KERO UDOM kuna changamoto ya baadhi ya Wanafunzi wanufaika wa Mkopo wa Elimu ya Juu, watakiwa kulipa ada kwa pesa zao ili wafanye mitihani ya muhula

KERO UDOM kuna changamoto ya baadhi ya Wanafunzi wanufaika wa Mkopo wa Elimu ya Juu, watakiwa kulipa ada kwa pesa zao ili wafanye mitihani ya muhula

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Wanafunzi hao wameshindwa kusaini malipo ya ada kwenye mfumo kutokana na changamoto za mfumo wenyewe, jambo hili linawafanya washindwe kufanya mitihani yao ya muhula huu ambayo inaelekea kuanza hivi karibuni, na endapo watataka kufanya mitihani hiyo watatakiwa kulipa ada kwa kutumia fedha zao za mifukoni.

Kila wakifuatilia jambo hili wanaambiwa linashughulikiwa huku siku zikiwa zinakwenda bila kuwa na majibu katika changamoto hii.

Tunaomba Bodi ya Mkopo kwa kushirikiana na chuo watatue kero hii kwa haraka hata kama wao hawatokuwa sehemu ya maumivu juu ya matokeo kwenye changamoto hii.

==================================
Screenshot 2025-02-14 165312.jpg
MAELEZO YA BODI YA MIKOPO
Mkurugenzi wa Habari, Elimu na Mawasiliano wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), Amani Kakana amezungumza na JamiiForums kuhusu hilo, amesema:

Mifumo ya Serikali inasomana, UDOM ni Taasisi ya Serikali kama ilivyo Bodi, hivyo ni suala la wao kutujulisha sisi kama kuna hiyo changamoto na itafanyiwa kazi.

Kuna njia na mifumo sahihi ya utoaji taarifa kwa Wanafunzi, wanapaswa kuwasilisha suala lao Chuo au Bodi ili lifanyiwe kazi.

Kama chuo kinasisitiza mhusisika alipe ad abasi mnufaika ana nafasi ya kuwasilisha malalamiko yake kwetu na yakafanyiwa kazi kwa mifumo ya Kiserikali.


UFAFANUNUZI WA UDOM
JamiiForums
imewasiliana na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Masoko wa UDOM, Rose Mdami kuhusu hoja hii, amefafanua:

Utaratibu upo hivi, kuna Wanafunzi ambao wanalipiwa 100% ya Mkopo kutoka Bodi, hao hawana tatizo, wanachotakiwa ni kujisajili tu na kuendelea na taratibu za mitihani.

Wapo ambao wanapata chini ya hizo asilimia, hivyo kiasi cha fedha ambacho kinabaki wanatakiwa kukilipa wao wenyewe Wanafunzi, tumeshatoa matangazo kupitia njia mbalimbali kuwataarifu kuhusu mchakato huo na wanaujua.
 
Back
Top Bottom