Udsm,tcu na tma tunaomba ufafanuzi juu ya course hii,huu ni ubaguzi wa wazi kabisa

Ngalikivembu

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2010
Posts
1,959
Reaction score
876
TCU ndio chombo kinachohusika kwa sasa kuchagua wanafunzi wote wanaotarajia kujiunga na vyuo vikuu hapa nchini kupitia mfumo rasmi unaoitwa CAS. Kwa utaratibu uliowekwa kwa sasa, ina maana hakuna mwanafunzi yeyote atakayejiunga na chuo chochote nchini kuchukua shahada ya kwanza bila kupitia katika mfumo huu. Hii imewezesha kuziba mianya ya kudahili wanafunzi wasio na sifa. Wote wenye kujua hali ya nchi yetu atakubaliana nami kuwa huu kwa sasa ni mfumo mzuri ambao hauna malalamiko kwa wananfunzi kwani ni wa haki katika utendaji kazi wake. Mwaka huu mpya wa masomo 2013/2014 Chuo kikuuu cha Dar es Salaam kimeanzisha programu mpya ya shahada ya kwanza katika masuala ya hali ya hewa. Programu hii kwa mujibu wa kitabu cha mwongozo cha TCU mwaka huu wameshaonyesha programu hii ikiwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi 15 tu kwa sasa.Na programu hii itachukua miaka 3 na mkopo katika course hii ni “Priority” na hata mkopo wake wote utalipiwa na bodi, ikimaanisha kuwa atakayechaguliwa hapa, atalipiwa asilimia 100 na HESLB. Kwa tangazo hili, mwanafunzi yeyote mwenye sifa anaruhusiwa kuomba. Na course hii kwa mwanafunzi atakayeomba ina maana ataajiriwa na Mamlaka ya hali ya hewa Tanzania kwani ndio mwajiri mkuu.Hakuna popote kwa sasa mhitimu atakapoajiriwa nje na TMA. Huwezi kuanzisha programu ambayo wahitimu wake hawawezi hata kujiajiri wenyewe. Kuna wanafunzi kadhaa niliwashauri waombe course hii kwani nilijua kuwa inatoa ajira ya moja kwa moja na mshahara wake ni mkubwa ndani ya mamlaka hiyo. Mapema mwezi wa nne Mamlaka ya hali ya hewa ilitoa tangazo kwa wafanyakazi wake kuwa Chuo kikuu cha Dar es salaamu kwa kushirikiana na mamlaka itaanzisha course hii.Pale ambapo mipango itakapokuwa imekamilika basi itawatangazia tena wafanyakazi ili wale wenye sifa(Physics and Matheamtics) waombe kupitia mamlaka. Wakati tunasubiri kutolewa kwa tangazo hilo, ghafla tunaletewa barua kuwa watu wameshachaguliwa kujiunga na shahada hiyo, tena watu 15. Sasa kwa barua hiyo na mwongozo wa TCU, ina maana ile idadi ya wanafunzi wanaotakiwa kujiunga na course hii tayari wameshatosha. Hapa kuna maswali ya kujiuliza katika hili, Je wanafunzi ambao wamekwisha omba course hii hawatachaguliwa tena hata kama wana sifa zinazohitajika? Na kwanini hawa wafanyakazi hawakuomba kupitia TCU kama sheria inavyotaka? TCU inaweza kuwaambia wanafunzi wasiombe tena course hii kwani tayari wanafunzi wa kusoma wameshapatikana?Je huku si kuwanyima haki watanzania na kuwakosesha ajira ya moja kwa moja?Kama wanaostahili kuomba course hii ni wafanyakazi wa mamlaka ya hali ya hewa, kwanini TCU waliorodhesha katika kitabu chao kupitia chuo kikuu cha Dar es Salaam?Kama kulikuwa na tangazo kusema kuwa course hiyo wanafunzi wasio kwenye ajira wasiombe, naomba nijulishwe. Yaani kuna watu wanajiunga na chuo kikuu bila kupitia TCU!!? Kama TCU wana ubaguzi basi wawaeleze watanzania.Naamini kabisa TCU na Chuo kikuu cha Dar es Salaam hawajafanya haki kwa watanzania wanaoteseka kila leo kutafuta ajira.Hii ilikuwa nafasi nzuri sana kuwasaidia wanafunzi wa kike waliochukua masomo ya sayansi. Lakini pia ukibahatika kuiona listi ya waliochaguliwa kujiunga na chuo hicho hawana sifa.Na kwa mtazamo wangu hii ndio sababu iliyowafanya TMA kuchagua wafanyakazi kwa njia isiyo halali kwani wasingeweza kushindana na wanafunzi wenye sifa. Kilio changu ni kuwa kuna haki ya watanzania wengine imenyang’anywa.Chuo kama cha Dar es Salaam kwanini kimekubali kudhalilika kwa namna hii? Watanzania wenzangu tuseme hapana kwa utaratibu huu.Watoto wa walalahoi wamenyimwa haki yao.Tuchukue hatua.TCU itoe ufafanuzi wa hili.
 
