Jerry Farms
JF-Expert Member
- Jul 18, 2022
- 202
- 167
Idadi ya wazee Tanzania
Kwa mujibu wa sensa ya 2022 Tanzania ina jumla ya wazee 7,469,714 chini ya mgawanyo wa wazee 7,294,654 Tanzania bara na 175,060 Tanzania Zanzibar,( Ripoti ya Mgawanyo wa Idadi ya watu kwa Umri na Jinsi Tanzania,2022,Wizara ya Fedha na Mipango).
Jedwari: Mgawanyo wa wazee Tanzania
Chanzo: Ripoti ya Mgawanyo wa Idadi ya watu kwa Umri na Jinsi, Tanzania,2022,Wizara ya Fedha na Mipango.
Hali ya Ukatili kwa WazeeKwa mujibu wa sensa ya 2022 Tanzania ina jumla ya wazee 7,469,714 chini ya mgawanyo wa wazee 7,294,654 Tanzania bara na 175,060 Tanzania Zanzibar,( Ripoti ya Mgawanyo wa Idadi ya watu kwa Umri na Jinsi Tanzania,2022,Wizara ya Fedha na Mipango).
Jedwari: Mgawanyo wa wazee Tanzania
Chanzo: Ripoti ya Mgawanyo wa Idadi ya watu kwa Umri na Jinsi, Tanzania,2022,Wizara ya Fedha na Mipango.
Changamoto ya ukatili kwa wazee ni suala mtambuka katika jamii. Licha ya jitihada mbalimbali kufanywa na serikali na wadau wengine wa maendeleo, wazee wameendelea kukumbwa na changamoto ya ukatili, vitendo kama ukatili wa kuhisia, unyanyaswaji, kutengwa, kupigwa na mauaji kwa imani za kishirikina vikijumuishwa kwa pamoja.
Picha: Baadhi ya mambo yanayoashiria ukatili kwa wazee
Chanzo:Jamii forums
Mnamo mwaka 2020 kulikua na jumla ya matukio 54 ya mauaji ya wazee, mauaji yakitekelezwa na wanajamii, watu wasiojulikana na ndugu wa karibu wa wazee, mfano mauaji ya 2022 ya mzee Bi.Agness Msengi, Windila Saidi na Winifrida Gigila, maeneo ya Kisharita -Singida,(Gazeti la Mwananchi,Juni 10,2022).
Chati: Matukio ya mauaji yaliyotokana na imani za Kishirikina 2015-2020.
Chanzo: Muhtasari Ripoti ya Haki za Binadamu Tanzania,2021,LRHC.
Mnamo mwaka 2021 kulikua na jumla ya mauaji ya wazee 36, visa vikiwa vimekusanywa na LHRC katika mikoa ya Dodoma, Kagera, Mbeya, Arusha, Katavi, Tabora, Songwe, Njombe, Kigoma, Rukwa, Shinyanga na Manyara,( Muhtasari Ripoti ya Haki za Binadamu Tanzania,2021,LHRC). Ukatili kwa wazee pia ulijumuisha matukio 16 ya ukatili wa kimwili,kingono na utekelezaji.
Mnamo mwaka 2022 kuriripotiwa ongezeko la ukatili kwa wazee hasa hasa maeneo ya vijijini. Matukio 24 ya ukatili yakihusisha ubakaji, vipigo,mauaji 8 na mengineyo, (Muhtasari Ripoti ya Haki za Binadamu Tanzania,2022,LHRC).
Pamoja na jitihada za uanzishwaji wa mabaraza ya wazee,utoaji elimu, uboreshaji huduma za afya kwa wazee na ujenzi wa vituo vya kulelea wazee changamoto ya UKATILI KWA WAZEE bado ipo katika jamii. Hivyo katika andiko hili tutaangazia baadhi ya njia, kupambana na changamoto hii.
Serikali haina budi kuendelea na mapambano, jitihada zikielekezwa katika uangalizi wa usambazajwi wa taarifa hasi juu ya kundi la wazee katika jamii. Nguvu kubwa imeelekezwa katika Elimu, kupambana na waganga na wapiga ramli chonganishi, mila potofu nakadharika huku wigo wa upashanaji habari ukiachwa. Jitihada madhubuti hazina budi kuanzishwa kuangalia aina ya taarifa jamii inayolishwa ikililenga kundi la wazee.
