigania uhuru kwa upande wao tu wala hawakuwahi kufanya Ziara nchini kueneza Sera zao mpaka Nyerere alivyoingia ulingoni.
Na wasomi wengi huwa wanakiri kuwa, wanasiasa wa Tanganyika hawakuwa active kabisa kulinganisha na Nchi nyingine mpaka Nyerere alipokuja. Na kama tusingekuwa Trusteeship, walahi tungesumbuka sana kushindana na wakoloni kwa kuwa, tulienda kwenye mapambano hatujaungana vya kutosha. Chanzo cha kuzubaa huko pia kulichangiwa na uchumi usio na nguvu plantation & peasant economy.
 
Wanapendwa kisiasa kwa sababu wao hawajagawanyika hapa nchini kama Wakristo. Licha ya uwepo pia wa factions nyingi kwenye uislamu, Waumini wa Sunni Tanzania inadaiwa wanazidi asilimia 95% ya Waislamu wote. Fikiria Wakristo wote wangekuwa RC ama KKKT au Anglican? Hapo umoja ungekuwepo tu.
Vilevile, kutosoma na umasikini mkubwa umekuwa ukisabababisha kuwa rahisi kuwarubuni kuliko maeneo yenye wasomi. Aidha, maisha ya Kiislamu hayatofautishi dini na siasa, hivyo huwa ni rahisi viongozi wa dini kutumia vitabu vitakatifu kufundisha maisha ya kisiasa na kutoa msimamo wa kidini hivyo kuwa rahisi kupenyeza ajenda. Hali hii huwa ngumu kwa Wakristo, watakuhama.
 
Mgambilwa...
Mimi nitagusa para yako ya mwisho.
Hayo usemayo ni historia ya Chuo Cha Kivukoni.

Soma historia ya Hassan Suleiman na Ali Juma Ponda katika ''Modern Tanzanians.''
na ya Kleist Sykes, ''Modern Tanzanians, John Iliffe (ed), East African Publishing
House, Nairobi, 1973.

Hao hapo juu Hassan Suleiman na Ali Juma Ponda walikuwa
viongozi wa African Association katika miaka ya 1940 Dodoma.

Historia ya maisha yao katika siasa za kikoloni itakufungua macho.
Sitaki kukuambia umsome Abdul Sykes hapo ni karibu sana.

Ukitaka turejee kwenye historia ya Nyerere peke yake kazi itakuwa kubwa kwa kuwa
huko tushapita miaka mingi.

Lakini nakuwekea hapo chini taarifa za kijasusi za Special Branch usome huenda
utapa moja au mawili ya kukufikirisha:

 
Nimeona post zake mara nyingi, iko hivo! Mara utaona anaandika "ngoja tusiandike yote!"
Mwanyasi,
Kwangu kuitwa mdini kwa kusahihisha historia ya wazee wangu hainipi shida.
Kinachonishughulisha mimi ni mafanikio ya juhudi zangu.

Nakupa mfano mdogo tu.

Baada ya kuandika maisha ya Abdu Sykes katika kupigania uhuru wa Tanganyika
na kuunda TANU hatimae katambuiliwa na karejeshwa katika historia.


Kushoto Kleist Sykes, Miski Sykes Mwandishi (ameshika Medali ya Mwenge wa Uhuru
aliyotunukiwa Abdul Sykes katika sherehe za miaka 50 ya uhuru wa Tanganyika) kwa
kutambua mchango wake katika kuunda TANU na kupigania uhuru wa Tanganyika, Daisy
Sykes na Ilyas Sykes.

Jopo la Chuo Cha Kivukoni waliokuwa wanaandika historia ya TANU walikataa kupokea ''notes,''
za Abdu Sykes ziwaongoze kujua ni vipi Mwalimu Nyerere aliingizwa katika uongozi wa TAA
1953.


Pamoja na Abdul Sykes waliondolewa wote aliokuwanao, Hamza Mwapachu, Sheikh Hassan
bin Amir, Sheikh Suleiman Takadir, Iddi Faiz Mafungo kwa kuwataja wachache.

Hainishughulishi mimi kuitwa jina lolote liwalo lile muhimu ni kuwa leo historia hii imerudishwa
ilipostahili.
 
