Matemu
Member
- Nov 29, 2007
- 18
- 1
UDSM NA KUFUKUZWA KWA WANAFUNZI 2000
Utawala wa chuo kikuu cha UDSM kimetoa tamko la kuwafutia udahili wanafunzi wapatao 2000 kwa kile kinachodaiwa ni utovu wa nidhamu.Akizungumza mbele ya waandishi wa habari Makamu mkuu wa chuo hicho anayeshughulikia masuala ya Taaluma na Utafiti Prof.MABOKO hakufafanua kinagaubaga ni utovu upi wa nidhamu ambao umepelekea wanafunzi hao kutimuliwa chuoni.
Hata hivyo si lengo langu kujadili tamko hilo bali ni kuangalia namna Utawala wa chuo kikuu UDSM kinavyotoa matamko mengi kisiasa zaidi kuliko kiutendaji.KWA NINI NASEMA KISIASA KULIKO KIUTENDAJI?
1,Katika mgomo wa mwaka jana WAZIRI WA ELIMU Prof.Magembe alitangaza kuwafuti udahili wanafunzi wapatao 300 kwa kile kile wanachodai siku zote Utovu wa nidhamu.Hata hivyo agizo hilo halikutekelezeka kwa sababu ambazo hatukuelezwa na kuishia kusipojulikana.
2,Siku zote Uongozi wa chuo unapotangaza kufukuza wanafunzi chuoni ama kuwafutia udahili ni kwa nini hawatangazi majina yao hadharani badala yake huishia na matamko tu ya tumewafukuza? Maboko ama Magembe wanatakiwa kuwa na majina kwanza halafu ndiyo watoe hayo matamko yao BADALA YA KUONGEA TU NA KUWAWEKA WANAFUNZI ROHO JUU NA WAZAZI WAO KWA UJUMLA.
Ikumbukwe kuwa wanafunzi 2000 kwa chuo cha UDSM ni karibia asilimia 13% ya wanafunzi wote hivyo si jambo la mzaha la kuongea tu bila kutaja majina yao.KWA USHAURI TU KAMA WANATAKA KUTISHA WANAFUNZI NI BORA WAKATUMIA NJIA NYINGINE ZAIDI KULIKO HII YA MATAMKO YA KUFUKUZA WANAFUNZI.

Last edited by a moderator: