Bichwa ndani ya dryer
Member
- Sep 22, 2026
- 64
- 124
- Thread starter
-
- #21
Walichomeshwa na hila za wamagharibi kwani alishaleta tishio kuunganisha Africa kuwa na sarafu yake ambapo ingewezekana ingekuwa pigo Kwa mabeberu ,Mbona raia wa Libya walichukua silaha kupinga utawala wa Gadaffi?...
Wote Wanaoleta tafiti zao wanazifanyia ndani ya jukwaa la JF? Au ugeni wangu unahusiana vipi bossMkuu huna hata wiki humu jukwaani lakini umeshafanya na utafiti?? Au mlisaidiana na bichwa mwenzio BICHWA KOMWE - huo utafiti?
Afrika tatizo sio mfumo. Akili zetu bado ziko kwenye "hunting and gathering".Tabia za wa afrika, hata mfumo utoke mbinguni, rushwa,uchawa, unafiki,ufisadi uko pale pale
Mkuu hoja yako ya kwanza Ina nguvu ila ni general mno hujazingatia athari ya vita vya wenyewe Kwa wenyewe na uingilwaji kijeshi na NATO.Hii hoja yako ina madhaifu matatu makubwa
La kwanza Kuhusu Gadafi na uchumi wa Libya:*
Libya ilionekana tajiri sio kwa sababu ya Gadafi kuwa mchumi mzuri, bali kwa sababu ya MAFUTA. Pesa ya mafuta iligawanywa kidogo kwa wananchi ili wasihoji udikteta wake. Sarafu ilikuwa na nguvu kwa sababu aliifunga kwa akiba ya dhahabu na mafuta, sio kwa viwanda. Na huo ndio ulioiangusha - alipokufa system nzima iliporomoka kwa sababu hakujenga taasisi, alijenga utawala wa mtu mmoja. Nchi tajiri kweli haianguki inchi nzima siku kiongozi mmoja akifa.
Pili hili neno "Akiiba analeta ndani hakuna ubaya":*
Hapa ndipo unajichanganya mwenyewe. Ulisema hawa wetu wanaiba ndani na kupeleka Uswizi sio haki. Sasa Idi Amin kuiba Kagera na Trump kutaka mafuta ya Iran ni sawa na kuiba ndani na kupeleka Uswizi - ni wizi tu. Tofauti ni mmoja anaiba kwa jirani, mwingine anaiba kwa wananchi wake. Zote mbili ni wizi. Huwezi kusema wizi wa nje ni halali na wa ndani sio halali. Wizi ni wizi.
Kagera ya Idi Amin haikuwa faida, ilileta vita tukapoteza maelfu ya Watanzania na Waganda, uchumi ukaanguka mpaka leo tunalipa madeni ya vita hivyo. Faida gani?
Tatu Traore sio Gadafi:
Gadafi alikaa madarakani miaka 42 bila uchaguzi, akaua wapinzani, mwisho aliuawa na wananchi wake mitaani. Kama Traore anapita njia hiyo hiyo ya kukaa kwa bunduki bila taasisi, mwisho wake utakuwa ule ule, sio maendeleo ya kudumu.
Maendeleo ya kweli si sarafu iliyolazimishwa kuwa juu leo na kesho inakuwa karatasi, ni taasisi zinazobaki hata kiongozi akienda.
Mkuu hoja yako ya kwanza Ina nguvu ila ni general mno hujazingatia athari ya vita vya wenyewe Kwa wenyewe na uingilwaji kijeshi na NATO.
Kwahyo tatizo la Gadafi kutokuwa na taasisi halina mashiko Bali hakukuwa na mtu aliendaliwa kuendleza kma ilivyo kwa nchi za falme za ghuba ambao wanautaratibu wa mpito akifa mfalme
Rudi kwenye I'd yako Ile Ile acha maujingaWalichomeshwa na hila za wamagharibi kwani alishaleta tishio kuunganisha Africa kuwa na sarafu yake ambapo ingewezekana ingekuwa pigo Kwa mabeberu ,
ndio mana mpka Leo majuto na hatia hiyo inawala na wanakiri hilo
Wote Wanaoleta tafiti zao wanazifanyia ndani ya jukwaa la JF? Au ugeni wangu unahusiana vipi boss
Bichwa lake lipo kwenye dryer.Akili za matakoni hizi,mbona hutaji mifano ya Uganda,Congo,Rwanda,Burundi,Niger,Bolivia n.k.
Unatetea upumbavu
Taja nchi zote za kidkteta na nchi zote za kidemokrasia,linganisha maendeleo ndiyo urudi hapa kuandika maoni yako upya.Sawa kwenye msafara wa kenge mamba Nao wamo ni sawa Kuna nchi mfano Bolivia ulioitaja ambyo walioingia kidikteta walikuwa na motive ya kuuza madawa ya kulevya ila kwa Uganda nduli Amin alikuwa anarekebesha na kujenga nchi Kwa kutumia wa asia waliokuwa wanamiliki ardhi ya waganda akaonekana mbaya alikuwa anataka kuongeza mpka Kagera akaonekana mbaya lakini kujiangalia hapo alikuwa anatanguliza maslay ya Uganda hata Kwa mauaji aliyoyafanya ya wanasiasa alikuwa hataki kuingiliwa na kuruhusu Kila mtu kubwabwaja kma ambavyo Huwezi kumwacha mke wako ajiamulie amulie mambo ,
Hata tukija Kwa Gadafi ,Adolf Hilter na saivi huyu traore anapigwa vita ni kma ukiwa dikteta unatishia ulaji wa mgharibi ndo mana analetewa visa
Watu hawana akili kabisa yaaniBichwa lake lipo kwenye dryer.
Nasikia dryer huwa zinawaathiri sana wanawake.
Wewe nchi yako ina utawala gani demoracy au dictator ship, na je haya madhara yapo au hayapo?Kwa utafiti mdogo nilioufanya UTAWALA wa kidemokrasia ni utapeli tu na mtego ambao nchi nyingi za kiafrika zimejiingiza kingi bila kujua ,naamini udikteta NDIO mfumo Bora wa kutongoza nchi kwasababu dikteta anakuwa msemaji wa mwisho katika maswala ya nchi bila kuingiliwa na makuburu na walowezi weupe ,
Anauwezo wa kuvunja sheria ambazo anaona hazina maslai Kwa Taifa mfano mikataba ya kilaghai na unyonyaji
Nchi kama China, Korea kaskazini,Irani,na urusi ni mfano Bora wa nchi zenye udikteta mkubwa lakini viongozi wake wamevaa vazi la uraisi ili kujiepusha jina la udikteta ambalo kimsingi sidhani kama ni baya .ila wamesimama wima kama rula wawaruhusu ujinga ujinga na upuuzi unaoendlea kwenye inchi zinazojiita za kidemokrasia mfano hawalei ushoga, na matumizi ya dawa za kulevya ,mikataba ya kijinga kijinga kama nchi za kidemokrasia
Kwenye nchi za kidemokrasia matendo ya rushwa, uchawa na wizi wa mali za umma ,matabaka na kujibinafsisha mali za umma ,undugu katika kupeana vyeo na unafiki yamekithiri sana