Likasu
JF-Expert Member
- Jan 18, 2011
- 855
- 438
Nianze kusema kuwa mimi sina utaalam wa mambo ya sheria. Siku hizi kumezuka mtindo wa mahakama zetu kumdhamini mtuhumiwa mahakani eti ni mpaka aje mdhamini ambaye ni mfanyakazi wa serikali. Huwa najiuliza maswali kadhaa. Hivi raia hawezi tambulika mahakamani mpaka awe serikalini ? Wafanyakazi wa serikali wapo wangapi kutosha kudhamini watuhumiwa mahakani ? Serikali zetu za mitaa ambazo hutoa uthibitisho wa mkazi wake mahakamani haziaminiki tena na mahakama zetu ? Naomba wataalam wa sheria mtujuze kuhusu haki ya kumdhamini mtuhumiwa mahakani.