Taarifa hasi katika jamiiPicha: Baadhi ya mambo yanayoashiria ukatili kwa wazee

Taarifa ni mojawapo ya nyenzo muhimu katika ustawi wa jamii, taarifa huathiri makuzi, mienendo na utendaji wa wanajamii. Pamoja na jitihada kubwa kurahisisha upashanaji wa taarifa, jamii imekua ikilishwa taarifa hasi hivyo kupelekea changamoto ya chuki na ukatili kwa kundi la wazee. Taarifa hasi hizi husambazwa kwa kujua ama kwa kutokujua hivyo kuathiri jamii. Wafuatao ni baadhi ya wasambazaji wa taarifa hasi katika jamii( kwa kujua/kutojua) hivyo kujenga taswira hasi ya kundi la wazee katika jamii.
Dini(taarifa hasi katika nyumba za ibada)
Taarifa hasi kupitia taasisi hizi huangukia katika hotuba/mahubiri na mawaidha. Zoea la uhusishaji wa wazee kujengewa taswira ya watu wenye tabia mbaya( wachawi) limezoeleka kutolewa katika shuhuda za uponyaji za waumini. Utoaji wa shuhuda hizi katika hadhira hujenga taswira ya kuogopwa kwa kundi la wazee nnje ya nyumba za ibada(wasiosali/swari).
Watoto wadogo, vijana na watu wazima kuwa na zoea la kuskiliza aina hizi za shuhuda huathiriwa kisaikolojia taratiibu na kuanza kujenga taswira ya wazee kuwa ni watu wasiofaa katika jamii. Mfano, shuhuda ielezeayo mjukuu aliekua akiishi na babu/bibi yake nakufanya vitendo vya uchawi huwaathiri wasikikizaji taratiibu na kujenga taswira mbaya kwa kundi tajwa hivyo ukatili na unyanyapaa.
Wasanii kupitia kazi zao za sanaa.
•Tamthiliya na MaigizoWatoto wadogo, vijana na watu wazima kuwa na zoea la kuskiliza aina hizi za shuhuda huathiriwa kisaikolojia taratiibu na kuanza kujenga taswira ya wazee kuwa ni watu wasiofaa katika jamii. Mfano, shuhuda ielezeayo mjukuu aliekua akiishi na babu/bibi yake nakufanya vitendo vya uchawi huwaathiri wasikikizaji taratiibu na kujenga taswira mbaya kwa kundi tajwa hivyo ukatili na unyanyapaa.
Wasanii kupitia kazi zao za sanaa.
Uhusishaji wa wazee katika baadhi ya kazi za sanaa umekua ukiwajengea picha mbaya kwa umma. Wazee katika baadhi ya maigizo( "Bongomuvi") wanachezeshwa na kuvalishwa uhusika wa watu wenye roho mbaya na uchawi. Hii si sawa kwa afya ya watazamaji, mkazo mkubwa kusimamia maadili umewekwa kutazama maudhui ya udhalilishaji wa kimaadili( picha chafu, lugha na mavazi yasiyo ya staha) na si kuangalia uhusishaji wa waigizaji.
•Tungo za hadithi na Riwaya
Tungo nyingi zihusishazo visa vya kutisha mfano uchawi, wahusika katika tungo hizi wamefanywa kuwa ni wazee. Uhasi huu wa masimulizi ukizoewa na msomaji moja kwa moja humuathiri jinsi atakavyo kuwa na mtazamo juu ya wazee. Taarifa anayojazwa mtu inamchango mkubwa katika kufikiri na kufanya kwake maaumuzi.
Vyombo vya habari( redio, runinga, magazeti na mitandao ya kijamii)
Hivi navyo kwa kiasi fulani zinachangia usambazaji wa taarifa hasi zinazolenga kundi la wazee. Aghalabu masimulizi ya mikasa ya maisha ya wageni wanaoalikwa kutoa simulizi zao. Kwa wasimuliaji(baadhi) wamekua na kasumba ya kulimulika kundi la wazee na kulisemea sifa mbaya ambazo moja kwa moja humuathiri msimuliwaji mfano kutaja wazee kama watu waliowapa nuksi katika safari zao za maisha.
Muhimu: Mkazo wa serikali katika utoaji wa elimu alhali ikiacha uenezwaji wa taarifa hasi ukiendelea ni sawa na kufanya juhudi bure. Elimu dhidi ya ukatili wa wazee haina budi kuendana na vita dhidi ya taarifa hasi katika jamii.
