Udongo mtamu kwa wanawake Tanzania

Udongo mtamu kwa wanawake Tanzania

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363



Sasa kitu kichafu huenda kikaonekana si cha kuweza kupikwa, lakini ni kitu ambacho kinavutia katika maeneo mengi ya Afrika - hasa miongoni mwa akina mama wajawazito wanaohitaji virutubisho vilivyomo ndani ya udongo.
Nchini Tanzania kuna udongo maalum unaojulikana kwa jina la udongo wa pemba. Tulanana Bohela amesafiri hadi katika vilima vya vya Morogoro kujua udongo huo una ladha gani, lakini safari yake aliianzia katika soko maarufu la Kariakoo Dar Es Salaam
 
Last edited by a moderator:
Duh! mimi nilikuwa sijui kumbe unatoka Morogoro na Kigoma.Mwanzoni nilifikiri unatoka pemba!
 
Upungufu wa madini kama chuma, calciuma na magnesiuma ambayo ni muhimu kwa ukuaji wa mtoto aliye tumboni.

Nadhani mama anakuwa ananyonywa hayo madini na mtoto kwa sana, inamfanya atamani huo udongo.

Kwanini unapendwa zaidi na wajawazito?
 
Wa Morogoro sio mzuri sana, jamani wa Mwanza is the best

Wa moro una particle kubwa kubwa hivyo risk ya apendix kubwa, afu nadhani unatoka karibu na vyanzo vya maji au kuna unyevu unyevu mwingi, unakuwa na algae au sijui nini kwa ndani, kama una vitu unateleza teleza hivi, afu mchachu kama una ndimu.

Ila wa Mwanza msafi, fine particles hauna uchavu full maziwa na siagi

Duh! mimi nilikuwa sijui kumbe unatoka Morogoro na Kigoma.Mwanzoni nilifikiri unatoka pemba!
 
uuuwi............udenda umeanzakunitoka! nautamanije sasa!!!! mate yameshajaa mdomoni............aaarhg
 
mananikumbusha mamsapu wangu alipokuwa na ujauzito wa regina ilikuwa kero...udongo udongo.arrrrhg.
 
Back
Top Bottom