Udom: Wanafunzi wa info wanaokula ujasi wawekewa sumu na mmiliki wa cafeteria

UDOM SR

Member
Joined
Jan 25, 2014
Posts
47
Reaction score
26
Juzi wanafunzi wa UDOM waliobaki kwenye field katika college ya INFO (CIVE) wanaokula ujasi ya INFO waliwekewa sumu kwenye mpango ulioratibiwa na mzabuni anayeendesha cafeteria ya INFO.

Mchezo ulikuwa hivi: Baada ya kuona wakati huu wa likizo, mahudhurio ya wanafunzi kwenye cafeteria ya info yameshuka kwa kiwango cha kutisha ambapo wakati wa mchana wanafunzi wanaokula cafe hawazidi 20, Mzabuni wa cafe akishirikiana na uongozi wa chuo waliamua kwenda kubomoa vibanda vya ujasi ya info.

Baada ya kubomoa vibanda usiku, asubuhi yake walimpeleka mama mmoja ambaye alipika chakula na kukiwekea sumu ambayo baadaye ilikuja kujulikana na madaktari wa hospitali ya social. Yule mama alipika chakula na kukiwekea sumu ili wanafunzi wote watakaokula chakula waugue matumbo na ikiwezekena ipatikane hata "fatal case". Yaani wapatikane hata wanafunzi wachache watakao kufa ili wanafunzi waogope kabisa kwenda kula ujasi. Yule mama aliyekiuza chakula hicho inasemekana hajarudi tena pale ujasi. Wanafunzi wote waliokula hicho chakula wameharisha na kutapika mfululizo tokea juzi wengine wamelazwa pale social na wengine wanaendelea na matibabu hosteli. Hicho chakula kilipelekwa pale social kupimwa na kimegundulika kuwa na sumu ambayo iliwekwa kwa makusudi na siyo uchafu uliotokana na mazingira.

Chanzo cha Tatizo la Cafeteria ya Info:

Wanafunzi wengi wa info hawapendi kula kwenye cafeteria ya info kutokana na kudorora kwa huduma kwenye cafeteria hiyo. Ieleweke kwamba katika college ya info, mzabuni wa cafeteria yupo mmoja tu na hivyo hakuna ushindani ambao ungeweza kuboresha huduma. Chakula anapima kidogo sana kiasi kwamba hadi wasichana ambao inazoeleka wanakula chakula kidogo nao hawashibi. Wanaume ndio kabisa, ukitaka ushibe inabidi ule sahani 2 hadi 3. Malalamiko ya kupima chakula kidogo yameshapelekwa sana lakini hakuna marekebisho yaliyofanywa.

Mzabuni wa cafe anataka kuwaweka wanafunzi wa info mateka kuwa wakose altenative ya kula huku yeye akiendelea kuwauzia chakula kibaya na kidogo.

Kama Cafeteria zingekuwa zinasimamiwa na uongozi wa wanafunzi (UDOSO) yule mzabuni wa info angekuwa amefukuzwa zamani sana. Tatizo ni tenda za cafeteria kusimamiwa na chuo bila kushirikisha serikali ya wanafunzi ambayo ndiyo inayoelewa matatizo yaliyopo kwenye hiyo huduma. Lengo mahususi la cafeteria lilitakiwa liwe kutoa huduma kwa wanafunzi kwanza kabla ya kuangalia ukubwa wa faida. Sasa Chuo kimemwachia mfanyabiashara aendeshe cafeteria bila kumfanyia monitoring, matokea yake ni ame-monopolyze huduma ya chakula na kutengeneza channel za kuongeza faida hata kwa gharama ya afya za wanafunzi.

Semester iliyopita alipikia mafuta yaliyo-expire wanafunzi wakaharisha, eti serikali ya wanafunzi ikaandika barua kuwaomba msamaha wanafunzi kuwa itasimamia yale mafuta yasitumike tena. Alichokifanya baadae ni ku-blend yale mafuta yaliyoexpire na mafuta masafi ili kupunguza madhara. Ila in long-term ni kuwa cafe ya info bado tunakula chakula kilichopikiwa mafuta yaliyo-expire. Raisi wetu wa info amepewa chake katulia, funny enough ni kuwa wanafunzi wa info wamemchagua tena huyu raisi fisadi kuendelea kipindi kingine.

