Udhalilishaji: Video ya PNC akimuomba msamaha Ostaz Juma na Musoma

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Joined
Dec 11, 2012
Posts
6,067
Reaction score
10,938
PNC AKIMWOMBA MSAMAHA USTAZ JUMA - YouTube

Mimi kama mdau wa muziki wa kizazi kipya napinga na kulaani huu udhalilishaji wanaofanyiwa wasanii wetu.

Nimestushwa kuona hii video inayosambaa kwenye social network ambayo member wa zamani wa kundi la Watanashati PNC akiwa amempigia magoti don wa kundi hilo Ostaz Juma Namusoma huku akimwomba msamaha.

Hakika hii video inaondoa thamani ya wasanii wetu na kuonesha kuwa bila hao wanyonyaji wanaojiita mameneja wa wasanii basi muziki sio kitu.

Na nyie wasanii muwe na msimamo thabiti na sio kuhama hama makundi kama malaya na ndiyo maana mnaishia kudhalilishwa kwa ujinga wenu.

Na ninyi madon wa muziki acheni kudhalilisha wasanii,kwa kuwanyonya inatosha tu na sio kuanza kuwaanika kwenye mitandao mambo wanayofanya.Mimi sijafurahishwa kabisa na hii video.

Narudia tena; Nalaani vikali huu udhalilishaji kwa wasanii.

 

Attachments

  • 2112.jpg
    36.8 KB · Views: 24,451
Last edited by a moderator:
Kaz ipo...hata mimi sikupenda hata kidogo...kwanini kafanya hivi jamani?kweli tatizo ni bei ya mkaa
 
ustaz juma ndio nani, anahusika na nini na muziki na wanasanii...?

Mkuu, Ostaz Juma Namusoma ni mdau wa muziki hapa nchi na ndo anawamiliki wasanii walio chini ya lebo ya watanashati.Anapenda kuimbwa sana na wasanii.
 
Yaani imebidi nianze kucheka kwanza kabla ya kusikitika poor pnc na hao aliowaombea msamaha na yeye mwenyewe tatizo ni kutojiamini tu kwamba unaweza mbona wenzake akina kassim mganga walijitoa kwa hao mabosi wao na still wanafanya poa what matters ni kufanya nyimbo zinazopendwa na kukubalika.
 
Elimu ndogo ndio inayosababisha yote hayo, ina maana huyo ustadh akifa ndio utakuwa mwisho wa maisha ya hicho kitoto pnc? Nawachukia sana watu wanaopenda kuegemea sehemu.
 
Sura mbaya kama Ostadhi Juma wa Musoma,"mi sipigi magoti wala nini ana sura mbayaa kweli
 
PNC pimbi tu hana akili hata kidogo yaan hawa wasanii ambao shule zero kama hiyo kenge PNC ndo lazma asujudu kinyume na hapo hana akili nyingine nilijinga na meno yake ka ngurue
 
Hv munamuona pnc ana akili timamu?jamaa mwehu huyo
 
Nijuavyo mimi ni kuwa mtu huomba msamaha baada ya kukosea, na mleta uzi hajatuambia kosa la pnc ni nini....so mtu unavyochangia tu kwa kumshutumu ostaz/ustaadhi Juma sidhani kama ni sahihi sana.

Inabidi tujue kuwa pia hawa wanaowekeza kwa wasanii wana michango yao kuifikisha game hapa ilipo.....na msidhani kudili na wasanii ni jambo rahisi....inataka moyo, mapenzi na kujitolea sana wandugu....

Hebu muwaulize kina Fela, babu Tale na wengine.

Juzi juzi tu tumesikia jinsi Mr Nice alivyoshindwana na aliyetaka kumsimamia pale Kenya....pia tumesikia Mb Dog alivyorudi kwa babu Tale.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…