Udhaifu wa Hoja za Mohammed Said katika Makala ya Uislamu na Siasa katika Tanzania

mgambilwa Ni MTU Lkn Shekhe muhammed Saidi ni MTU na Nusu..

Sent using Jamii Forums mobile app
Alwayz...
''...I am a man and a half, two wrapped in one....
me and a camel went across the desert and and there
was no water in sight, the camel died trying and your
man and a half is here loving you tonight...''

Lyrics kutoka katika nyimbo ya Wilson Picket, ''A man
and a half.''

Umenirudisha nyuma miaka 50 nikiwa mtoto miaka 16
nasoma sekondari na nilikuwa na guitar langu Hoffner
electric ni ''make,'' ya Kijerumani.

Wakati wetu lilikuwa guitar linalotumiwa na wapigaji
maarufu duniani.

Nikiipiga hii nyimbo na opening yake ni lead guitar...

Sina hakika ile lead alipiga nani Steve Crooper au
Bobby Womack...

Itafute katika YouTube usikilize.
 
Swadakta Shekhe Mungu akuweke Na yy pekee ndo wakukulipa dunian na akhera kwa kazi kubwa uloifanya Ya kuileta historia halisi ya Tanganyika hutasahaulika milele..
 
Mchango wa waislam katka kuleta uhuru utakusaidia nini?......uhuru wa nchi Yetu uliletwa na wananchi wazalendo ambao ni mchanganyiko wa waislam na wakristo sasa wewe ukitaka kuleta maswala ya mgawanyko wa nani walikuwa wengi ama wachache katka zoez zima lakuleta uhuru unapandikiza hisia na miamko yakibaguz sana.....ukitaka kuujua mchango wa wenyekujibagua fuatilia kile kilichoitwa AMNUT hapo ndo utajua kuwa wabinafsi ni kina nani haswa vinginevyo kaa kimya sababu unachokitafuta huto kipata kwakuwa watanzania wa sasa tunaishi kama ndugu.....wewe uza tende zako na haluwa hapa mimi niuze kitimoto yangu pale na baadae ww umuoe Grace mimi nimuoe Khadija uone kama k2 udin kitaendelea kukaa vchwan kwa wa tz wenye vinyongo vya kijinga na mfu kama hcho chakwako ww...enough is enough khaaa!.....huo ukumbi unaosema ulikukalia kimya atamlio wa sindano ungesikika walikuwa wanautafakari mtizamo wako uliojaa umbumbumbu wa kiwango cha juu. Kama taifa inatupasa tuwe bize na vipaumbele vya maendeleo yetu kwanza badala yakukaa kujua nani wengi nani wachache sabu haitotusaidia k2 kwa dunia ya sasa inayo emphasis unity rather than disunit.....
Hiyo research yako ni nzur tunashukuru lakin ukiiangalia kwa jicho la3 ni sawa na menu iliyowekwa mezan inayoeleza jinsi ya kumla mbwa ilhali twajua kuwa mbwa ni kharam.
 
Mwana...
Mchango wa Waislam utanisaidia nini?

Swali zuri lakini ili uelewe kwa nini niliandika kitabu kuhusu mchango
wa Waislam inabidi kwanza nikusomeshe jina la la kitabu.

Lakini tambua kuwa hii ni ''field of inquiry,'' maarufu sana katika vyuo.
Mimi si wa kwanza ukipenda msome Augustus Nimtz, Imtiaz Yusuf na
James Brennan kwa kuwataja wachache.

Kitabu kinaitwa, ''The Life and Times of Abdulwahid Sykes (1924 - 1968)
The Untold Story of the Muslim Struggle Against British Colonialism in
Tanganyika.

Sasa wewe kamata hapo kwenye, ''Untold..'' yaani hakukupatapo kuelezwa.
Sasa jiulize iweje historia hii haikupata kuelezwa?

Ukiipata sababu itaondoka ajabu.

Lugha ya matusi kama matumizi yako ya neno, ''ujinga,'' hapana sababu una
hoja tunajadili kwa adabu huna cha kuchangia unakaa kimya.

Hao waliokaa kimya Chuo Kikuu cha Iowa ni kwa sababu wote hawakuwa na
majibu katika hoja niliyowapa kujibu swali lao waliloliweka mwisho ili nitoke
jukwaani kichwa chini.

Majibu yale ndiyo yaliyosababisha nialikwe papo kwa papo Chuo Kikuu Cha
Northwestern, Chicago kufanya mhadhara mwingine kwa somo hili hili ambalo
mimi na wewe tunajadili hapa.

Mtu ''mbumbumbu,'' kama ulivyoniita haalikwi kuzungumza kwenye vyuo vikuu
tena Marekani.

Hayo mengine sioni sababu ya kuyasemea.
 
Hicho kitabu chako ni kama menu inayoelezea jinsi yakumla mbwa ilhali twajua kuwa mbwa ni kharamu....miaka 50 ya uhuru ndo unakuja leo kuamsha hisia mfu kwamba waislam tunapuuzwa katka historia ya kupigania uhuru....nchi imetulia tuliii ww unaanza kupandkiza mgawanyiko itakusaidia nini? Ok tumesha kusoma nakukuelewa sasa je taifa linanufaika vipi na hiyo historia ilopuuzwa then ukaja kuiibua ww.....umeongelea kualikwa chuo kikuu cha Northwest chicago as if its a big deal,....ndugu ondoka kwenye mfumo wa industrial age sabu tupi katika information age zaid....andiko lako la ulalamish la kuchanganya siasa na dini linazd kutia kinyaa kwa kila anaelisoma sababu limejaa ukakas wa kila rangi.....narudia tena MKUU WACHA KULIGAWA TAIFA.....hao unaowasema kwamba mchango wao umepuuzwa wanakupuuza kwa vijitabia vyako vya udini....thanks God mtu kama wewe huna wadhifa mkuuubwa serikalini kwa maana tungeshuhudia ajira na tenda za udini...narudia tena kila anaeskiliza uzushi wako anakupuuza sababu fikra zako ziko very far backward about 1950s.
 
Mwana...
Unaandika umeghadhibika na kutukana kwangu inakuwa tabu
maana si mjadala bali ni ugomvi na matusi.

Hapana udini ila nimeandika historia ambayo ilikwepwa kwa
makusudi na kitabu wala si cha jana kilichapwa Uingereza
mwaka wa 1998 Kiingereza (London) na Kiswahili 2002
(Nairobi).

Kitabu kimependwa na sasa tunakwenda toleo la nne Kiswahili
na la tatu Kiingereza.

Kupuuzwa si kweli.
Kitabu hiki kimenifikisha kwingi wala sikutegemea.

Lakini ikiwa unataka kuwajua walioligawa taifa hili nakupa rejea
hizi uzisome.

Msome P van Bergen, ''Religion and Development in Tanzania,''
(1981) na Sivalon, Kanisa Katoliki na Siasa...(1992).

Ukipenda msome Hamza Njozi, ''Mwembechai Killings...'' (2002)
ila kitabu kimepigwa marufuku.
 

Mkuu Mohammed Said,
Kuna siku moja ulitoa ushauri hapa kuwa ukiona umetoa hoja na unajibiwa kwa jazba au matusi basi ni dalili fika kuwa mpinzani wako ameishiwa na hoja
Huyo aliyekujibu na matusi tayari umeshamshinda.
Hongera
 
Mkuu Mohammed Said,
Kuna siku moja ulitoa ushauri hapa kuwa ukiona umetoa hoja na unajibiwa kwa jazba au matusi basi ni dalili fika kuwa mpinzani wako ameishiwa na hoja
Huyo aliyekujibu na matusi tayari umeshamshinda.
Hongera
Sheriif,
Mwalimu wangu Sheikh Haruna alinifundisha elimu ya mjadala
alikuwa akisema kuwa mwenye hoja hatukani na ukiona mtu
anatoa lugha chafu jua kashindwa.