 
Nashukuru kwa kujibu hoja kwa hoja but nikiri wazi kuwa, tangu ni kuwa Primary, nimefahamu thamani ya Jina Sykes coz walikuwepo wawili kwenye Wajumbe wa Mkutano Mkuu uliosnzisha TANU. Na sikubaliani kabisa na mitazamo kuwa, kuna watu Historia imewasahau, bali wao wenyewe walitaka kupinga na Kanuni ya Somo la Historia na Siasa - Wanaoandikwa ni wenye nguvu, so ukitaka kujulikana kwenye Historia, fuatana na mwenye nguvu. Nadhani yaliyowatokea watu wenye nguvu ndani ya TANU kama Zuberi Mtemvu, ni matokeo tu ya hii Kanuni.
Hata hivyo, endapo Nyerere hakuwa extraordinarily good, asingeteuliwa kamwe kuwa Rais wa TAA, kutokana na
nguvu ya Waislamu na jinsi ambavyo walikuwa wako skeptical na Wakristo.
Angalia hapa chini, uone wingi wa Waislamu kwenye miaka ya hadi 1950s.

Tanganyika African National Union - Wikipedia, kamusi elezo huru
 

WAKIRUDISHA ITASAIDIA KUPATA KUJUA DEOGRATIAS KISANDU NA DINI YAKE MPYA INA WAUMINI WANGAPI PIA, HAPO BAADAE ITASAIDIA KUMUWEKA KWENYE HISTORY YA KUIKOMBOA TANZANIA KAMA ANAVYO DAI YEYE PIA ILI ISIJE IKATOKEA KAMA HAYA YA MUSLIM KUSAHAULIKA
 
Mgambilwa...
Kwanza napenda kidogo niongeze kitu katika kauli yako kuwa kulikuwa na Sykes
wawili katika mkutano wa kuasisi TANU.

Ndani ya chumba cha mkutano walikuwa ndugu wawili Abdul na Ally Sykes na
mlangoni, nje ya mkutano ule alikuwapo mdogo wao Abbas Sykes.

Si hivyo tu na hata hiyo African Association yenyewe, baba yao Kleist Sykes ndiye
alikuwa katibu muasisi mwaka wa 1929 na Kleist ndiye na wenzake alijenga hiyo ofisi ya TAA ilipokuja kuzaliwa TANU.

Hii itakufikirisha kidogo iweje iwe hivi?

Unasema hukubali kuwa kuna watu waliosahauliwa katika historia lakini ukweli ni
kuwa kitabu cha maisha ya Abdul Sykes kilipoingia nchini kutoka Uingereza mwaka
wa 1998 na watu kusoma vipi Abdul Sykes na Hamza Mwapachu waliunda TANU,
palikuwa na mshtuko mkubwa kwani si wengi wakiyajua haya.

Swali lililofuatia likawa, ''Nyerere anaingiaje katika historia hii?''

Kitabu kilijibu kila swali lililoulizwa ikawa wale waliosahauliwa katika historia nimewarudisha na
wasomaji wakawa sasa wanasoma historia mpya kabisa na majina mapya kabisa ambayo
hawakupatapo kuyajua au kuyasikia maishani kwao.

Na nani alikuambia kuwa wazee wangu walitaka kujulikana?
Wajulikane ili iwe nini?

Hawa watu walikuwa maarufu kwa miaka na miaka wala hawakupata umaarufu kwa ajili
ya siasa.

Hili ni muhimu ulijue.
Ikiwa unataka ushahidi wa ukweli huu sema nitakupa In Shaa Allah.

Kuwa Nyerere alienea vyema katika uongozi hilo wazee wangu walilijua na ndiyo kisa cha
kumtanguliza mbele na nimeeleza hili kwa kirefu katika kitabu.

Kuhitimisha umenichekesha kidogo kwa kunipa rejea yangu mwenyewe nisome.
Hiyo Wikipedia ni mimi huyo.

Nadhani tumefahamiana vyema.
 
Hiyo rejea haikuwa kwa ajili yako, maana najua kupitia mabandiko yako ya nyuma ambayo nilishayasahau. Nilitaka watu waone jinsi Waislamu walivyokuwa wengi miaka ya Inter-War Periods (1920s - 1940s).
Nina uhakika hakuna Mtanzania mwenye akili timamu asiyetambua mchango wa Wazee wetu hao na in fact, kuna wengi katika kizazi chetu tunawafurahia hasa wale jamaa walioibadilisha TAA 1954 kuwa TANU.

