tutafikatu
JF-Expert Member
- Dec 17, 2011
- 3,435
- 4,788
Competition kaka. 1 point 5 kwa PCM ni division 2 ya point kadhaa miaka ya 90.Habarini wana jukwaa.
Nimeona nije hapa jukwaani nitoe hili jambo, huenda nitapata ufafanuzi.
Nimekuwa nikikutana na malalamiko ya wanafunzi waliomaliza form 6 mwaka huu, wanaotarajia kujiunga na vyuo hivi karibuni. Wengi wao wanalalamika kuwa kila waombapo nafasi UDSM wanakataliwa, na wengine wanadiriki kusema kuwa vigezo sahihi wamekidhi kulingana takwa husika.
Sio mtaani wala mtandaoni ni malalamiko juu ya vijana na mabinti wanaotarajia kujiunga na Elimu ya Juu. Kuhusu Kukataliwa kuwa admitted hapo UDSM.
kuna huyu jirani yangu, yeye alisoma Ilboru Sec mchepuo wa PCM, kapata 1 ya 5, kachagua Udsm Course ya Civil Engineering, kakosa, bas analalama kila muda, hapa hata mie nimeshanga, huyu vigezo amekidhi kabisa, au labda huu mwaka 1 ya 3 na 4 ziko nyingi, hivyo inafanya wenye 5 na kuendelea wakose nafasi hapo COET?
Na Malalamiko ni kwa kila kada wanalalama mno, huku wakiwa na 1 zao nzuri, shida nn? Au utaratibu umebadilika hapo siku hizi? Kulikoniii?
Najua hapa kuna wafanyakazi, wana taaluma, wahadhiri, kutoka hapo UDSM, hebu mje mtoe ufafanuzi kutuondolea sintofahamu hii, maana huku uraiani hali ni mbaya watoto wanavurugwa vibaya, wakati ndoto zao ni kuwa hapo Mlimani main campus.
Tujuzweee kulikoniiiii?
HUjAeleweka hapa Mkuu rudia tena!!PCB one ya 5 mpaka 9 aliyeweka first choice doctor of medicine chuo cha MUHAS,kakosa chuo.Kwa sababu MUHAS wanaangalia first choice tu,other choices wanakuambia kabisa the selection wasn't runned.Wengi wameliwa kichwa hadi UDOM.
hapana mkuu,me nimemaliza form six 1939.H
HUjAeleweka hapa Mkuu rudia tena!!
Nyie sio Wanafunzi wa Mchonde kweli!?
in short kwa mwanafunzi wa PCB aliyepata chuo mwaka huu wapo wa aina tatuH
HUjAeleweka hapa Mkuu rudia tena!!
Assume 70% ya 1 ya 3 na 4 ya PCM nchi nzima waombe UDSM ( chuo pendwa) unahisi competition itakuwaje?Hata huyu wa CE? 1 ya 5? Ina maana huu mwaka 3 na 4 ziko za kutosha eeh?
Jina lako kule TikTok ni nani nimekuona juzi nishasahauYaan watoto wanavurugwa huku hatariii. Sasa kila mtu akitaka awe UDSM vyuo vingine watasoma kina nani? Dooh
Nimekusomz mkuuin short kwa mwanafunzi wa PCB aliyepata chuo mwaka huu wapo wa aina tatu
1.wanafunzi vipanga waliopata 3,4 na 5 baadhi
2.wanafunzi waliopata 7 mpaka 9,ila hawakung'ang'ania courses zenye competition kama doctor of medicine,DDS,pharmacy kwenye vyuo vikubwa kama MUHAS .
3.wanafunzi wa PCB waliokimbia course za afya na kuchagua computer sciences,accountancy.