Huu ni mjadala tu hakuna sababu ya watu kutukanana.

Huyu kashindwa hana hoja kwa hiyo ghadhabu zinapanda na
mwishowe anaishia matusi.
 
achana nae huyo,tupe elimu mzee
 
Acha kudanganya watu wewe alicho kisema Mohamed saidi ndio ukweli halisi ukitaka ndio hivyo usitake ndio hivyo baki na chuki zako
 

Sasa wafiche ili isaidie nini, sensa ya 2012 Kikwete na Gharibu wote walikuwepo? Viongozi wenu wachache wanajua ukweli mmebaki nyie wachache ambao kwenu dini imewazidi akili
 
Acha kudanganya watu wewe alicho kisema Mohamed saidi ndio ukweli halisi ukitaka ndio hivyo usitake ndio hivyo baki na chuki zako

Kina ukweli gani, nchi hii imewahi kuongozwa na waislamu kati ngazi za juu za uongozi, kivipi yafichwe haya, Mzee Saidi kwa kuwa sasa ameelimika ndio maana baadhi ya maneno anaondoa kwa kuwa anaujua ukweli, na nyakati hizi mambo yamebadilika kweli
 
Mgambilwa,
Ahsante kwa darsa hii uliotuwekea hapa.

Mimi nataka nikujibu kitu kimoja tu nacho ni kuhusu historia ya Mwalimu Nyerere
katika TAA na TANU kwani wengi hawaijui na hili nimeliona pia kwako.

Hata Mwalimu Nyerere mwenyewe hakupatapo kueleza vipi aliingia katika uongozi
wa TAA na TANU hebu soma hapo chini:

''Mwaka wa 1950 palifanyika mapinduzi TAA kuwatoa madarakani TAA President Mwalimu Thomas Plantan na Katibu Clement Mtamila.

Waliopanga na kukamilisha mapinduzi haya walikuwa Hamza Mwapachu na Abdul Sykes wakisaidiwa na Schneider Abdillah Plantan.

Sababu ya mapinduzi haya ni kuwa TAA chini ya uongozi wa Mwalimu Thomas ilishindwa kukidhi mategemeo ya wanachama ambao walitaka kuiona TAA inaingia katika siasa za kuitoa nchi katika mikono ya Waingereza.

Kutokana na mapendekezo ya TAA Constitutional Development Committee ambao wajumbe walikuwa Mufti Sheikh Hassan bin Ameir, Sheikh Said Chaurembo, Hamza Mwapachu, Steven Mhando, Abdul Sykes na John Rupia yaliyopelekwa kwa Gavana Edward Twining, serikali ikishtushwa sana kwani mapendekezo yalizungumza ''kura moja mtu mmoja,'' na Tanganyika huru 1963.

Earle Seaton Mwanasheria kutoka Bermuda aliyekuwa akifanya shughuli zake za uwakili Moshi alisaidia sana katika kutayarisha mapendekezo haya.

Huyu Seaton alikuwa rafiki wa Abdul Sykes.

Kutokana na mapendekezo haya Dr. Kyaruzi akahamishwa kupelekwa Jela ya Kingolwira kisha Nzega.

Hii ilikuwa njama za Twining kupangua uongozi thabiti wa TAA.
Mwapachu akapelekwa Nansio, Ukerewe.

Abdul Sykes akashika nafasi ya Dr. Kyaruzi akawa Kaimu Rais na Secretary.
Huko nyuma Abdul na Mwapachu walikuwa wamepanga kuibadili TAA kuwa chama cha siasa.

Kuanzia mwaka wa 1951 Abdul akawa na mazungumzo na Chief David Kidaha Makwaia kumtaka ajiunge na TAA wamchague Rais wa TAA na kisha waunde TANU kwenye mkutano mkuu wa TAA wa mwaka unaofuatia.

Mazungumzo haya hayakuzaa matunda.
Mwaka wa 1952 Julius Nyerere akaja Dar es Salaam kama mwalimu Pugu.