Mimi naongea haya kama Mtaalamu wa Jiografia na Historia ya Kimataifa. Naelewa wazi kuwa, pasipo Hitler - WW II & UNO, mambo ya African Nationalism, tungeendelea kuyasikia bombani possibly hadi leo, Africa ingekuwa chini ya Muingereza na Mfaransa. Ni wazi kuwa, kabla ya WW II, ni South Africa na Southern Rhodesia pekee zilizokuwa angalao active kwenye siasa nayo ilitokana na settler economy kwenye nchi hizo. Ndiyo maana hata model wa Afrika - Ghana (Gold Coast) hawakufanya chochote cha maana mpaka baada ya WW II. Angalia nchi nyingine zilizokuja kuwa active pia - Nigeria, Ivory Coast, Kenya - zote zilisikika baada ya 1945 coz ndipo ambacho Resistance (Passive) ilijibadili kuwa Nationalism baada ya Maaskari wa Kiafrika kujionea wenyewe kwa macho yao jinsi Waingereza (na Allies) walivyokuwa wakichapwa huko Ethiopia & Eritrea dhidi ya Waitalia ama Burma dhidi ya Wajapan na hivyo kuua ile myth ya muda mrefu ya White superiority.
Of course, Nchi za kiarabu zilianza kupata uhuru kwa urahisi kuanzia mwaka 1951 (Libya), lakini yote hayo yalikuwa ni matunda ya athari za WW II. So, ndiyo maana wanasiasa wa kuanzia miaka ya 1950s wamejijengea umaarufu mkubwa siyo Afrika na Asia tu bali Dunia nzima. Kulikuwepo Euphoria kubwa sana Afrika na Dunia nzima kati ya mwaka 1945 (UNO) hadi 1963 (OAU).
 
Mgambilwa...
Ahsante sana kaka kwa historia hiyo.

Umenigusa nilipokusoma kuhusu Rhodesia kwani imenileta kwenye kumbukumbu za Ally Sykes na
Kenneth Kaunda katika miaka ya 1950 wakati Mwalimu Nyerere bado hajajuana na yeye.

Hizi barua zipo katika Nyaraka za Sykes na mimi nimezisoma zote wakati naandika kitabu cha Abdul
Sykes.


Si hili tu Ally Sykes alikamatwa Salisbury 1953 wakati yuko njiani kwenda Lusaka kuhudhuria mkutano
ulioitishwa na Kaunda, mkutano ambao ungewakutanisha vyama vya wapigania uhuru vilivyoko Chini ya
Jangwa la Sahara.

Hiki ni kisa cha kusisimua sana.
Umeitaja Ghana.

Ally Sykes alihudhuria sherehe za uhuru wa Ghana 1957.

Nkrumah alikuwa kiongozi muhimu sana na TAA walinakili katiba ya Convention Peoples Party (CPP)
neno kwa neno kuwa katiba ya TANU.

Katiba ya TANU haikuandikwa na Nyerere kama wengi wanavyoamini.
Umetaja Kenya.

Ally Sykes akijuana na Kenyatta akiwa Nairobi 1945 baada ya kutoka Burma WWII.

Abdul Sykes alifanya mkutano na Kenyatta, Nairobi 1950 pamoja na viongozi wengine
wa KAU kama Bildard Kaggia, Paul Ngei, Achieng Oneko, Kungu Karumba kwa
kuwataja wachache.

Jiulize agenda ilikuwa nini?
Sasa tuhitimishe na Burma.

Ilikuwa Burma ndipo Abdul alipokuja na fikra ya kuunda TANU.

Nakuwekea hapo chini Abdul na Ally Sykes wakiwa Burma WWII katika sare za King's
African Rifles (KAR).


