hiyo inatokana na uzoefu, wameshawapokea wadhamini wengi ambao si wafanyakazi, address yao haijulikani vizuri, washitakiwa wengi wakawa wanalala mbele, ikabidi mahakama waangalie njia nyingine. chukulia mfano, mtu ameiba gari yako wewe hiyo unayoendesha kama unayo, anakuja mahakamani, kosa hili ni bailable, anapata dhamana kwa mtu asiye na address ya kueleweka, analala mbele na kesi inaharibikia hapohapo kwasababu unaweza kukesha miaka kadhaa bila kumkamata, utajisikiaje? mahakama nafikiri wamefanya hivyo ili kulinda maslahi pia ya victim aliyetendewa kosa, usiangalie tu upande wa mshitakiwa, angalia na kwa muathirika aliyedhurika na kosa lililotendeka.