Joseph Kasella Bantu akampeleka Nyerere nyumbani kwa Abdul Sykes kumtambulisha.

Unaweza ukasema safari ya Nyerere kuja kuwa kiongozi kwa kuchaguliwa kwanza kuwa TAA President 1953 inaanza hapa.''

Itaendelea In Shaa Allah...

Kuanzia mwaka wa 1952 Nyerere alipokutana na Abdul Sykes kulikuwa na mazungumzo baina ya Abdul Sykes na Hamza Mwapachu kuhusu kumuingiza Nyerere katika uongozi wa TAA kama rais katika uchaguzi wa mwaka wa 1953.

Haya ni baada ya mazungumzo kati ya Abdul Sykes na Chief Kidaha Makwaia kutofikia muafaka.

Miezi ya mwanzo ya mwaka wa 1953 Abdul akiongoza na Ali Mwinyi Mwinyi Tambwe walisafiri kwenda Nansio kwa Hamza.

Huyu Ali Mwinyi Tambwe alikuwa Katibu wa Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika, yaani umoja wa Waislam wa Tanganyika chama alichoasisi Kleist Sykes mwaka wa 1933 akiwa Katibu na Mzee bin Sudi akiwa Rais.

Viongozi hawa walishika nafasi hizo hizo pia katika African Association.

Abdul alitaka kauli ya mwisho kutoka kwa Hamza kuhusu Nyerere kama yeye ampishe Nyerere kwenye nafasi ya urais na amsaidie kushinda nafasi hiyo na mwaka unaofuatia 1954 waunde TANU na kudai uhuru wa Tanganyika.

Hamza alkuwa anaamini kuwa kwa ngwe ile iliyobakia kwa Waafrika kupata nchi yao Nyererealikuwa anafaa sana katika kuongoza vita vile kuliko Abdul Sykes.

Hamza alimtaka Abdul amsaidie Nyerere kuchukua uongozi kwani kwa siasa za Dar es Salaam za wakati ule ikiwa Abdul atagombea urais wa TAA dhidi ya Nyerere kwa nia ya kupata ushindi, Nyerere asingeweza kumshinda Abdul hata kidogo kwani chama chenyewe kilikuwa kinaishi ndani ya nyumba ya akina Sykes kuanzia mwaka wa 1929 baba yake Abdul alipokuwa Katibu muasisi wa African Association na 1950 Abdul alipoingia katika uongozi wa TAA baada ya kifo cha baba yake 1949.

Lakini kubwa ambacho Hamza alimweleza Abdul ni kuwa yeye Abdul ni Muislam na ikiwa ataongoza harakati za uhuru Waingereza watachukulia hilo kama vurugu zingine za Waislam dhidi ya serikali lakini Nyerere kama Mkristo Waingereza hawatokuwa na hofu kubwa.

Ikiwa historia ya TANU itaandikwa bila kuwataja Hamza Mwapachu na Abdul Sykes mengi sana katika historia ya Nyerere yatapotea na kwa hakika historia yenyewe ya TANU.

Sasa unaweza kusoma kuhusu uchaguzi ule wa mwaka wa 1953 kati ya Abdulwahid Kleist Sykes na Julius Kambarage Nyerere uliofanyika Ukumbi wa Arnautoglo tarehe 17 April 1953 hapo chini:


Ukumbi wa Arnautoglo safari ndefu ya Mwalimu Nyerere ilipoanzia - JamiiForums
UKUMBI WA ARNAUTOGLO SAFARI NDEFU YA MWALIMU NYERERE ILIPOANZIA George Arnautoglo alikuwa Mgiriki tajiri na ndiye aliyejenga jumba hilo akalitoa kwa matumizi ya Waafrika wa Tanganyika. George Arnautoglo alikuwa hawapendi Waingereza kwa kuwa walikuwa wameikalia nchi yake Greece ambako Padri...
www.jamiiforums.com
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…