Tanzania ya leo tuna tatizo moja KUBWA, nalo ni hili. Linapotokea tatizo au uvunjwaji wa sheria au suala lolote linaloonekana kuwa ni tatizo,basi solution au majibu au namna jinsi uamuzi unaotolewa ktk tatizo hilo huwa unakuwa ni TATIZO KUBWA kuliko hata tatizo lenyewe linalotatuliwa. Sasa mimi najiuliza, hawa wanaotoa maamuzi siku hizi, wanatumia nini kufikiri Kweli?? Tanzania tumekumbwa na nini?? Kuna mdudu gani kawaingia hawa wanaotoa maamuzi? au ndio matokeo ya ile Habari inayoendelea ambayo sasa iko PART 2? Hembu nijuzeni wanajamvi. Kwa sababu nacho kiona kinafuata ni hili: BORA wote tukose. Tusishangae tukaona hii mandhari nzuri ya maendeleo inayojichomoza sasa, ghafla ikawa ni magofu, ghafla tukasikia watua wanaanza kupotea, ghafla tukasikia mahali fulani siku hizi hakupitiki, ghafla tukasikia familia fulani fulani zimeshambuliwa. Hii yote ni kutokana na kushindwa KUFIKIRI kwa walio na nafasi za kutoa Maamuzi. Haya wee, endeleeni kuchochea tu moto na Petrol zenu.