Mdau, ninavyo jua mimi kwauzoefu wangu wa chuo, sikuzote boom huwa halitoshi hata liongezwe vipi. Nachojua mimi hali ya boom kwa wanafunzi sasa ni nzuri ukilinganisha na miaka ya kuanzia 2005/06 na kurudi nyuma. Pili ifahamike kuwa accomodation ya mtaani siku zote ni cheap kulinganisha na ile ya chuo kwa upande wa kifedha. Lakini kwa upande wahuduma accomodation za chuo ni very very cheap kuliko za mtaani kwani unatumia umeme utakavyo, maji utakavyo, na ikitokea hitirafu mnagoma mambo yanawekwa sawa.
Pamoja kuwa kunamatatizo vyuoni nimuhimu kutizama kwa umakini sana, sometimes wanafunzi hugoma kwa sababu za kipuuzi sana huwezi amini. Wanafunzi wanaweza kugoma kwasababu ya kufeli mitihani, sasa utajiuliza walitaka wapewe marks za bure ili wote wafauru?. Hivyo ni vema kujua kiini chake then tutachangia mawazo. Hivyo ndivyo njuavyo mimi.