Tetesi: UDOM kupunguza programme degree za ualimu, sasa zitabakia nne tu


Kwa hiyo huwa unajaza tu facilities zilizopo bila Malengo wanafunzi wanatarajiwa kuelekea wapi?
 
Nini maoni kuhusu mpango huu wa wizara ya elimu?
Huko ni kutapatapa tu kwa serikali yetu. Kimsingi bado kuna uhitaji mkubwa sana wa walimu kote nchini, kutokana na ukweli kwamba hakuna uwiano sahihi kati ya mwalimu mmoja na wanafunzi ambao unatakiwa uwe 1:40/45 hivi.

Ni kawaida sana ukienda shule za serikali kumkuta mwalimu mmoja anafundisha watoto zaidi ya 100-300!

Ukija kwenye masomo ya sayansi, bado nako hali siyo nzuri! Na kinachoshangaza walimu wa msomo yote wamejaa mtaani hawana ajira! Huku serikali ikishindwa kuwaajiri ili kutatua changamoto ya upungufufu wa walimu kwenye shule zao, na pia kupunguza tatizo sugu la ajira kwa vijana na wasomi wetu.

Ushauri kwa serikali;
1. Ipunguze matumizi yake yasiyo ya lazima, ili fedha zitakazo patikana zikaajiri walimu.
2. Ipunguze mishahara ya wabunge na maafisa wake wa ngazi za juu ili fedha itakayopatikana ikaajiri walimu.
3. Iondoe yale mafao yasiyo na tija kwa wake/waume wa viongozi wa ngazi za juu ili fedha itakayo patikana ikatatue changamoto za elimu nchini.

Ila siyo kukimbilia tu kupunguza hizo course za ulimu kwenye vyuo vyake. Kwa sababu uhitaji wa walimu kote nchini, bado ni mkubwa.
 
Nimeshangazwa
Ni kawaida kukuta vijijini mwalimu mmoja anafundisha madarasa mpaka matatu peke yake tu

Wakati huo serikali iko busy na maturities ya hovyo kila mara

Nadhani shida sio hizi course shida ni mpango mbovu wa serikali tu
 
Maradhi ❌
Malazi βœ”

Kuna typo zingine ukizifanya (kama ni typo) unaharibu kila kitu!
 
Wangesimamisha kutoa degree za ualimu kwa sasa zikabaki za science tu
 
Bora wangefuta hiyo sijui mnaita ndaki resources hususan majengo etc zitumike kwa manufaa mengine.

Mfano, paboreshwe na kugeuzwa "Silicon Valley". Vitu vya maana vitoke pale tayari kupakiwa SGR for export.
 
BAEd na BED art ndio zinazojaza nyomi ya walimu hao wengine wanawaonea tu kwanza hizo course vyuo vingine havina
 
Hali ya wasomi ni tete kwakweli, leo nmeingia ofisi ya kata....yani watu waliokaa pale ofisini kwamba wapo field ni wengi kuliko hata wateja......

Ukiingia ofisi ni imejaa hadi unaona ngoja nisubiri nje wateja wapungue kumbe sio wateja. Ofisi moja watu 20 wamekaa pale πŸ™ŒπŸ™Œ

Inasikitisha
 
Hapa ndio umeongeaje

Wasimamishe za ualimu watoe za science kwani hakuna course za ualimu za science au zote zitolewe?
Degree za Arts zimekuwa nyingi Sana na mbaya zaidi hakuna walimu Competent .

Kwahiyo nashauri wasimamishe degree za ualimu kwa upande wa Arts zote Ila science iendelee
 
Kuna mambo hata sio ya MTU kupoteza muda kusoma kutokana na wakati tulionao .

Hizi course za utendaji n.k ni course za kisiasa Sana ambazo hazihitaji hata MTU kuzisomea .

Ningekuwa Mimi ni waziri nigekuwa nafanya hivi natafuta wanafunzi waliofanya vizuri form four unawapa training then unamkabidhi ofisi ya kata


Unamkalisha MTU chuo miaka 2-3 kwa Kazi ya kuandika barua , kutatua migigoro , kupiga muhuri na kusimamia shughuli za kimaendeleo za eneo husika


Tunatumia rasilimali muda vibaya Sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…