Salaam wanajamvi!! Naomba tuchangie mawazo katika hili:
Kumekuwa na hii dhana kuwa namna ya kuwasaidia wakulima ni kuhakikisha wanauza mazao yao kwa bei ya juu miongoni mwa namna zingine.
Nionavyo mimi hii inaweza kuwa njia nzuri kwa mazao yale ya biashara lakini sio kwa mazao ya chakula.
Kwa nchi kama yetu nadhani inabidi mamlaka zihakikishe wanachi wake wanapata chakula kwa gharama za chini sana.Hii inapunguza ugumu wa maisha, inapunguza utapia mulo hasa kwa watoto,akili inakuwa vizuri, watu wanakuwa na nguvu za kuzalisha mali na familia zinastawi kisha taifa linapata kuendelea. Njaa inaathiri akili na ufanisi kwenye uzalishaji.
Wakulima wa mazao haya wawezeshwe kupata huduma kwa gharama nafuu sana, ikiwezekana bure.Wapate huduma za msingi kama Eilimu, afya, umeme,maji n.k bure.Ulinzi uimarishwe vijijini, barabara zielekezwe huko,shule na vituo vya afya pamoja na hospitali viongezwe,masoko yawepo, vifaa vya ujenzi wa nyumba vipatikane kwa bei nafuu sana n.k.Pembejeo pia zipatikane kwa gharama za chini.
Kodi ya mapato iongezwe kwa wafanyakazi na wafanya biashara, mishahara ya wafanyajazi ipunguzwe pamoja na posho za viongozi wakuu,Mamlaka za mapato zikusanye kodi kwa umakini mkubwa ( TRA&Halmashauri), tutasonga mbele na mabadiliko tutshuhudia.
Kwa muda sasa kumekuwa na bei za juu sana za chakula kutoka kwa wafanya biashara hata kama ni msimu wa mavuno na kusababisha ugumu wa maisha. Pia kuiwe na mamlaka itakayokuwa inaweka bei elekezi kama ilivyokuwa EWURA kwa sekta ya nishati na maji.
Nakaribisha mawazo yenu!!