Huyu raisi wa serikali ya wanafunzi wa info amempa demu wake uwaziri, anatembea na yule muhudumu wa cafeteria mweupe mwenye matege anayegawa chakula upande ule wa choroko,"Disgusting". Anachowahadaa watu ni kujificha kwenye kichaka cha ulokole. Ndio maana mimi nazichukia dini sana maana zinawafunga watu kufikiri nje ya box.

Turudi kwenye mada: Vyuo vingine kama Ardhi na UDSM, Cafeteria zinasimamiwa na serikali ya wanafunzi kuanzia kwenye Tenda hadi kodi inaingia kwenye account ya serikali ya wanafunzi. Ndio maana matatizo ya cafeteria yanashugulikiwa mara moja. Ukienda pale ARDHI, unakuta cafeteria zaidi ya 5, ushindani wa biashara unafanya huduma iboreshwe. Sasa wenzetu wa kule COED-UDOM na social wana wazabuni wawili na ujasi, hivyo ushindani wa biashara umefanya huduma zao zimeboreka.

SULUHISHO:

Tunaomba kama Uongozi wa chuo kama umeshindwa kumfukuza huyu mzabuni wa cafe ya INFO, umpe zabuni mtu mwingine wawepo wazabuni wawili katika mwaka ujao wa zabuni. Ile cafeteria ina maeneo mawili ambayo yametenganishwa, (kule kwenye wali nyama na kule kwenye choroko). Tunaamini wakiwepo wazabuni wawili, huduma zitaboreka.

ANGALIZO:

Kuchelea kutatua haya matatizo ya chakula na kumwacha mzabuni akiendelea kuwalazimisha wanafunzi kula chakula chake kutakuja kusababisha maafa siku wanafunzi watakapoamua kufanya vurugu. Wanafunzi ni binadamu wanaofikiri, wametafuta njia za kutatua matatizo ya cafe kwa kula ujasi, Ujasi wamewekewa sumu na mzabuni ili kuwatisha na kuwakomesha, wakikosha channel ya kutatua matatizo yao wata-resort into desparate measures ambayo no one knows ita-end up vipi. Inaweza ikahatarisha hata maisha ya wafanyakazi walioajiriwa kwenye cafeteria. Ni hayo tu.
 
Mnamjua aliyewawekea sumu na bado hamtampa hata makwenzi mawili !
 
dah hiyo kali,polen kwa yaliyowakuta muache ubahiri sasa.Sie tulitoka salama mwaka 2011pia tulikuwa wadau sana wa wajasi
 
Ujasi ndo nini?
au hapa jamvini wote ni UDOM graduates?
 
Ujasi kwa tulio soma Udom ni jina linalotumika kwa mama lishe, yaani mama ntilie. Hawa ni akina mama wanaouza vyakula kando kando ya chuo kikuu cha Dodoma, wengine wako nje ya mipaka ya chuo wengine wako ndani wanauza kinyemela. Poleni sana bandugu.
 
UDOM ni chuo kinachosifiwa na serikali kwa nidhamu basi muwe wapole na wazalendo,hii ni nchi yetu sote."chukueni hatua"
 
Hana adabu huyo mzabun afungwe bila zamana shetan huyo hatakiwi kuigwa hata kidogo
 
Hapa ndipo napata shida nawasomi wetu kama wanashindwa kujisimamia wenyewe wataweza kuisimamia nchi? Haiwezekani mkajuwa mmewekewa sumu alafu mnaleta story humu jf badala yakufungua Kesi na sheria ichukue mkondo wake
 
Hivi huko Udom hamnaga uongozi wenu wa kufatilia haya mambo muhimu na afya za watu na kama huyo aliyeingia mkataba na cafeteria kama hana vigezo si abadilishwe awekwe mwingine
 
ila wajasi ni ngumu kuwazuia hasa info na humanities.... nikitoa education(ujasini)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…