Kulia: Abdul na Ally Sykes Burma Infantry
 
Hiyo picha ya akina Sykes nilishaiona though sikumbuki ni wapi? Seriously uko vizuri kwenye historia yetu hasa small details ambazo probably ndizo zilizokuwa na athari kubwa kwenye siasa yetu.
Kwa kuwa, nilishasoma zamani nyaraka zako huko nyuma (kupitia humu JF), nikiri wazi kuwa, kwenye historia umesema maneno yaliyo kweli kabisa.
Shida inakuja (hata wewe umeiongelea vyema) kwenye Sera za kikoloni na jinsi zilivyowabagua wananchi wasiosoma. Ubaguzi huu wa kielimu na kipato hasa kwenye Uchaguzi wa 1958, siyo kosa la Nyerere na kamwe Nyerere asingeweza kufuata mfumo mwingine zaidi ya Mfumo unaotumiwa Dunia nzima wa Merit System katika kuajiri watumishi Serikalini.
Watu wengi huwa wanalalamika kuwa, Serikali imeitenga Mikoa ya Kusini. Lakini kwa mwenye akili yoyote hawezi kukubaliana na usemi huo. Umasikini use uliletwa na uduni wa eneo hilo katika uzalishaji wa mazao muhimu ya kibiashara. Mtu utongelea juu ya ukosefu wa miundombinu lakini watu hao wajiulize kwa nini, Mkoa wa Kagera haukuwahi kuwa na Barabara ya lami mpaka miaka ya 1990 (Nyakanazi - Ngara) but still wakazi Bukoba, Misenyi, Muleba na Karagwe walizunguka Uganda - Kenya - Arusha kufika Dar? Mbona Mkoa wa Mara nao ulisubiri mpaka 1980s kupata lami ya Mwanza - Musoma? Unaweza kuilinganisha Mikoa hiyo na upi kule Kusini?
Isingekuwa jitihada za Nyerere, Mikoa ya Kusini na Mkoa wa Pwani, ingekuwa masikini zaidi kuliko ilivyo sasa, ndiyo maana ina wastani mkubwa wa uwakilishi bungeni kuliko Ukanda wowote hapa nchini. Ndiyo maana katika jitihada za Serikali kuwainua zaidi Waislam kielimu, wanaofaidika zaidi ni Waislamu wa kutoka Lushoto, Muheza, Korogwe, Same, Kigoma na Morogoro (upstairs wako vizuri), huku wale wa Mtwara, Lindi, Tunduru, Bagamoyo, wakiachwa nyuma.
Kama Nyerere angekuwa na upendeleo, angepigania sana kujenga kwao Mara but nenda Butiama, isingekuwa juhudi za Mkapa, Nyerere hakuwa na nyumba ya maana mahali popote. Mlinganishe na Viongozi wengine utapata jibu jinsi walivyo na mahekalu lakini wameshindwa kufanya chochote cha kuondoa tofauti ya kielimu.
Muhimu ni kuwa, siyo maeneo yote ya Kikristo yamekuwa na maendeleo kuliko ya Waislamu na hata maeneo ya kikristo yamekuwa na utofauti mkubwa. Angalia mifano ya Wilaya masikini za Kasulu, Kibondo, Kasulu, dhidi ya Rungwe, Kyela, Rombo ama Hai.
 
Mgambilwa...
Mie siko katika hayo unayoeleza hapo juu.

Mimi nilinyanyua kalamu baada ya kujua kuwa kuna watu hawaitaki historia ya
kweli ya uhuru wa Tanganyika na waliokuwapo madarakani wamekaa kimya,
''basking under other people's shadow.''

Na walipokujakutoa nishani wakawa wanajipa wenyewe kwa wenyewe hapo
ndipo nikaamua kuzungumzanao kupitia kalamu na karatasi.
 
Nadhani kwa mwenye akili, ataelewa wazi kuwa, kutokana na maendeleo makubwa na coordination nzima iliyokuwepo katika Ukanda wa Pwani kuanzia Karne ya 10 AD, kutokea Sofala (Msumbiji) hadi Kisimayu, Merca mpaka Berbera (Somaliland) atakubali kuwa, umoja wa Watanzania umeletwa na mchango wa ustaarabu huo katika kueneza lugha ya Kiswahili, pamoja na Dini ya Kiislamu.
Mimi nilichokubali sana katika uandishi wako ni namna baadhi ya 'small details' zilizoachwa (kwa kujua ama kutojua) kwenye vitabu vya Historia zilivyosababisha kuwepo kwa gap kubwa ya taarifa na data za kipindi cha ukoloni.
Kama nilivyokuwa nimetangaza awali interest yangu kuwa Mimi ni mkristo, nimefurahi kujibiwa katika bandiko na Muislamu kuliko ambavyo ningejibiwa na Mkristo mwenzangu. Zaidi nimefurahi sana kujibiwa na mlengwa mwenyewe kwani umelipa bandiko hili legitimacy kubwa na possibly tungekuwa kwenye Jukwaa la Siasa, tusingeweza kuelewana. Thanx Saeed, you had already done your part, now it's our turn to try to amend the former mistakes or rather to be ready to face the consequences of making uninformed decisions ....
 
Mgambilwa ni mntu na mohamed said asanteni sana kwa discussion zenu kwani tunanufaika wengi na hili somo. Mungu awaoengezeeni ilmu na hikma.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…