Mkuu punguza stress aisee..inawezekana hao walioomba sio direct from form six labda wametumia mature age entry au qualifications zingine..diploma etc..sasa ki kawaida nafasi ya waliohitimu kutoka form 6 itakua pale pale tu mkuu..usiwaze sana ni kufikiria nje ya box..tu..!!! hata kama wameandika 15..haifanyi direct from school wakose nafasi..mkuu..over..!!!
 
Hakuna mature age entry.Najua mature age utaratibu wao.Hapo wewe unataka kutetea kuminywa kwa haki.TCU inakaribisha maombi kuanzia waliomaliza shule baada ya 1987.Unadhani kwanini waliandika hivyo?Hakuna cha mature age, kwanza kuna process ya kupitia mfumo huo.Kwa mfano ili ukubaliwe mature age entry ni lazima upite mwaka toka ulipoomba kujiunga.Mimi mwenyewe niliwahi kutaka kuingia kwa mfumo huo lakini nilipoona utanichelewesha nikaamua kuachana nao.
 
Ni kweli hapo kwenye udahili kuna utata,Ila naomba nizungumzie kwenye suala la ajira za moja kwa moja;Sio 'guarantee' kupata ajira ya moja kwa moja kwenye serikali ya TZ (japokua kwenye sekta ya afya,kilimo na elimu huwa sometime wanatoa),serikali ya TZ haina mipango endelevu,Nasema hivi kwa sababu mimi nafahamu kua hii serikali yetu ya TZ imekua ikisomesha watu wengi nje ya nchi na ndani ya nchi kwa kutumia mabilioni ya pesa lakini inakua shida kuwapatia ajira,..Tena kwa zile kozi za kwenda kusoma nje ya Nchi serikali imekua ikiziita 'priority' kwamba ukisoma na kurudi utaajiriwa serikalini (wakiamini kua kusoma kwenye vyuo vya nchi zilizoendelea mtu atakua na kitu fulani cha ziada),.lakini watu wamekua wakipelekwa nchi mbalimbali kusoma shahada mbalimbali na wanarudi Bongo hawapatiwi hizo ajira,.wanaishia kuzeeka tu bila hata kua na kazi za maana(maana kozi zenyewe nyingi ni za kuajiriwa serikalini zaidi).Mimi nashauri fanya utafiti wa kozi yoyote ambayo una uwezo wa kuisoma vizuri na yenye 'future' nzuri ktk ujumla wake ili utakaposoma na kumaliza iweze kukusaidia utakapoanza harakati za kuachakarika nayo mtaani kukupatia chochote kitu.
 
Hakuna mature age entry.Najua mature age utaratibu wao.Hapo wewe unataka kutetea kuminywa kwa haki.TCU inakaribisha maombi kuanzia waliomaliza shule baada ya 1987.Unadhani kwanini waliandika hivyo?Hakuna cha mature age, kwanza kuna process ya kupitia mfumo huo.Kwa mfano ili ukubaliwe mature age entry ni lazima upite mwaka toka ulipoomba kujiunga.Mimi mwenyewe niliwahi kutaka kuingia kwa mfumo huo lakini nilipoona utanichelewesha nikaamua kuachana nao.

Nina wasiwasi na uelewa wako kuhusu mature age entry. Hebu jaribu kupitia tena sifa za mature age entry.
 
Back
Top Bottom