Chanzo: ZanziNews
Mapendekezo ya utatuzi wa usambazwaji wa taarifa hasi katika jamii
Uwepo wa taarifa hasi huleta ukinzani katika kuielimisha jamii, kufanikisha ufikishaji wa Elimu kwa jamii serikali haina budi kufanya yafuatayo ili kuzuia usambazaji kwanza wa taarifa hasi.
•Kazi za wasanii kusimamiwa na kuondolewa kwa maudhui chochezi.
Ushiriki wa wazee katika tamthiliya upewe mkazo kuonesha wazee wenye vitendo safi katika jamii. Wazee wasipewe uhusika wa watu wenye tabia mbaya katika uigizaji mfano roho mbaya ama uchawi. Kama itarazimu wao kuigiza sifa hizo basi mwisho wa igizo ufafanuzi utolewe kwa mtazamaji lengo likiwa kuwafumbua macho/fikra watazamaji wasijekuondoka na mtazamo hasi.
Hadithi zenye visa vyenye utata mfano uchawi visiandikwe zikilenga moja kwa moja kundi la wazee, hii itasaidia kujenga mtazamo chanya kwa kundi hili. Hapa tutoe heko kwa serikali kuondoa hadithi katika vitabu vya kiswahili shule ya Msingi zilizokua na mlengo wa kuonesha wazee kuwa na tabia za ulozi. Mfano, hadithi ya Watoto waliogeuka mawe, japo hadithi ililenga kujenga maadili lakini inaonesha bibi kizee kuwa na tabia ya ulozi.
•Semina elekezi kwa viongozi wa madhehebu namna ya uwasilishaji wa maudhui yao kwa waamini/waumini na jinsi ya kuwasimamia waumini wao.
Shuhuda za uponywaji na visa vya kurogwa zisilenge kuwahusisha moja kwa moja wazee, viongozi wakemee hili. Sio lazima kuhusisha kundi la wazee na urozi, itafutwe namna nzuri ya uwasilishwaji wa shuhuda na mahubiri yasiyolenga kueneza taarifa hasi kwa wasikilizaji. Vitendo ovu vikemewe na kukosolewa pasipo kulenga kundi moja la watu katika jamii.
•Maudhui chonganishi yafanyiwe uhariri kabla ya kurushwa kwa hadhira.
Katika masimulizi yenye urazima wakutaja kundi la watu fulani katika jamii( wazee) patumiwe neno la jumla. Mfano msimuliaji anaweza sema," nilipofika sehemu ANC....nikakutana na mchawi, akaniambia ABCD..." na sio kuingia moja kwa moja na kusema," nilipofika ABC nikakutana na bibi/babu mchawi akanipa...." Kwa vyombo vitakavyokiuka vipewe onyo na adhabu. Imezoeleka maonyo na adhabu kutolewa kwa kurusha nyimbo zenye tungo tata, picha chafu, lugha za kuudhi nakadharika sasa tuhamie na katika usemwaji wa kundi la wazee.
HITIMISHOVyombo vya habari( redio, runinga, magazeti na mitandao ya kijamii)

Taarifa ni kitu chenye matokeo makubwa katika kumjenga mtu, taarifa anazolishwa mtu humjengea muenendo wake, maamuzi na utendaji wake katika jamii. Mtoto akilishwa taarifa mbaya juu ya kundi la wazee ataamini na kuishi na dhana hio kichwani vivyo hivyo mtu mzima akizoeshwa kuona maudhui yanayochafua kundi fulani la watu basi ataishi na imani hio.
Upashanaji wa taarifa hasi katika jamii hauna budi kupigwa vita kwa hali na mali, shime kwa wizara husika kuangalia kwa ukaribu aina ya taarifa na upashanaji wetu wa taarifa katika jamii.
Chanzo: Dar24
Wazee ni tunu, waheshimiwe na kupatiwa hadhi wanayostahili katika jamii. Tanzania tuitakayo ni ile isiyo na matabaka na ubaguzi kwa misingi yoyote ile. Ni rai yangu kwa serikali na jamii kwa ujumla kuachana na kasumba ya uzee ni mzigo na uzee ni kitu kibaya, taarifa hasi si afya kwa jamii. Jamii ijivunie wazee na ikumbukwe kila mtu ni mzee wa kesho ijayo.

Upvote
4