kilimasera
JF-Expert Member
- Dec 2, 2009
- 3,068
- 277
MGOGORO katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), umeibuka upya baada ya wanafunzi wa Kitivo cha Sayansi ya Jamii kugoma kuingia madarasani jana kwa lengo la kuushinikiza uongozi wa chuo kutoa agizo la kuwaachia huru wanachuo wanaoshikiliwa na polisi.
Mgomo huo ulianza jana baada ya baadhi ya wanafunzi wa kitivo hicho kukamatwa na polisi huku ikidaiwa kuwa wapo wanafunzi walioumizwa kutokana na vurugu zilizotokea kati ya wanafunzi na Polisi juzi.
Akizungumzia suala hilo, Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Idrisa Kikula alisema wanafunzi wamegoma kuingia darasani huku wakidai hawawezi kuingia mpaka hapo uongozi wa chuo utakapowahakikishia kwamba waliokamatwa na polisi wameachiwa huru.
Profesa Kikula alisema pamoja na wanachuo kuandamana na kufanya mgomo kudai fedha hizo, ni wazi chuo kilishakaa na kuweka mikakati ya kuwawezesha wanafunzi wafanye masomo yao kwa vitendo.
Alisema kikao cha kwanza kilikaa Agosti mwaka huu, kujadiliana jinsi ya kupanga bajeti ya serikali kupitia Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), kuwawezesha kupata fedha kwa lengo la kufanya masomo yao kwa vitendo.
Sikiliza, kwanza katika masomo hayo ya vitendo, wanafunzi wanatakiwa kuwa na walimu wao hivyo ni lazima kuwepo na pesa kwa ajili ya wanafunzi na walimu wao tena suala hili lina utaratibu wake, siyo suala la kukurupuka tu.
Kunahitajika utulivu na mipango ya kueleweka, alisema Profesa Kikula. Hata hivyo, Profesa Kikula alitilia shaka mgomo huo kwa madai inawezekana umechangiwa na baadhi ya walimu, hivyo kuundwa kwa tume ya watu watano inayotakiwa kutoa majibu ndani ya siku saba.
Alidai kuwa iwapo watabainika watumishi wa chuo hicho kwa maana ya walimu, kuwa chanzo cha mgomo na migogoro, watachukuliwa hatua za kinidhamu haraka iwezekanavyo na wengine wanaweza kuachishwa kazi kwa mujibu wa taratibu na kanuni za kazi.
Jana, chuo kilikuwa katika ulinzi mkali ambapo kila kona kulionekana kuzingirwa na askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) huku kila askari akiwa na bunduki ya kurusha mabomu.
Wanafunzi 11 wanaodaiwa walijeruhiwa na Polisi wakati wa vurugu za juzi za kutaka kuandamana kwenda kwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda, kudai fedha za masomo kwa vitendo, waliruhusiwa kutoka hospitalini baada ya hali zao za kiafya kuendelea vizuri.
Kutokana na vurugu hizo, mawaziri walilazimika kufika chuoni hapo wakiwa na viongozi wote wa Mkoa wa Dodoma pamoja na maofisa usalama na kuwataka waandishi wa habari kutoweka katika eneo la chuo kwa madai kuwa wana kikao cha ndani, japo hawakuwa tayari kuzungumzia kikao hicho.
Viongozi waliofika chuoni hapo japo ilionekana kama siri ya chuo ni Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Shamsi Vuai Nahodha, wakiambatana na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk. James Msekela, Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa, Elizabeth Masanga na Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Betty Mkwasa anayekaimu nafasi ya Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini.