Udhaifu wa mabondia waongeaji

BETONY

Senior Member
Joined
Apr 4, 2012
Posts
188
Reaction score
170
Ni ukweli usiopingika kuwa kwa bondia yeyote anatakiwa mdomo kuwa nao ili kuweka hofu kwa mpinzani wake.

Hakika mdomo ni sehemu ya mchezo wowote katika kumtisha mpinzani. Leo nataka kuwazunguamzia mabondia wawili wanaoshabiiana kwa ukaribu. Mabondia wenyewe ni Dulla Pazi (Almaharufu Dulla Mbabe) na Deontway Wilder. Hawa ni mabondia wanaojua kuongea sana na kumpandisha mpinzani uogo.

Ukiangalia kwa ukaribu mabondia hawa wawili ulingoni huwa wanakutana na wakati mgumu sana. Tukiangalia michezo yao miwili iliyopita tunajifunza yafuatayo.

Mosi, wote ni mabondia wazungumzaji wazuri, lakini kile wanachozungumza mara nyingi hakionekana ulingoni. Ukiangalia mahojiano yao kabla ya kukutana na wapinzani wao na kwa kuangalia yale wayasemayo unaweza kuzani kuwa wanaweza kuua mtu ndani ya ulingo. Wote wawili wamewekeza kwenye maneno na si matendo.

Pili ukiangalia wote wawili ni watu wanotegemea mpigo wa aina moja (sucker punch) yaani wawavizie wapinzani wao kwa ngumi moja nzito na kuwakalisha. Aina hii ya mapigano imekuwa ndio silaha yao, japo sasa inawagharimu hasa wakikutana na wapinzani wanaoweza kukimbia na kuwa na mnyumbulisho.

Tatu wote si wazuri katika mijongeo ya miguu wawapo uwanjani. Hii upelekea kuchoka kadri mda unavyoyoyoma kwa kukutana na mpinzani mzuri. Ni ukweli usiopingika kuwa makocha wao wanatakiwa kufanyiankazi udhaifu wao huo.

Nne, wote ni wachovu kadri mda unavyokwenda na wanaanzaga kwa kasi kwa nia ile ya kurusha konde moja chali. Mbinu hii ya mapigano alikuwa anaiweza mtoto wa kiswahili MIke Iron Tyson. Mike Tyson yey alikuwa anakuja na lengo moja tu la kuhakikisha mpinzani wake anamkarisha kabla ya raundi ya tatu.

Sasa ukiwangalia Dulla Pazi na Wilder wanakuwa nao na lengo hilo, lakini si wazuri kwa kumaliza mchezo mapema kwani hawana kasi ya kurusha makonde kama ilivyokuwa kwa Tyson.

Tano na mwisho mabondia wote wawili ni wazuri wakiamuu kupeleka yale wanayongea kwenye mazoezi na kuhakikisha kuwa wanakuwa na uwezo wa kucheza raundi zote za mpambano na si kuja ulingoni na jukumu la kuua mpinzani tu.

Tchaoo

Sent from my SM-G955U using JamiiForums mobile app
 
Mohammed Ali alikua muongeaji wa majigambo kifasihi plus trash to.indimidate opponent wake tu na kucheza na saikoloji but kazi aliijua na akiingia ulingoni alijua anataka nini.

Jana Aldallah Pazi alipgigwa ngumi akatema udenda aka uji huku akiyumayumba hiyo ni hatari sana kwa bondia.

Sent from my SM-G9350 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…