buhange
JF-Expert Member
- Oct 23, 2011
- 505
- 110
Kwa mara nyingine Tume ya uongozi wa wanafunzi(UDOSO) ngazi ya Shirikisho la Colleges zote wameendelea kushangaza Umma wa wana-UDOM na kuwaacha vinywa wazi, Ni ktk tukio lililotokea tar.26(jana) wakati wa kuaga mwili wa marehemu aliyefariki kwa kupigwa na radi tar.25/11 muda wa saa 3:00 usiku eneo la nje pale Cafteria ya MML. Sasa ktk hali isiyotarajiwa na wengi UDOSO-FEDERATION walitangaza kutoa 50,000 tuu wakimaanisha kuwa urefu wa kamba yao umekomea kwenye ELFU HAMSINI kama rambirambi yao ngazi SHIRIKISHO(Yaani "Baba" na "Kitovu" kikuu cha Viongozi wa wanafunzi ktk Colleges zote).Tume ya UDOSO- ktk College husika alipokuwa akisoma marehemu yaani SOCIAL SCIENCE wao walitoa 200,000 kama rambirambi yao. Umma wa wanafunzi wa SOCIAL SCIENCE wao walichanga Milioni moja na usheeeeeh! kwa moyo mmoja bila kujali hali ngumu ya maisha iliyopo ktk chuo hicho kwa hivi sasa.Mmmmh! Sasa Nini FEDERATION wanachomaanisha,hawana fungu zaidi ya hiyo pesa waliyotoa au bajeti ipo kwa ajili ya mambo mengine? maana siyo Leo tuu....imekuwa tabia yao kutoa fungu la ajabu ajabu.
MWANDISHI WA MAKALA HII SI MWANAFUNZI WA UDOM ILA ALIKUWEPO KTK ENEO LA TUKIO WAKATI WA KUAGA MWILI WA NDUGU YETU
MWANDISHI WA MAKALA HII SI MWANAFUNZI WA UDOM ILA ALIKUWEPO KTK ENEO LA TUKIO WAKATI WA KUAGA MWILI WA NDUGU YETU