kanga
JF-Expert Member
- Jan 13, 2011
- 1,025
- 494
Jaji Mkuu wa Tanzania, Mohamed Othman Chande, amesema kuwa mahakama imeelemewa na mzigo wa kesi kutokana na uhaba wa majaji na mahakimu.
Amesema kuwa mahakama inakabiliwa na changamoto ya watumishi hali inayosababisha kasi ya kumaliza kesi kuwa ndogo.
Jaji Chande alisema idadi ya majaji waliopo bado ni ndogo na haikidhi mahitaji ya mashauri yaliyopo mahakamani.
Akizungumza jana katika maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini, jijini Dar es Salaam, Jaji Mkuu alisema kwamba katika majaji 65 wa Mahakama Kuu, kila mmoja anahudumia Watanzania 560,000, hali ambayo alisema kuwa inaonyesha bado
mahakama inaelemewa na kasi ya kumaliza kesi.
Hata hivyo, Jaji Chande alisema kutokana na mikoa 12 kutokuwa na Mahakama Kuu na ongezeko la watu kuwa kubwa katika mkoa wa Dar es Salaam, mahakama inakusudia kuigawa Kanda ya Dar es Salaam katika kanda tatu za Ilala, Temeke na Kinondoni.Source
source: Nipashe/7/2013
My Take.
Mahakama nchini bado zina utendaji wa kazi wa kijima sana na urasmi uliotawaliwa na rushwa.Pia jambo lingine ni kule kutegemea kufanya kazi kwa kutegemea posho za vikao au sitting allowance kwa majaji.Hivi kwa nini Majaji waendelee kufanya kazi kwa kutegemea posho wakati wanafanya kazi zao za kawaida zenye marupurupu mazuri na mafao bora zaidi?.
Pia muundo mbovu wa mahakama unahitaji ubadilishwe ili kupunguza urasmi na rushwa ilikomaa ndani ya taasisi hii muhimu.
Mahakama za mwanzo na mkazi/Wilaya zisimamiwe na Serikali za mitaa na kuwajibika kwa Halmshauri moja kwa moja na Mahakama kuu,rufaa zibaki kwenye serikali kuu kama vyombo vya rufaa na makosa maalum.
Hii itapunguza urasmi na rushwa.Katika tafiti za sasa mahakama na polisi ndizo zinashindania namba ya kul rushwa wakati serikali za mitaa na Halmashauri rushwa ni kidogo sana.
Jaji mkuu kulalama kote huko hata akipewa majaji na mahakimu wa kumwaga tatizo halitakwisha maana ni nature ya utendai kazi wa taasisi katika kutafuta kuneemeka na rushwa, Dawa ni kuunda upya mfumo mahakama za chini ziwajibike na zisimamiwe na Halmashauri moja kwa moja.