SoC01 Udhibiti wa posa chafu kwa Wanawake

SoC01 Udhibiti wa posa chafu kwa Wanawake

Stories of Change - 2021 Competition

Ally MO98

Member
Joined
Mar 23, 2021
Posts
19
Reaction score
22
Posa ni kitu chenye thamani ambacho hutolewa katika familia ya mwanamke na kundi la watu wenye lengo la kuthibitisha uwepo wa ndoa kutoka kwa mwanaume.

Katika karne hii ya 21, kundi la wazandiki wa kindoa hutumia mwanya huo kutokana na sababu za wanawake wenye msimamo kutokukubali kuingiliwa kimwili bila utambulisho wowote kutoka kwa wanaume wenye ahadi za kutaka kuwaoa na kua wake zao, hivyo kutokana na uchu wa kingono ndipo wanatafutwa washenga uchwara kwaajili ya kuiendea familia ile ya mwanamke kwa kutoa posa ili kuzidi kuiteka mioyo ya Mama/Dada zetu na kuwaaminisha ya kwamba wako pamoja nao na lengo la kuwaoa lipo, kitendo hicho ndio hupelekea mwanamke kuvunja misimamo yote aliyoiweka akiamini kua anakutana kimwili na mume wake mtarajiwa.

Kwa masikitiko makubwa na fedheha katika jamii mwanamke anaachwa akiwa haelewi na hatambui sababu yeyote iliyomfanya amkose mwanaume anaeaminika atamsitiri hapa duniani na kua wake katika maisha yake ya ndoa.

->MADHARA

1. Msongo wa mawazo

Msongo wa mawazo ni mfadhaiko wa akili anaoupata mtu kutokana na shida, taabu, dhiki, matatizo au changamoto zinazomkabili katika maisha ya kila siku hivyo moja ya madhara ya vitendo hivi kwa mwanamke ni kumpatia mawazo lukuki yatakayo mpa matatizo zaidi .

2. Kukata tamaa ya maisha
Ni hali ya mtu kupoteza matumaini baada ya kushindwa kupata njia ambayo ingeweza kumfanya atatue au ajitoe katika matatizo au changamoto inayomkabili.

3. Kifo
Ni kitendo cha nafsi kutengana na mwili na kupelekea utendaji wa mwili kusimama kabisa.


Nimeelezea madhara wapatayo wanawake wenye kuumizwa kwa njia hiyo hivyo ni jukumu la serikali na wananchi wote kushiriki kwa pamoja katika kulaani vitendo hivi vya kikatili kwa mwanamke ili kuweza kukomesha kabisa tabia hii chafu.

->VIDHIBITI

1. Kitambulisho
Serikali kupitia taasisi za kidini zinazohusiana na maswala yote ya ndoa, zishirki kwa pamoja katika kukusanya taarifa za raia wake walio katika mahusiano waweze kuingia katika data base za utambulisho wa ndoa kitaifa na kuzingatia pia usalama wa raia wake hii itapelekea uwazi wa mambo baina ya mwanamke na mwanaume.

2. Mshenga
Ni miongoni mwa msuka mipango ya kindoa na mtu wa hatua ya kwanza kabisa katika upatanishi wa familia mbili kuweza kuungan na kua wamoja pia hutumika katika usuruhishi wa matatizo na migogoro ya kindoa hivyo basi ni vizuri watu hawa wenye nia nzuri katika upatanishi wakawa na usajili ulio wazi na wenye kutambulika bila shaka hii itaokoa washenga uchwara wanaojitokeza kama nilivyoeleza hapo juu.

3. Elimu ya jinsia
Ni muhimu sana kwa sasa wazazi na walezi kutoa elimu bila uoga maswala yote ya kijinsia hii itampa uwezo mwanamke kutambua thamani yake na utu wa mwanamke, halkadharika elimu hii isambae mashuleni na sehemu mbalimbali kwenye jamii zetu kwa mabinti wote waliopevuka kiakili ili namba ya uelewa wa mwanamke uongezeke.


Hili ni jukumu letu sote kufundishana na kuachana kuendekeza ngono zembe na kuepuka utesi kwa wanawake wote nchini, kura yako ni muhimu kunipigia ili kutumia fursa zaidi kwa kufikisha elimu kwa jamii.

Asante kwa kusoma mpaka mwisho.


Ally MO98
+255625981281
Dar-es salaam
 
Upvote 5
Duh kuwe na masijala ya watu wenye mahusiano!
 
Kwahiyo washenga warasimishwe kama madalali?[emoji276]
Ni bora tuwatambue kama washenga kamili na waliopitia mafunzo na wakifunzu watunukiwe cheti cha ushenga hodari kwani kwa kufanya hivyo itasaidia kupunguza au kukomesha uhatari wa michezo michafu kwa wanawake.
 
Back
Top Bottom